Kama wewe ni kijana mwenye umri usiozidi miaka 22, na una ubunifu au uvumbuzi wa hali ya juu tayari na unatafuta fedha za mradi wako fuatilia uzi huu

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,819
18,557
  • Soma vizuri hadi mwisho na ujaze fomu iliyowekwa mwishoni kabla ya mwisho wa mwezi February.
  • Researchlink International (www.researchlinktz.com) itatoa msaada wa kitaalam wa ku-apply kuongeza uwezekano wa kufaulu.
Kuna fursa nzuri ya kupata fedha kutoka kwa kampuni ya Thiel Foundation. Kampuni inatangaza fursa ya kupata $100,000 ambazo ni karibu TShs 250,000,000 hivi.

Fedha hizo zitakazotolewa kwa washindi ni kwa ajili ya fellowship, ambapo vijana wenye mradi waliokwisha anzisha lakini wamekwama katika jambo fulani watapatiwa usaidizi wa fedha na mafunzo ili waweze kujiendeleza zaidi katika wazo au mradi wao.

Thiel Foundation wanataka uwe na wazo la kipekee sana ambalo linawezekana kufanyika na kuleta manufaa katika jamii. Wazo lako liwe ni la ubunifu wa hali ya juu sana juu ya kitu kinachoshikika au mfumo e.g. mfumo wa computer, mawasiliano, n.k. au chochote kile cha kiteknolojia.

  • Unapaswa kuwa na umri usiozidi miaka 22, sio lazima uwe shule na ukiwa shule (college) na ukapata fellowship hii unaweza kulazimika kusimamisha masomo kwa muda hadi fellowship iishe.
  • Vijana waliokwisha kupata degree ya kwanza hawapaswi kufany application!
  • Fursa hii ni kwa wale vijana wadogo, watundu sana na wenye akili na wazo kubwa la ubunifu wa hali ya juu katika jambo lolote.
  • Usilete wazo uliloiga kwingineko kama vile kuiga kutengeneza helcopter, simu au kitu kingine; wazo lako liwe original na lenye ubunifu wa kitu kipya au mfumo mpya wenye manufaa kwa jamii.
  • Wazo liwe la kwako peke yako na sio shirika na mtu mwingine
  • Uwe tayari ulishafanya kitu na sio wazo tupu la kufikirika
Kampuni ya ResearchLink International itawasaidia kuapply. Unapaswa kuonesha interest yako kwa kujaza fomu hii: Google Forms: Sign-in. Unaweza kujaza fomu hii kwa Kiswahili pia.
 
Back
Top Bottom