Kamanda Nzowa ajitokeza, ataja mchungaji anayejihususha na dawa za kulevya

Raisi hatakiwi kulipigia hadithi jambo kama hili, badala yake ilikuwa ni kutoa amri wakamatwe na kuwekwa ndani na mashtaka kufunguliwa. Mpaka yamefika kwake na kuona yanafaa kuyaweka kwenye hotuba ina maana uchunguzi ulikuwa umekamilika na pale alitakiwa awataje jina na angeliarifu maaskofu kuwa nimeagiza wakamatwe na kufikishwa mahakamani. Nchi haiendeshwi kimajungu majungu!
Kwani alisema wanaohusika hawatachukuliwa hatua? kwamba akimaliza kuhutubia ndio hao wauzaji mihadarati wanakuwa 'wamesamehewa dhambi zao'? Mi sioni hoja hapa.
 
na Mch. Sheikidola Omarisegun Obilemehi, huyu ana sura saba zenye jinsia mbili tofauti na paspoti za mataifa mbalimbali, ni jitu la hatari sana! Bado hajakamatwa....popote utakapomuona toa taarifa kwa kamanda nzowa au kituo cha polisi kilicho karibu nawe.


Next utasikia Mch. Olesagugan Okumakumborochetu KanuokochauchwekafirimkubwaZowa... Mtu anakamatwa na madawa ya kulevya red handed, exhibit kipo open, anaachiwa, unaishia kumtaja jina tu, what is this? yaani jokes kibaooooo, i am tired na uzembe mkubwa huu wa uongozi
 
Hii apelekewe mkurupukaji Mokiwa, asikae mbali chakula kinaiva majina yatabwangwa pwaaa mbele yake na atakimbia ofisi.
Wewe kila mtu mkurupukaji basi nafikiri hata baba yako alikurupuka kukuzaa ndiyo maana akili hazikutoshi.
 
Mi napata shida sana kuamini maneno ya polisi kwa sababu ni wabambikizaji wazuri. Angalia sakaka la Mwanza askari kurushiana makonde wakigombea Madawa ya Kulevya (Mirungi) ilivyopotezewa.
 
Yupo gereza gani tukamzoomee!
kama yuko Kempinsk hotel nasi tukaambulie kitu kidogo, daah!
 
Na wamemchukulia hatua gani? Hai2shi ku2ja, muhimu ni kusimamia mkondo wa sheria!
 
Mi napata shida sana kuamini maneno ya polisi kwa sababu ni wabambikizaji wazuri. Angalia sakaka la Mwanza askari kurushiana makonde wakigombea Madawa ya Kulevya (Mirungi) ilivyopotezewa.
Afu ndo zao hawa askari njaa wa tz, wanakamata madawa ya kulevya wanawauzia raia. Hawayaangamiz wala nini. Na ndo mana watuhumiwa huwa hawachukuliwi hatua zozote. Kama huku Ar, askari akikukamata na bange au mirungi mnagawana nusu kwa nusu then anakuachia uende zako je hili jk halijui
 
Saa 48 zinakaribia kwisha,wengine please,tunataka kuwajua,hatutaki kuambiwa hilo dhehebu lina makao makuu nigeria,bado halijasajiliwa tz,duh!
 
1.jpg


Kiongozi mkuu wa wauza Misuba according to JK
 
Saa 48 zinakaribia kwisha,wengine please,tunataka kuwajua,hatutaki kuambiwa hilo dhehebu lina makao makuu nigeria,bado halijasajiliwa tz,duh!
Wengine watoke wapi? Huyo aliyetajwa mwenyewe hayupo sayari hii. Zitaisha mpaka saa 72 hutasikia akitajwa mtu. Hv umesahau usanii wa hii SERIKALI ya jk?
 
Kesi ipo mahakamani na inaendelea. Hajasema kama yupo rumande au nje. Ametaja dhehebu, lina jina refu kama dawa ya ukoma...


Mkuu hapo kwenye red kidogo unisababishie umauti! Nimecheka saaaana, nusura nizimie! Long Live JF!:becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky:
 
Next utasikia Mch. Olesagugan O****kumborochetu KanuokochauchwekafirimkubwaZowa... Mtu anakamatwa na madawa ya kulevya red handed, exhibit kipo open, anaachiwa, unaishia kumtaja jina tu, what is this? yaani jokes kibaooooo, i am tired na uzembe mkubwa huu wa uongozi

Mheshimiwa "Rais" acha matusi!
 
Labda nishereheshe maneno yako ni kwamba taasisi nyingi za dini na NGO's zinatumika sana ktk usafirishaji na uingizaji wa Unga nchini na taarifa inajieleza wazi kwamba Tanzania na Kenya (Mombasa) ni uwanja mkubwa wa transit ya biashara hizi kwenda Ulaya kama ilivyo Mexico na Canada kwa unga unaoingia Marekani. Jana tu nilikuwa nilisoma ktk gazeti moja kwamba biashara ya Unga Marekani inaingiza Billioni 360 kwa mwaka wakati biashara ya Microsoft kwa mwaka ni billioni 50. Na ile ya Afghanstan (Heroin) leo hii wana supply asilimia 65 ya unga duniani compared to asilimia 17 wakati wa Taliban..Mind you Cocaine na Heroin (Opium) ni vitu viwili tofauti.

Hawa Wanigeria (wageni) hawakuja nchini kutangaza imani ya dini na wala hatuhitaji kufundishwa dini na Wanigeria kwa sababu Ukristu ulikuwepo nchini hata kabla hawa jamaa hawajafika na tuna madhehebu makubwa yanayotoa elimu ya dini na mwisho wa yote Biblia ndio elimu yenyewe na inapatikana tena bure. Hawa watu hawakuja nchini kuitangaza dini bali wamekuja fanya biashara haramu baada ya Tanzania kuwa kiwanja kikubwa...

Kama tunavyokemea Ugaidi wakuu zangu tusiwe wepesi sana kutoa hukumu ikiwa rais atakemea viongozi wetu wa dini ambao kanisa navyosikia wana KINGA na wanatumia nafasi hiyo kama mabalozi na mawaziri wetu kusafirishia unga na money laundry.. Kumbukeni tu kwamba biashara ya Unga na money laundry vinachangia kwa kiasi kikubwa sana mfumko wa bei hasa ktk nyumba na mashamba.

Wewe mkulima na mfanyakazi unapotaka kununua nyumba ya thamani ya Tsh 40mil anatokea muuza unga na kutoa Tsh 100, kesho jirani akitaka kuuza nyumba atachukua bei ilouzwa jirani yake. Na ndio ilivyotokea Kariakoo na sehemu nyingi nchini kutokana na biashara haramu za unga. Jirani yako ataendesha Range sports na wewe mtumishi wa Umma utaingia tamaa na kuanza kuiba ili mradi uwe na gari au nyumba kama ya muuza unga.

Tuachane na hisia za Udini ktk kulijenga Taifa kwani vita hii haiwezi kuishia makanisani na misikitini bali kila kitu kina mwanzo na haiwezekani kuzungumzia swala hili pasipo Hassan na Richard kuhusika. Na tabia hii imetuathiri hata ktk chaguzi za viongozi wetu kwa sababu siasa za Tanzania zimefikia kiwango ambacho dini ya mhusika kuwa CV ili kuleta uuwiano sijui tukiwakilisha kitu gani..Maana hachaguliwi Muislaam kusimamia Waislaam wlaa hachaguliwi kiongozi mkristu kusimamia maslahi ya Wakristu, sasa kuna sababu gani ya kutafuta uuwiano ktk ajira za viongozi wasiosimamia imani hizo!
 
na haya makanisa nayo menginewe ni ya kimagumash tuuu! mitume,manabii wanamovogue na mabenki hivi sadaka zetu ndo source za luxury zote hiziii? af na hawa kina nzowa nao dawa wakishka wanapeleka wapi?!!!na kesi mbona znapotelea jukwaju? wanauhakika na wanachokinena kuhusu maaskofu? bora wangetaja askofu muhusika kuliko kuwajumlisha!!!! na wewe okochuku rudi kwenu vijana wetu tunawahitaji kwa taifa la sasa.shindwa na ulegee.........
 
Kwani alisema wanaohusika hawatachukuliwa hatua? kwamba akimaliza kuhutubia ndio hao wauzaji mihadarati wanakuwa 'wamesamehewa dhambi zao'? Mi sioni hoja hapa.

Narudia tena Mkuu, kama Raisi hawezi kutolea amri jambo la hatari kwa Taifa kama hilo baada ya kuwa limechunguzwa na amepelekewa ripoti ya upelelezi kutoka kwa wataalamu basi hiyo ni balaa!!! Ina maana anawaonea haya? Kwanini? Hapo hakuna kitu porojo tupu. Ndiyo maana maamuzi ya serikali hii huwa hayaeleweki. Ni ya kufumba fumba wananchi tuuu! Nakuahidi utafika mwaka 2015 bila hatua yoyote madhubuti kuchukuliwa.
Siyo mpaka mwanao apigwe dhoruba ya mhadarati ndiyo ukubali kuwa serikali ilizembea!
 
JK acha kutuzingua huyo mpopo alikuja kufanya biashara na si kama kiongozi wa dini, alitumia tu gia ya uchungaji

...ndio maana Mkuu ameagiza watumishi wa kiroho wakemee!

... the core of the Nigerian drugs dealers cum 'born again faithful of churches of later day evangelism' can squarely be traced back into the gates of the Nigearian Commission in Dar in the form of dirty diplomats facilitating their relatives, kin and friends in such lucrative get rich quickly schemes by taking into adavantage, vivid porousity and other loopholes in our systems!

...well said!

SIJUI kama huyu mtu alishawai kuishi Tanzania

pamoja na uchungaji wake hakuna hata gazeti moja lililomuandika? kwanini alipokamatwa na coceine 81 hakuna chombo cha habari kulichotoa habari hii????? wizi wizi wizi mtupu
:glasses-nerdy::glasses-nerdy::glasses-nerdy::glasses-nerdy:

...Loh, hukuiona hii?




RAIA wanne wa kigeni, Dennis Okechukwu na Paul Obi wote wa Nigeria, Stani Hycenth wa Afrika Kusini na Shoaib Muhammad Ayaz kutoka Pakistan wakitoka kusomewa mashitaka ya kula njama na kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya sh. bilioni 2.8, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam

Source: Habarileo
Wageni wadaiwa kuingiza Heroin za bilioni 3/-

na hapa; http://www.ippmedia.com/frontend/?l=26806
 
Back
Top Bottom