Kama Lowassa alitabiriwa na TB Joshua kuwa Rais TZ, Iweje sasa atumie Pesa kukampenia Urais?

Mlipomtema,mngefuata utaratibu tu ila mkatumia ubabe sasa mnalia nini? Hivi ni vyama Vingi au mlisahau? Mwacheni mzee wa watu aangalie plan B

Huyo tumemtema kwa fikra zake za kuwa kila Mtanzania anaweza kumnunuwa kwa fedha zake, leo kathibitisha kuwa anaoweza kuwanunua ni wachagga tu.
 
Kwan lowassa alikua cdm akahama na kurudi cdm ndio mseme cdm inakula matapishi yake? Kwa cdm ni mwanachama mpya izo mambo za matapishi sijui zinatoka wapi,ccm ndio mnachanganyikiwa akili.
 
Wewe unayemtukana mtumishi wa Mungu unajipalia mkaa wa moto. Angalia maneno yako ndiyo uzima au mauti kwako.
 
Wewe unamsikiliza porojo zake? waliotemwa wote hakuna hata mmoja alisema utaratubi haukufatwa, yeye kama nani zaidi mgonjwa mwenye uchu wa madaraka?

Mnaonishangza ni nyinyi mnakunywa matapishi yenu? Kulikoni?

Leo ndiyo nimejuwa mchagga kwa pesa anaweza kula matapishi yake.

Mwandosya kaanza kusema na yeye
 
mh Edward lowasa alionekana amehudhuria kwa mchungaji Joshua na kutabiri kuwa raisi wa tanzania je utabiri utatimia kupitia ukawa baada ya kukatwa na ccm.au ndo utakuwa mwisho wa kumwamini TB JOSHUA na Gwajima ule utabiri wake pale Arusha lowasa alipotangaza safari ya matumaini.
 
Jibu la utabiri analo aliyetabiri (Tb Joshua), sisi kujibu hilo swali utakuwa unatuonea. Labda kama tusubiri hakimu wa haki (muda) utakapowadia, ndipo tutatoa jibu la kama umetimia au hajatimia.
 
mh Edward lowasa alionekana amehudhuria kwa mchungaji Joshua na kutabiri kuwa raisi wa tanzania je utabiri utatimia kupitia ukawa baada ya kukatwa na ccm.au ndo utakuwa mwisho wa kumwamini TB JOSHUA na Gwajima ule utabiri wake pale Arusha lowasa alipotangaza safari ya matumaini.

Hakuna siku TB Joshua ametabiri Lowasa atakuwa rais kama mna udhibitisho wekeni clip.
 
Katika moja ya vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano TZ, kuna mbunge mwanamke alimfagilia sana E. Lowassa; na pia gazeti moja la kila wiki nchini lilimnukuu mbunge huyo mwanamama kutoka Tanga akisema alipoenda Nigeria aliambiwa na Mtumishi maarufu wa mungu nabiiTB Joshua kwamba mh.Lowassa ndiye rais ajaye wa Tanzania.

Sasa inakuwaje tunasikia katika makundi ndani ya CCM(mafisadi) kundi lake ndilo hutumia fedha kwa kiasi kikubwa ili kupenyeza watu wake kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya chama na serikali; huku yeye Lowassa akijiandaa kugombea urais kwa tiketi ya ccm kwa kutumia fedha? Je, hauamini unabii uliotolewa juu yake na TB Joshua? Kwa nini amsaidie mungu kukamilisha unabii wake? Au huyo, mbunge mwanamama alikuwa mzushi tu?
Lowasa21.jpg

Mh. E. Lowassa akiwa Nigeria akishiriki ibada katika SOAN na mwenye kipaza sauti ni nabii TB Joshua
mwaka jana.

Mwacheni Mungu aitwe Mungu!.

Edward Ngoyai Lowassa ndiye rais wa tano wa JMT!.

Pasco
 
Mwacheni Mungu aitwe Mungu!.

Edward Ngoyai Lowassa ndiye rais wa tano wa JMT!.

Pasco

Pasco umerudi na speed kubwa sana!.,maana lowasa alivyokatwa ukawa mdogo kama piriton na pia ukaanza kutetea threads zako za nyuma ukisema ''lowasa sio lazima awe raisi'',,mara ''president could be J.P Magufuli '' nk,,anyway karibu kwenye muda wa mabadiliko
 
Back
Top Bottom