mwalimu nyerere alituonya
kutaja majina kabla ya sifa...... sijui lakini kwa vile umetulazimisha
kutaja majina basi nadhan kwa sasa labda mwakyembe!!!
Sisi tuna mupigia
upatu Dr slaa ndiye candidate wetu wa rais 2O15.CCM tunaomba mutupe jina
moja tu la mtu munaye ona anafaa kua rais kutoka chama chenu musitupe
majina mengi tunaomba jina moja tu
"Kwa nini tusifikirie majina kama haya:
Emmanuel Nchimbi
Zitto Zuberi Kabwe
John Mnyika
January Makamba
William Ngeleja
Nape Nnauye
Halima Mdee
n.k
Afazali Zitto mi namkubali, Lakini hawa wengine mmmmh.... Mungu apishie mbali
Kiukweli nionavyo mimi viongozi ambao wanafaa kuliongoza taifa letu kwa 2015 ni wafuatao:
1. William Ngeleja (Mr Megawatt)
2. Zitto Kabwe
3. Dr Mwinyi
4. Shamsi vuai Nahodha
Uzuri wa hawa jamaa wako smart, waelewa, wazalendo, si wanafiki, ni wakweli, ni wachapakazi na wana misimamo, hawababaishwi na ushabiki wa kisiasa. Aida, ni watu wenye hekima na watulivu, hawana jaziba kwa umma hata kama wanashutumiwa.
Vinginevyo ni majanga matupu!
Mimi kama Mtanzania mpiga kura ,siwezi kumpigia kura Slaa ikiwa atakuwa mgombea wa Uraisi kupitia Chadema.Huyu ukiangalia ana tatizo la ndoa,unaweza kusema ni private lakini haikubaliki kuwa hivyo ,kwani kuiba au kuchukua mke wa mtu na kuzusha kuwa alitalakiwa na kuitumia nafasi hiyo kuwa wako ,huko siko na si kweli kwani bado kuna kesi au ilikuwepo kesi. wacha yote hayo lile tendo la kuchukua mke wa mtu hadi kufikishana mahakamani si la kiungwana na halikufaa kuwepo kwa mgombea Uraisi.
Slaa hafai kuwa mgombea kwani hili jambo limemuengua kimaadili ,inaonyesha hana maadili mema ,na hata kuukimbia Upadre nalo pia ni suala la kuwa si mtu mwenye msimamo ,zaidi ni mwenye kuonyesha dalili za mtu mwenye tamaa na asieridhika.
Ingawa anaonyesha ni mpiganaji hodari katika duru za kisiasa ,yeye ni bora angebakia hukohuko kwenye ngazi za chini za ubunge na nyinginezo Uraisi kwa mtu wa aina hii ni mwiko na hafai kabisa.
Sasa hayo majina kwenye red si ni vituko tu hapa jamvini au unataka umefanya balance kwa vyama vikuu nchini,afadhali kwa ccm ungemweka mtu kama Filikunjombe ningekuelewa mkuu."Kwa nini tusifikirie majina kama haya:
Emmanuel Nchimbi
Zitto Zuberi Kabwe
John Mnyika
January Makamba
William Ngeleja
Nape Nnauye
Halima Mdee
n.k
Afazali Zitto mi namkubali, Lakini hawa wengine mmmmh.... Mungu apishie mbali
Mkuu wanatajwa wengi tu:
Dr. John Pombe Maghufuli
Mr. Membe
Mr. Six
Mr. Sumaye
Mr. Mwinyi
Ms. Tibaijuka, nk.
Mkuu analysis yako ni nzuri kwa hao watu uliowataja lakini bahati mbaya hujatuwekea umri wao ifikapo October 2015 ambao ni mwezi wa uchaguzi.
Matatizo yangu ni kwamba watu humu JF tumekuwa tukisema wazee wetu ni vyema wakapumzika kama tulivyotoa maoni kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Lakini linapofika suala la Urais tunawaangalia watu ambao wako beyond 60 years! Hawa wanatakiwa wawe wameenda kupumzika baada ya kuutumikia umma (Najua urais hauna retirement age).
Nadhani kwa mantiki ya kutaka vijana watwae madaraka basi ni vyema wakatwaa na Urais pia. Ningefurahi kuona wana JF wanakuwa chachu katika hili kwa kuwapendekeza vijana na si wazee ambao wanatakiwa wawe washauri tu kama mzee Mtei, Kisumo, nk.
Ningefurahi kuona tunawapigia chapuo vijana na wala si babu zetu (najua wana JF wengi ni .com na Tab).
Kwa nini tusifikirie majina kama haya:
Lakini wawe of age but below 60 years by October 2015. Kila siku wazeee wazeee. Ni muda muafaka wa kutafuta vijana na kuwakabidhi mikoba. Ila wasiwe wavuta shisha tu!
- Emmanuel Nchimbi
- Zitto Zuberi Kabwe
- John Mnyika
- January Makamba
- William Ngeleja
- Nape Nnauye
- Halima Mdee
- n.k