Kite Munganga
Platinum Member
- Nov 19, 2006
- 1,773
- 952
ya anaitwa Liberatus Lyimo Barrow,ni mchaga ndiyo na huwa ana jaziba sana katika kutoa maamuzi,kamanda Simon Nyakoro Sirro amepandishwa cheo na kuwa Naibu Kamishina Wa Polisi yaan Deputy Commissioner of Police,ni tofauti ya cheo kimoja tu cha Kamishina ndo unamfikia IJP,ni mpiganaji na anajua kusoma alama za nyakati,hana upendeleo wa kikabila wala kikanda,ni kipenzi cha askari na wananchi. alijiunga na Jeshi mwaka 1992 alipomaliza shahada yake ya kwanza ya sayansi ya elimu - Bachelor of science with education pale UDSM,alihudhuria kozi ya ukaguzi msaidizi wa polisi na baada ya kumaliza alipangiwa kuwa mkuu wa upelelezi wa kituo cha buguruni na baadae akahamishwa kuwa mkuu wa upelelzi kituo cha Magomeni baada ya kupandishwa cheo na kuwa mrakibu msaidizi wa polisi-assistant superintendent of police. Alifanya kazi pia mkoani Tabora kama naibu mkuu wa upelelzi mkoa wa Tabora na baadae akahamishiwa tena Dar kuwa naibu mkuu wa upelelezi mkoa wa Dar. Alihamishiwa Shinyanga kama mkuu wa upelelezi mkoa na baadae akawa kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga. Alihamishiwa baadae mkoani Tanga km kamanda wa polisi wa mkoa na baadae mkoani mwanza kama kamanda wa polisi wa mkoa. Amepandishwa cheo na pia kuhamishiwa makao makuu ya polisi kama mkuu wa kitengo cha operesheni maalum ndani ya jeshi la polisi! Mungu amjalie maisha mema na marefu!
Asante sana mkuu....(lakini mie nimeomba Background ya Barow), Huyo Sirro tunamjua toka akiwa UDSM akiwa mtu makini darasani na nje katika jamii iliyomzunguka,