Kama unamuona Hakimi ni hatari, Basi wacha nikujuze kuhusu huyu mwamba

Mchagah

JF-Expert Member
Sep 8, 2021
488
926
Dunia haitomsahau Gabriel Villa, mwanasheria kwa taaluma aliyefanya pia kazi ya uwakala wa usafirishaji.

Bwana huyu mwaka 1994 alikutana na mwanadada mrembo Christina Carta kwenye sherehe

Wawili hawa wakapendana na hatimaye kufunga ndoa licha ya kuwa Gabriel alimzidi mrembo huyo miaka 30.

Tajiri huyo mara tu baada ya kufunga ndoa alimpeleka mkewe nchini Jamhuri ya Dominica kwenye visiwa vya nchi hiyo kula maisha kwa miezi minne.

Na waliporudi waliishi pamoja kwenye ndoa ya furaha kubwa kwa miaka 20.

Baada ya miaka hiyo ishirini ya kuishi pamoja hatimaye wawili hawa waligombana na Mwanamke akaenda kudai talaka kisheria ili wagawane mali.

Lakini baada ya kufuatilia taratibu hizo za kisheria, Wanasheria wa Mwanamke huyo walimjulisha kuwa bwana Gabriel alimtaliki mke wake huyo miaka 20 iliyopita bila yeye kujua hivyo kwa miaka yote hiyo hawakuwa wanaishi kwenye ndoa.

Kumbe bwana, ile fungate bwana Gabriel aliyompeleka mkewe nchini Jamhuri ya Dominican alitumia pia mwanya huo kuandikisha talaka kabisa kwa mkewe bila mwenyewe kujua kwani kwa wakati huo ni nchi ya Jamhuri ya Dominican pekee ndiyo iliyokuwa inaruhusu kisheria talaka kutolewa bila mmoja wapo kujua.

Mwamba huyu alipoulizwa alisema alijua kuwa siku moja Mwanamke huyo angetumia mbinu ya kudai talaka ili kuchukua mali zake hivyo alijiandaa mapema

NDUGU YETU HUYU ANAPASWA KUPEWA CHEO GANI?
 
274150b9-8766-4e9c-9d42-4f1c2091953f.jpg
 
Kumbe Hakimi Ni Cha mtoto kwa Gabriel Villa🤔

Hii Dunia Ina watu werevu Sana kwa kweli.

Kuna mwamba mwingine huko uzunguni ilimtaliki mkewe kimasihara Sana, unaambiwa jamaa alikuwa anafukunyua mafiles akakutana na barua ya kimapenzi aliyoandikiwa mkewe miaka 45 iliyopita na mwanaume mwingine.

Licha ya huo muda mrefu kupita jamaa hakusita kutoa talaka kwa mkewe.

Hii Dunia Ina mengi maajabu!
 
Back
Top Bottom