ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 44,005
- 50,733
Nimekuwa najiuliza swali na kuharibu kutafiti ni mambo yapi au vitu gani spesho ambavyo vinavuta Mamilioni ya watalii kutoka Nchi mbalimbali Duniani Kutembelea Nchi za Kaskazini mwa Afrika za Egypt, Morocco na Tunisia? Watu wanatoka Duniani kote kwenda kutumia mabilioni ya pesa huko, Kunani hasa? Nikatafuta kufahamu.
Yaani majibu niliyopata yamenishangaza sana.Kwamba kinachowapeleka watu kwenye hizo Nchi ni Magofu ya kale (Majengo chakavu ya tawala za kale),beaches na labda eti Pyramids.
Nikajiuliza zaidi na kuchimba ndani ni mambo hayo tu? Na Je idadi kubwa ya Watalii wanatoka wapi? For the case of Tunisia wengi wanatoka Algeria na Libya, Kwa Morocco wanatoka Ulaya hasa Spain na Egypt Kwa sehemu kubwa ndio wanatoka maeneo mbalimbali.
Maswali Yanayonitatiza.
Kwamba Utalii ni Magofu na Beaches na sio Nyumbu au vifaru. Yaani watu Wana shida na Magofu zaidi kuliko Wanyama ambao kutwa kucha tunafunga watu Wetu eti ni vivutio vya Utalii.
Nikaendekea kutafakari na kujiuliza, mbona Tanzania tuna Magofu ya kale ya kutosha tuu mfano Stonetown Zanzibar,Bagamoyo, Kilwa, Ismani nk? Hao Watalii mbona hatuwaoni Kwa Wingi? Kwani Magofu wanayokuja kuangalia yanatakiwa kuwaje?
Mbona Tanznaia tuna beaches nzuri kushinda wao na kubwa kuanzia Mtwara Hadi Tanga? Zanzibar yote na Maziwa yote Makuu? Mbona hatuwaoni wakija Kwa Wingi Kuchezea,kupiga picha na kuingiza aunkufanya matamasha?
Hata South Africa ambao nao Wana Wanyama kama sisi ,idadi kubwa ya Watalii wao hawaendi kuangalia Wanyama Bali ni majirani wanaokuja Kwa Ajili ya biashara,fukwe na wachache ndio wanakuja Kwa Ajili ya Wanyama.
Maswali.
Kama Utalii unaobamba Duniani kote hauhusiani na Wanyama Wala misitu Kwa nini mambo haya yanafanyika?
1. Kwa nini Serikali inafuata Vijiji,kunyang'anya watu maeneo Kwa kisingizio Cha Uhifadhi na kuwa kivutil Cha Utalii ambacho sio kitu watalii wanakipenda?
2. Kwa nini tutumie mabilioni ya pesa kuhamishia watu kwenye maeneo Yao Kwa kisingizio Cha Utalii ambao sio bidhaa ambayo Watalii wanahitaji?
3. Kwa nini tuwafunge watu Wetu miaka jela Kwa sababu eti za kukutwa na vipande vya Wanyama pori,tuwalipishe faini,mazao Yao yanaharibiaa na Wanyama nk? Huo Uhifadhi una faidia ipi Kwa jamii wakati sio kati ya mazao ya Utalii yenye soko Duniani?
Hitimisho.
Ni vyema Serikali ikajitafakari Kwa hayo niliyoeleza hapo Juu Kwa sababu tunakomaa na kuumiza jamii yetu Kwa vitu ambavyo havina faida Kwa watu Wetu labda kuwafaidisha Wazungu.
Kama tunataka Utalii tuweke Nguvu kwenye mazao ambayo Watalii wanataka na sio kuhangaika na Wanyama.
Tujiulize Kwa nini tuna fukwe nyingi na Magofu ya kutosha lakini hakuna watalii wa maana wanaokuja.
Mwisho tukuzee Utalii wa ndani Kwa Kuinua uchumi wa watu na pia tuishi vyema na Nchi Majirani na kukitangaza kwao maana hao ndio Watalii Wetu wa uhakika badala ya kuhangaika na WA Ulaya ambao wanaenda Kwa majirani zao.eg Cuba, Malta nk
View: https://twitter.com/AfricaFactsZone/status/1751212698614858037?t=PPV0rMBdm6kh-f_vFn_oXg&s=19
Wenye Magofu na fukwe wanapata watalii kati ya Milioni 9-15 na wenye Mbuga za Wanyama Wana pata watalii kati ya Milioni 1-5.Tutumie akili.