Kuna jamaa mmoja hapa mtaani ambae ni ndugu wa mbatia nilimdadisi kuhusu nduguye kupewa ubunge buuure, wakati ni mpinga sera za ccm, akanijibu kwamba mbatia mara nyingi toka akose ubunge na kufuta kesi aliyoona angeshndwa aliamua kuwa karibu na JK kwa kumpigia simu mara kwa mara kuomba afikiriwe nafasi ya uongozi wa kuteuliwa hasa ubunge. Ili kujitengenezea mazingira mazuri zaidi jamaa akawa ndo mshauri asiye rasmi wa JK na kumpelekea maneno yote kutoka kwa viongozi wengine wa ccm wanaomsema vibaya au kumjulisha juu ya utendaji mbovu wa watu kadhaa.
Ndani ya maongezi yao, tetesi zinasema kwamba Mbatia amekuwa akimwambia JK kiutani "Mh.. Tazama, wenyeviti wenzangu wa vyama vikubwa kama TLP, CHADEMA, UDP ni wabunge kasoro mimi tu.. Naona aibu, nakosa hata confidence ya kuongea, pia sina mahala pa kuongea nijenge chama. Pia tazama ulivyowajali CUF, umewapa urais usaidizi huko zenji.. Mheshimiwa nikonside na mimi, nisipotee kisiasa pia nipate hata huto tuposho"
Haya wadau ni tetesi kuhusu Mbatia. Kwa heshma ya Jamvi nawasilisha.
..mods mambo mengine usiwe unapost humu yanachefua