Kama Pilato alikiri Yesu ni Mfalme wa Wayahudi kwanini alimsulubisha? CHADEMA someni kwa Busara Uamuzi wa Jaji Mkeha!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,038
Wayahudi walimpeleka Yesu mbele ya Pontio Pilato shtaka kuu likiwa "alijifanya ni Mfalme wa Wayahudi".

Pontio Pilato alitumia mbinu nyingi kutaka kumnusuru Yesu lakini ilishindikana baada ya Wayahudi kujiapiza kuwa Damu ya Yesu na iwe juu yao na vizazi vyao.

Mwisho Pilato akawakabidhi Yesu wakamsulubishe LAKINI cha ajabu Pontio Pilato akaandika Juu ya Msalaba "Huyu ni Yesu wa Nazareth Mfalme wa Wayahudi" na Wayahudi wakashangilia sana.

Nimesoma kwa sehemu uamuzi wa Jaji Mkeha Juu ya Shauri la Halima Mdee na wenzake na nimeona pahala anasema "Uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA ulikuwa sahihi".

Ndio najiuliza kama Uamuzi wa Kamati Kuu ulikuwa sahihi, huo Usahihi unaishia wapi?

Kama Kamati Kuu ilikuwa Sahihi maana yake kuna kipindi fulani kabla Covid-19 hawajakata Rufaa walikuwa siyo Wabunge. Kwa kifupi Jaji apewe maua yake!

CHADEMA itisheni Baraza Kuu msameheane Taifa lisonge mbele.
 
We bwashee ile Iesus Nazarenus Rex Iudaeorum (INRI) nijuavyo mimi ni cheo cha kejeli. Kwamba wakati huo Roma ikitawala hapo Pilato kama gavana wa Judea mwajiriwa wa Tiberius asingeweza kumuita mtu mwingine mfalme.

So ni kama alimwona Yesu ni chizi ikabidi tu ampe hiyo title ya yesu mnazarthi, mfalme wa wayahudi.

Sidhani kama ina relate.
 
Hii hukumu hata huyo Jaji mwenyewe anaishangaa sababu naye kakutana nayo mahakanai imeandikwa na Tulia, kazi yake ilikuwa ni kuisoma pekee kama ilivyoandikwa
 
Back
Top Bottom