Kama ni wewe ungefanyaje?

Aug 18, 2019
80
177
Majambazi waliingia nyumbani Kwa Jamaa,, wakauliza pesa na mikufu ya dhahabu ipo wapi?

Jamaa akawaonyesha sehemu zilipo.

Baada ya kukusanya kila kitu mle Ndani kile wanachoweza kubeba, Hali ikawa hivi:

Majambazi wakampa Baba mwenye nyumba Bunduki Kwa maelekezo ya kumpiga mkewe Risasi za kichwa la sivyo yeye mwenyewe apigwe risasi afe.

Baba mwenye nyumba akaichukua Bunduki, anaielekeza kichwani kwa mkewe, lakini Rohoni mwake akaingiwa na roho ya majonzi, hivyo alisita kufyatua Risasi.. Hakumpiga risasi Mke wake.

Kwa maana alifikiria namna walivyoishi vizuri na mkewe Kwa Miaka mingi,. alifikiria mambo ambayo amepitia maishani na mkewe na jinsi mkewe alivyoteseka na kujitolea kwa ajili yake.

Ndipo yule Baba mwenye nyumba akairudisha Bunduki Kwa Majambazi na kusema.

"SAMAHANI SIWEZI KUMUUA MKE WANGU KWA KUFYATULIA RISASI. Siwezi kumuua mke wangu.

Basi yule mkubwa wa majambazi akamnyang'anya bunduki yule Baba mwenye nyumba na kumpa mke wake.

Jambazi Akamwambia yule Mwanamke "chukua hii Bunduki mpige mmeo Risasi za kichwa .. la sivyo wewe mwenyewe utauwawa Kwa kupigwa risasi.

Ndipo yule Mwanamke akachukua ile Bunduki Kwa yule mkubwa wa Majambazi na bila kusita sita hata dk moja anaelekeza Bunduki kichwani Kwa mmewe na anakavuta risasi ili ampige mmewe kichwani.

kumbe yule Jambazi hakuweka Risasi yoyote kwenye ile Bunduki. Bunduki haikuwa na hata risasi hata moja.

Majambazi wakachukua Bunduki yao wakaingia kwenye Gari wakaondoka huku wakicheka na hakuchukua hata kitu kimoja.

MASWALI YA MAJADILIANO

1. Je, ingekuwa wewe ndio mwanaume katika nyumba hiyo ungemchukuliaje Huyo Mwanamke wako?

2. Je, ingekuwa wewe ndio mwanamke Katika nyumba hiyo, ungemwambia nini Huyo Mwanaume wako?

3. Je, ingekuwa ndio umeitwa kuleta amani kati ya wanandoa hawa, Kama wewe ungetoa ushauri gani kwao?
 
Nahama nyumba muda huo huo naambatana na majambazi uelekeo Bar kuwashukuru kwa kunionesha jambazi la ukweli lililo ishi karibu yangu kwa muda mrefu.
Km ni game lilipangwa ili watake chance yako je?

Na ukihama uzee wote huo utaishije?
 
Ningefanya "maridhiano" tu kama wale jamaa kule Visiwani pamoja na roho na mali za watu kupotea. There is no time to be bitter in life, talk about it, forgive or be forgiven
 
Back
Top Bottom