Kamanda wa Polisi Mbeya ACP Kuzaga afunga "Polisi Jamii Interclasses Super Cup"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,970
12,289
Kuzaga 1.JPG

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamini Kuzaga Machi 25, 2023 huko katika Kata ya Kisiba iliyopo halmashauri ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya alifunga mashindano ya mpira wa miguu na ngoma za asili yaliyojulikana kama "POLISI JAMII INTERCLASSES SUPER CUP 2023"

Akifunga mashindano hayo, Kamanda Kuzaga amewataka wanafunzi na wananchi wa Kata ya Kisiba kutokomeza uhalifu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Mkaguzi Kata wa Jeshi la Polisi aliyepangiwa kazi katika Kata hiyo.
Kuzaga 2.JPG

Aidha, amewataka viongozi wa kimila na wazee waliopo Kata ya Kisiba kukemea vitendo vya ubakaji na ulawiti ambavyo awali havikuwepo kwa wingi kama ilivyo sasa. Amewaomba kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa elimu kwa wananchi na kukemea matendo hayo ya aibu, yanayokiuka utu wa mwanadamu na ambayo ni kinyume cha sheria za nchi.

Naye Diwani wa Kata ya Kisiba Mhe. AMBAKISYE MWAKANYAMALE kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Kisiba amelishukuru Jeshi la Polisi na kupongeza utendaji kazi wa Mkaguzi Kata ya Kisiba A/INSP.MENG’ANYI kwa namna alivyombunifu na kwa ushirikiano mzuri na uongozi wa Kata na wananchi kwa ujumla.
Kuzaga2.JPG

Mashindano ya mpira wa miguu ya Polisi Jamii katika Kata ya Kisiba yalianza rasmi Machi 07, 2023 na kushirikisha timu nne cha kidato cha kwanza hadi cha nne kutoka Shule ya Sekondari Kisiba.

Mashindano ya ngoma za asili yalishirikisha vikundi nane vya ngoma ya Iseselo, Isabula, Kibundugulu, Ikama, Ikomelo, Mambwe, Magosi na ngoma ya Kitum kutoka vitongoji na vijiji vilivyo ndani ya Kata ya Kisiba.
Kuzaga 3.JPG

Mashindano ya Polisi Jamii Interclasses Super Cup yameratibiwa na Mkaguzi Kata ya Kisiba A/INSP.DEOGRATIUS MENG'ANYI kwa kushirikiana na Diwani wa Kata, Mtendaji wa Kata, Wadau, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisiba na wananchi huku akieleza lengo la mashindano hayo kuwa ni kuwaleta pamoja wanafunzi na wananchi kupitia mchezo wa mpira wa miguu na ngoma za asili.
 
Back
Top Bottom