Kama unataka paa lako liwe imara tumia mbao za mlingoti

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
24,988
33,625
Kwenye ujenzi bhna kuna mambo ukikosea utakuja kujilaumu sana baadae.

Hizi mbao mnazoambiwa ni treated ni wizi mtupu,
Mbao za pine pia ni laini sana, mafundi wanazipenda sababu ya urahisi wa kunyoosha.

Ila kama unajielewa tumia mlingoti kwa sababu 2.

1. Utapunguza gharama kubwa sana ya mbao. Mfano, fundi akikwambia nyumba yako inataka mbao 100 za 2x4 na mbao 100 za 2x2, wewe cha kufanya nenda dukani nunua mbao 50 za 2x6 peleka mashineni uchaniwe katikati zitoke 2x3 tayari umepeta mbao 100, hizi kwa kenji ni balaa unakuwa umempita mbali sana kwa uimara na alieweka kenji za pine za 2x6

Kwenye zile za papi 100 unachukua mbao 30 za 2x6 unachana mara 3 zinatoka mbao 90 za 2x2, umemaliza kazi.
Mbao ya mlingoti ya 2x6 inauzwa sh. 8,000 mpaka 9,000 kwa Dar. Ukipiga hesabu hapo utakuwa umeokoa hela nyingi sana.

2. Utaepukana na mbao kuliwa na wadudu!

Mlingoti hauliwi hovyo hovyo na wadudu

NB: Kupaulia mlingoti unahitaji upate fundi kweli kweli na umsimamie kwenye unyooshaji, vinginevyo nyumba inakuwa na vibyongo.
 
Kwenye ujenzi bhna kuna mambo ukikosea utakuja kujilaumu sana baadae.
Samahani, hiyo mbao ya 2x6 inachanwa vipi mpaka inatoa 3x3!? Maana kwa uelewa wangu mdogo ingeweza kutoa 2x3 au nyinginezo lakini sio 3x3.
 
Samahani, hiyo mbao ya 2x6 inachanwa vipi mpaka inatoa 3x3!? Maana kwa uelewa wangu mdogo ingeweza kutoa 2x3 au nyinginezo lakini sio 3x3.
Ndiyo mkuu.. Inatoa 2x3
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom