kama ni kweli ulitumia njia hii kupata ubunge, baasi Mbatia umechemka..

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,283
976
Kuna jamaa mmoja hapa mtaani ambae ni ndugu wa mbatia nilimdadisi kuhusu nduguye kupewa ubunge buuure, wakati ni mpinga sera za ccm, akanijibu kwamba mbatia mara nyingi toka akose ubunge na kufuta kesi aliyoona angeshndwa aliamua kuwa karibu na JK kwa kumpigia simu mara kwa mara kuomba afikiriwe nafasi ya uongozi wa kuteuliwa hasa ubunge. Ili kujitengenezea mazingira mazuri zaidi jamaa akawa ndo mshauri asiye rasmi wa JK na kumpelekea maneno yote kutoka kwa viongozi wengine wa ccm wanaomsema vibaya au kumjulisha juu ya utendaji mbovu wa watu kadhaa.

Ndani ya maongezi yao, tetesi zinasema kwamba Mbatia amekuwa akimwambia JK kiutani ”Mh.. Tazama, wenyeviti wenzangu wa vyama vikubwa kama TLP, CHADEMA, UDP ni wabunge kasoro mimi tu.. Naona aibu, nakosa hata confidence ya kuongea, pia sina mahala pa kuongea nijenge chama. Pia tazama ulivyowajali CUF, umewapa urais usaidizi huko zenji.. Mheshimiwa nikonside na mimi, nisipotee kisiasa pia nipate hata huto tuposho”

Haya wadau ni tetesi kuhusu Mbatia. Kwa heshma ya Jamvi nawasilisha.
 
Duuu haya tena na ya jussa kupewa ubunge. Na bado tutasikia mengi wadanganyika sie.
 
...JK anatekeleza masharti ya Cameroon ya kuzitambua haki za watu wa aina ya Mbatia. Msiumize vichwa bure,JK anataka misaada toka kwa Waingereza. Walisema asitambua haki za hao watu watakata kutoa misaada
 
jamani hii habari sio ya great thinkers ni ya wambeya wa vichochoroni! hivi leo Kikwete angeamua kumteua Dr. Slaa kuwa mbunge kuidhihirishia dunia ukomavu wake tungesema Slaa ni kibaraka wa ccm? Habari yenyewe inaonyesha ina wivu na uchungu jambo ambalo sio sahihi kwa great thinkerS. kumbuka kwama SMALL MINDED PEOPLE huwa wanajadili mambo ya watu! naoma modds muanzishe SMALL MINDED PEOPLE FORUM!!!!!!!!!!!!!!!
 
...JK anatekeleza masharti ya Cameroon ya kuzitambua haki za watu wa aina ya Mbatia. Msiumize vichwa bure,JK anataka misaada toka kwa Waingereza. Walisema asitambua haki za hao watu watakata kutoa misaada
Huu ni wivu usiokuwa na maana kabisa. Hata mleta thread naye anaonekana ni mbea tu. Kwani katiba inamtaka Kikwete ateue mbunge kutoka CCM peke yake? Wakati mwingine watanzania mmezidi mno kwa gossips, hamtaki kutumia akili zenu kufikiria wala kufanya research ili mseme kile ambacho mna uhakika nacho mnabaki tu na kauli za "labda", "tetesi", "inasemekana", "pengine", "nimesikia", "habari za kuaminika" na mengine kibao ya uzushi mtupu! Kama hamna ushahidi wa mnachokisema nyamazeni. Mlitaka mteuliwe ninyi? Au mlitaka wateuliwe watu wenu? Kikwete katimiza haki yake kikatiba, na Mbatia ni mtanzania kama wewe na mtu mwingine ambaye katiba inamruhusu kuteuliwa, sasa oooh, inasemekana, ooh, ukameroon, haya yote yanatoka wapi? Ungeteuliwa wewe tungesema nini?
 
JF siku hizi imekuwa kama KIJIWE CHA KAHAWA...kitu chochote mtu anachowaza anakuja ku post..
 
Back
Top Bottom