Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Wakati akifunga mjadala wa bajeti ya wizara ya Fedha ya mwaka 2023/2024 waziri Mwigulu alinukuliwa akiwaambia wabunge kuwa, kama ripoti ya CAG inadai kuwa pesa nyingi zimeibiwa serikalini, je pesa yote anayoitoa Rais Samia kwenye miradi mbalimbali nchini, angezitoa wapi, iwapo pesa nyingi zimeibiwa serikalini?
Akauliza pia, kama Rais Samia ametoa pesa nyingi zaidi kwenye miradi mbalimbali, kuliko Rais mwingine yeyote, tokea nchi yetu ipate uhuru wake mwaka 1961, je hao Marais wengine waliowahi kuongoza nchi hii, pesa za nchi hii, walikuwa wakizipeleka wapi?
Kiukweli ni kuwa katika hotuba yake ya kufunga bajeti ya wizara ya Fedha ya mwaka 2023/2024, waziri Mwigulu Nchemba, alitumia sehemu kubwa ya hotuba yake, akitoa sifa kemkem Kwa Rais Samia na kuwaomba watanzania kuwa Mama anastahili kupewa maua yake, hadi nikajiuliza hivi waziri Mwigulu, amekuwa ndiye "chawa" mkuu wa Rais Samia Suluhu Hassan??
Kwa tafsiri nyingine, ni kama waziri Mwigulu alikuwa akimanisha kuwa Marais wote, waliowahi kuongoza nchi hii, ndiyo walilkuwa "wapigaji" wa pesa za nchi hii na Rais Samia Suluhu Hassan, ndiye Rais ambaye utawala wake hauna ufisadi hata kidogo!
Je nini maoni yako mwana JF