Kama kwenye mitandao ya kijamii wanapiga kelele matukio haya yangefanikiwa bila uwepo wa Mitandao ya Kijamii?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Wakuu,

Waziri Nape alitoa kauli hivi karibuni akisema watu waliokuwa kwenye mitandao ya kijamii wanapiga kelele tu na kwamba wapiga kura na wale wanaojielewa wanafanya mambo mengiine mtandaoni lakini sio kutumia mitandao ya kijamii.

Haya ni baadhi ya matukio ambayo mitandao ya kijamii ilisaidia pakubwa kuyafanikisha;

Uchaguzi wa Rais wa Marekani mwaka 2008

Mwaka 2008 timu ya Rais Obama iliweza kuingiza mitandao ya kijamii kwenye mkatati wao kampeni na kumshinda mpinzani wake John McCain.

Obama alishinda karibu asilimia 70 ya kura za Wamarekani walio chini ya umri wa miaka 25 kwa kufanikiwa kukutana na wapiga kura kwenye majukwaa ya Facebook, YouTube na blog mbalimbali

Kila ambacho kilikuwa kinafanyika nje ya mtandao kwenye kampeni zilizopita mfano kuwasiliana na watu wa kujitolea kwenye shughuli za kampeni, kupata michango ya kuendesha kampeni, kuandaa mikutano na kutangaza sera zilifanyika mtandaoni,

Uchaguzi huu ulisababisha kuibuka kwa “watumiaji wa mtandao wa kiasiasa” na ulionesha 74% ya watumiaji wa mtandao walikwenda mtandaoni kipindi cha uchaguzi kutafuta habari na taarifa mpya zilizokuwa zinatoka.

Tetemeko la Ardhi Haiti mwaka 2010

Maudhui yaliyotengenezwa na watumiaji wa mtandao wa Facebook na Twitter (sasa X) yalisaidia kwa kiasi kikubwa kusambaza habari kuhusu Tetemeko kubwa la Ardhi mwaka 2010

Wakati watu wengi walikuwa wakitegemea habari kutoka kwenye vyanzo vya habari kama redio, TV na magazeti, kulikua na upungufu wa habari kutoka kwenye maeneo yalioathirika. Watu waligeukia kwenye mitandao ya kijamii kupata taarifa mubashara lakini pia kuhamasisha watu kutoa msaada

Katika uhamasishaji wa watu kutoa michango, watumiaji wa mitandao ya kijamii waliweza kutuma ujumbe maalum wa maadishi “Haiti” kwenye namba maalum ya Msalaba Mwekundu ambapo dola 10 ilikuwa inaongezwa kwenye bili yao na kufanikiwa kukusanya michango ya Dola milioni 8 ndani ya siku chache

Harakati za kampeni ya Black Lives Matter baada ya kifo cha George Floyd mpaka leo

Baada ya video tukio la mauaji ya George Floyd mwaka 2020 kusambaa sana kwenye mitandao ya kijamii hasa Facebook, harakati za “Black Lives Matter” zilisambaa duniani kote, japokuwa kampeni hiyo ilianzishwa mwaka 2013 baada ya kijana Tryvon Martin mwenye asili ya Kiafrika kuuliwa.

Mitandao ya kijamii ilibadilisha hadithi ya kifo cha George Floyd; kipande hicho cha video japokuwa kilikua kinaumiza kiliweza kupatikana kwa watu kuangalia kwa ukamilifu kupitia mitandaoya kijamii, tofauti na vyombo vya habari vya kawaida ambavyo vinabanwa na sheria kuonesha maudhui ya ukatili.

Kutokana na video hiyo, watu walitumia mitandao ya kijamii kutoa misaada kupitia kupitia links mbalimbali, kupeana vitabu vya kusoma kuhusu ubaguzi, kupanga maandamano na kupinga ubaguzi wa rangi.

Januari 2011, ulimwengu ulishuhudia Wamisri wakiandamana kuondolewa kwa Rais wao dikteta.

Baada ya mapinduzi kufanikiwa Tunisia, waandaaji nchini Misri walitengeza tukio Facebook kuwaita watu kuungana nao mtaani tarehe 25 Januari, wakitaja mahali ambapo maandamano yatafanyika pamoja na namba za mawakili wa haki za binadamu.

Wakati wa maandamano, wanaharakati walitumia Twitter kutuma habari za matukio yaliyokuwa yanatokea muda huo, maeneo waandamanaji waliyokuwa wakielekea na sehemu ambazo walipaswa kuepuka.

Tarehe 28 Januari, maandamano yalirudi kukiwa na idadi kubwa zaidi ya waandamanaji kuliko mwanzo.

Janga la Covid-19 mwaka 2022

Kufungwa kwa mipaka na vizuizi vya safari kutokana na janga la COVID-19 kulipelekea watu kutumia mtandao na mitandao ya kijamii kujiburudisha, kuwasilina na kushiriki kwenye mambo mbalimbali, pamoja na kufanya kazi.

Watu hawakutosheka tu kutuma ujumbe, walitaka kuonana. Hii ikachangia katika utafutaji wa njia mpya kuwasiliana, ambapo Zoom, Google Duo, na Facetime zilizokuwa maarufu zaidi.

Wakati watu walipoanza kufanya kazi kutoka nyumbani, Zoom na program nyingine za kufanana nayo zikazoeleka kama njia za mawasiliano, jambo lililoibua swali kama kuna haja ya kuwa na maeneo ya kazi ofisi.

Kutokana na watu kuchapisha habari mbalimbali kwenye Facebook, Twitter, Instagram, na TikTok wakati wa COVID, wakati wa baadae watu wataJifunza kwa usahihi nini kilijiri kipindi cha Covid na watu waliishije kipindi hiko, anguko la kiuchumi na mambo mengine kuhusiana na janga hili.

***

Mitandao ya kijamii haitumiwi tu kama sehemu ya kujiburudisha, kupitia kwayo watu wanajiingizia vipato, kutoa maoni juu ya mambo mbalimbali yanayofanyika kwenye jamii na serikalini lakini pia kufichua maovu kwenye jamii zao. Viongozi wanatakiwa kuacha mawazo yao mgando na kubeza mambo kwa ushabiki badala yake itumie kila njia kuchota fursa zinazoletwa na teknolojia ili kuleta maendeleo nchini.
 
Back
Top Bottom