Kama Lowassa alitabiriwa na TB Joshua kuwa Rais TZ, Iweje sasa atumie Pesa kukampenia Urais?

M.L.

Senior Member
Feb 11, 2012
185
119
Katika moja ya vikao vya bunge la Jamhuri ya Muungano TZ, kuna mbunge mwanamke alimfagilia sana E. Lowassa; na pia gazeti moja la kila wiki nchini lilimnukuu mbunge huyo mwanamama kutoka Tanga akisema alipoenda Nigeria aliambiwa na Mtumishi maarufu wa mungu nabiiTB Joshua kwamba mh.Lowassa ndiye rais ajaye wa Tanzania.

Sasa inakuwaje tunasikia katika makundi ndani ya CCM(mafisadi) kundi lake ndilo hutumia fedha kwa kiasi kikubwa ili kupenyeza watu wake kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya chama na serikali; huku yeye Lowassa akijiandaa kugombea urais kwa tiketi ya CCM kwa kutumia fedha?

Je, hauamini
unabii uliotolewa juu yake na TB Joshua? Kwa nini amsaidie Mungu kukamilisha unabii wake? Au huyo, mbunge mwanamama alikuwa mzushi tu?

Lowasa21.jpg

Mh. E. Lowassa akiwa Nigeria akishiriki ibada katika SCOAN na mwenye kipaza sauti ni
Nabii TB Joshua mwaka jana.

 
Hata Shekh Yahaya alitabiri mwisho wa dunia ila ilipofika hiyo siku tukasikia amekufa yeye mwenyewe.

Huyo TB ni wale tunaoambiwa ktk vitabu vitakatifu kuwa ni manabii wa uongo.

T2015CDM
 
Hajawahi kutabiriwa kuhusu uraisi, msichafue watumishi wa Mungu bure.

Tupe link ya huo utabiri kama unayo!
 
Pamoja na yooote, huu upepo dhidi ya EL utapita na safari yake kwenda kupanga Magogoni itatimia bila ya kutegemea utabiri wa Joshua au utabiri wa kiumbe mwingine yeyote..... Chezea nguvu ya Laingwanani nyie..../^^^>>>???
 
Utake usitake ukweli ni kwamba Hon. Lowassa ndiye rais wa Tanzania 2015. Acha chuki binafsi, Lowassa hatumii rushwa bali anakubalika kutokana uchapa kazi wake.
 
Rais wa vibaka na waizi wenzie sio watanzania,hizo bora angetumia kusafiri mapema kuihama nchi
 
Urais tuu mtu unakwenda TB joshua! Dhaifu alikuwa analindwa na majini ya marerehemu sheikh yahaya!
namshauri Lowassa aende kwa Anton lusekelo mzee wa upako au aende kwa mtume na nabii Mwingira.
 
Hainiingii akilini kwa mtu mwenye fikra ya kawaida kutumia muda kuzungumzia habari za Lowasa kuwa rais. Inakuwaje watu kuzungumzia mtu anayetumia pesa nyingi kutafuta ikulu (rejea hotuba ya Nyerere). Inakuwaje watu kuzungumzia urais kwa mtu aliyeshindwa hata kumaliza kipindi kimoja cha Uwaziri Mkuu, tena aliyefukuzwa kwa kashfa mbaya ya ufisadi!!!!
Tunahitaji kama vija kuhoji uzalendo wetu na uwezo wetu wa kufikiri. Teupuke kuwa makuwadi wa Mafisadi. Ni dhambi mbaya. Epuka kutumika.
 
Hakuna ushahidi uloshawahi kutolewa kuhusu ufisadi wa Lowasa, hizo zilikuwa plan za mahasimu wake kimdhoofisha kisiasa lakini zimeshindwa. Hao wanampinga lowassa mbona hawapendekezi majina mengine? au ndo mahasimu wenyewe. Kimsingi hakuna anaeweza kuvaa kiatu chake.
 
Be careful and alert, you the hopeless majority. For these are the very times that the manipulative and clever few will manipulate your dead minds to foster their lust.
 
unashangaa nini, mbona hata jk walisema ni chaguo la mungu?
Leo wanatamani kumeza maneno yao.
 
unashangaa nini, mbona hata jk walisema ni chaguo la mungu?
Leo wanatamani kumeza maneno yao.

Lowasa ananuka rushwa, hakuna mtanzania asiejua.
Bora sita au membe kuliko lowasa.
 
Back
Top Bottom