Kama kweli Mungu hayupo, who organized haya mambo duniani?

Swali lako lenyewe la "nani" linaonesha ufinyu wa mawazo na anthropic bias.

Ni hivi, watu huwa tuna bias ya kujiona sisi ndiyo tupo maalum ulimwenguni na vile tunavyouelewa ulimwengu ndiyo kweli.

Wakati ukweli ni complex zaidi.

Ndiyo maana zamani watu walisema kwamba jua linazunguka dunia, kwa kutuweka sisi katikati ya ulimwengu halafu jua lituzunguke sisi.

Baadaye wakagundua kuwa, dunia ni sayari moja tu kati ya nyingi, zinazunguka jua, na jua nalo ni nyota moja tu kati ya mamia ya mabilioni ya nyota zilizo katika Milky Way Galaxy. Zinazunguka Saggittarius A hapi katikati ya Milky Way Galaxy.

Kwa hivyo, swali lako la nani linaturudisha kulekule kwenye bias ya kufikiri vitu lazima viumbwe na conscious being (hence nani). Swali hili linaonesha ufinyu wa mawazo na anthrooic bias.

Suala lingine linaloonesha bias na ujinga (natumia ujinga kama ignorance, kutokujua kitu, sikusudii kukutukana) ni hili suala la kutafuta mwanzo wa vitu kama vile mwanzo ni kitu cha msingi.

Mwanzo si kitu cha msingi.

Suala la nani kaanzisha, hata tukilipanua na kuondoa "nani" (ambayo nimesema ina anthropic bias) tukaweka swali zuri zaidi lililo inclusive zaidi, la "nini" kimeanzisha, si lazima kiwepo kitu cha kwanza kimeanzisha.

Hili swali linaonesha kutojua physics tu, hususan quantum physics.

Katika quantum physics, kuna sehemu causality - hii dhana ya kwamba hii cause A inaenda kupelekea kuwepo effect B - hii dhana ya causality ukizama deep huko katika quantum physics huwa inavunjika.

Yani ni hivi, kunatokea hali kwamba, unaona A inaanza, inasababisha B, halafu, B nayo inakuwa ndiyo iliyosababisha A kuwapo kabla A haijasababisha B kuwapo.

Hapo kunatokea quantum causality loop.

Swali zima la A kasababisha B iwepo au B kasababisha A iwepo linakuwa halina maana, vyote vimesababishana.

Hivyo, swali lako la causality, linaweza kuonekana interesting kwa mtu ambaye hajasoma quantum physics tu.

Kwa mtu aliyesoma quantum physics, msingi mzima wa swali una makosa.

Kwanza swali limeulizwa kutumia "nani", hiyo ni anthropic bias.

Ni kama vile umekuta jani la muembe mlangoni mwako, halafu unauliza "Mmasai gani kaweka hili jani la muembe hapa mlangoni mwangu?".

Sasa wewe, hujui jani kimefikaje hapo. Umejuaje aliyeliweka ni Mmasai? Kama Msukuma? Kama Mpemba? Kama ni upepo tu?

Pili, hata tukiondoa anthropic bias, suala zima la causation, si suala la msingi, kwa sababu si lazima kuwe na cause moja. Kwenye quantum physics tunaona inawezekana ukaona cause A imeleta effect B, halafu ile effect B nayo ikawa ndiyo cause ya cause A kabla cause A haijatokea. Hata huu muda wenyewe unavunjika, na hivyo concept yote ya causality inavunjika.

Yani ni kama upo katika ulimwengu ambao Mama kamzaa binti, halafu binti akawa mama wa huyo mama yake. Hapo unauliza, nani kasababisha mwenzake awepo?

Swali lako linakosa maana katika ulimwengu huo, kwa sababu, time imefanya quantum loop, wote wamesababishana. Unachukua sheria za ulimwengu unaouona wewe huu wa macro world, halafu unafikiri ulimwengu wote uko hivyo.

Wakati hata ukitumia macho yako tu huoni bacteria, huoni virus, huoni sehemu kubwa sana ya electromagnetic spectrum.

Inabidi ujivue kwanza hiyo anthropic bias ya kuukiza "nani", usome ma quantum physics yanavyoshangaza, ili uuelewe ulimwengu ulivyo vizuri.
Kuna vitu vinachanzo kimoja tu, siyo kila uumbaji unavyanzo vingi, mwanadamu anavizazi vingi au vyanzo vingi kwa vile ni uzazi wa muendelezo kutokana na uzazi, mfano jua mbona hua halizai majua mengi? The creator kakupa akili kipunje tu ili utumie kuishi kwenye hii universe lakini Siri za sirini kwake wanapata wachache.
 
Kuna vitu vinachanzo kimoja tu, siyo kila uumbaji unavyanzo vingi, mwanadamu anavizazi vingi au vyanzo vingi kwa vile ni uzazi wa muendelezo kutokana na uzazi, mfano jua mbona hua halizai majua mengi? The creator kakupa akili kipunje tu ili utumie kuishi kwenye hii universe lakini Siri za sirini kwake wanapata wachache.
Hujaelewa somo, omba ueleweshwe tena kama unataka kuelewa.
 
Nimekuuliza hivi, unajuaje hizo sheria ni za Mungu na si za watu tu?

Unaniambia hati za makubalianonhutoka kwa founder.

Sawa. Hata ikiwa hivyo.

Unajuaje huyo founder wa hizo habari ni Mungu na si watu tu?
Siri za Mbinguni utapewa ukiwa karibu na huyo Mungu unayesema hayupo, unapenda Siri zake? Jisogeze kwake akupe, Siri za familia zinajulikana kirahisi na Wana familia ndo hivyo na mambo ya Mungu yalivyo.
 
Who and why it’s okey kulingana na utakavyo jibu
Nimekuuliza hivi, why are you asking who?

Nimekutolea maelezo marefu hapo juu.

Nimekwambia hivi, wewe ni sawa na mtu aliyeamka asubuhi nyumbani kwake, akafungua mlango. Akakuta jani la muembe liko mlangoni.

Hajui jani la muembe limefika vipi hapo mlangoni.

Akauiza. "Mmasai gani kaweka jani hili la muembe hapa mlangoni mwangu?".

Sasa, naye anaulizwa swali.

Wewe unajuaje ni Mmasai? Vipi akiwa Msukuma? Vipi Kiwa Mpemba? Vipi ikiwa jani halijawekwa na mtu, lmepeperushwa na upepo tu?

Sasa wewe uanpouliza swali la "who?" ni sawa na mtu huyo anaueuliza "Mmasai gani?".

Unajuaje jibu lipi kwenye swali la who? Unajuaje swali la who ndiyo swali sahihi?
 
Siri za Mbinguni utapewa ukiwa karibu na huyo Mungu unayesema hayupo, unapenda Siri zake? Jisogeze kwake akupe, Siri za familia zinajulikana kirahisi na Wana familia ndo hivyo na mambo ya Mungu yalivyo.
Hujathibitisha Mungu yupo, katika kujaribu kuthibitisha yupo, unaongeza habari nyingine z auongo ambazo nazo huwezi kuzithibitisha.

Kama habari za mbinguni.

Thibitisha Mungu yupo.

Thibitisha mbinguni kupo.

Acha longolongo.
 
Na kwa vile naenjoy uwepo wake siwezi kukubali kwamba hayupo, na debate ya kuchagua upande kwamba yupo ama hayupo nitasema yupo maana namtumia kama Mungu aliyepo.
Hu enjoy uwepo wake bali una enjoy illusion ya uwepo wake.
 
Kwa hiyo una amini ulimwengu unajiumba wenyewe bila kuumbwa na mtu yeyote si ndio ?

Mpaka Leo sijasikia sehemu Fulani kuna mbuzi wamejiumba au kuna bata au Kuku au kuna wanadamu wametokea sehemu Fulani


Kuna mda najiuliza ivi akili zenu zona fanya kazi kweli kuna mmoja wenu uko kwenye comment ya za juu amekataa biblia akaanza kunipa kitabu kingine cha wana sayansi kwa akili yake yeye a anafikiri wana siasa sio wanadamu

Any way swali langu liko pale pale
Who organized mambo yote haya duniani ?
Na wewe kwa nini una amini Mungu alijiumba mwenyewe?

Unavyo shindwa kuamini kwamba ulimwenguni hauwezi kujiumba wenyewe, Vivyo hivyo amini hata huyo Mungu HAWEZI kujiumba.

Kwa nini unalazimisha ulimwengu uwe na muumbaji na una amini kwamba Mungu hana muumbaji,

Kama Mungu hana muumbaji na una amini hilo, Basi tambua kwamba hata ulimwengu hauhitaji muumbaji na uamini hivyo.
 
Kama kweli Mungu hayupo ni Nani aliye organized haya mambo duniani na mbinguni

Mfano kuna wakati wa jua na wakati wa mvua. Kuna wakati wa Giza na wakati wa mwezi. Kuna wakati wa baridi na wakati wa joto.

Tutoke uko twenda kwa mwanadamu
Angalia jinsi organ’s zake zinavyo jipangilia mwilini. Kama waya za umeme hivi.

Kwa wanyama, kuna wanyama wa angani na wanyama wa mwituni. Kuna nchi kavu na bahari.

Maswali ni mengi. I want to know who organized haya mambo duniani.

Kama sio Mungu kweli au kama hakuna mtu ambaye ali organized haya je, ilikuwaje mambo haya yakakaa kama vile yamepangiliwa?
MUNGU yupo. shida ni dini. ndio kelele zinakoanzia hapo.
 
Mungu yupi?? Mkiambiwa mlete ushahid mnashindwa mnabaki kutoa vitisho ambavyo haya huyo Mungu wenu hajawai watisha wasiomuabudu.

Dunia ina Miungu wengi sana kila jamii na Miungu yao, kwa bahati mbaya Afrika ndiyo ilipata laana ya kupata hizi dini mbili haramu za uislam na ukristo zilizoaminisha watu kuwa hizi dini miungu yao ndiyo sahihi na miungu ya imani nyingine ni uongo.

Mnasema kuna Mungu njoo na ushahidi wa uwepo wa Mungu wako kwa imani yako pia uje na proof kuwa Mungu wako ndie kaumba dunia.

Mimi si kwamba siamin ktk mambo ya kiroho bali napinga hiyo Miungu ya dini za wakoloni walizowaaminisha ndio Miungu sahihi na waumbaji.

Dini ya ukristo haina muda mrefu tangu itungwe, ina karibu miaka 1700 tangu kuundwa kwake kutoka ktk imani za warumi ambao waliCopy dini ya kiyahudi ambayo nayo ilicopy stori za uongo kutoka misri ya watu weusi, warumi hao wakaweka stori zao walizoona zinawafaa mfano Imani ya Miungu watatu yaan Mungu baba, mwana na roho, pia story za uzushi za yesu kristo ambaye hajawai kuwepo, pia story za jehanamu na mbingu za mchongo,

Story hizi zilitungwa na wahuni wa kirumi miaka ya 320 A.D huko kwao na ndio kipindi walicholeta huu utaratibu wa kalenda ya kuyatambua matukio kabla na baada ya huyo Yesu ambaye hajawai kuwepo, utaratibu ujulikanao kama A.D na B.C ama agano jipya na agano la kale haya walitunga kwa manufaa yao.

Baada ya kuunda ukatoric ndipo likaibuka , vuguvugu la mgawanyiko wa hili kanisa ama dini yakaibuka madhehebu pinzan ambayo yote kwa pamoja wanajulikana kama wafuasi wa kristo ama wakristo ama wanaYesu ama waliouhasi ukatoric lkn bado wako chini ya katoric(ukristo), na baadae hawa hawa wakatoric wakaunda uo uislam ambao ndio huu.

Kiufupi lengo la kuandika haya yote ni kuwaonesha kuwa hao mnaowaita Miungu mmetoa stori za hadithi kutoka ktk dini ambazo zimeundwa juzi tu ilihali dunia ina maelfu ya miaka, je miaka 500, 000 iliyopita hao mnaowaita Miungu wenu walikuwa wapi? Mbona vitabu vya dini zenu havielezi matukio yalokuwepo miaka maelfu iliyopita zaid zaid mnaelezwa vijitukio vya wakina falao wa Uongo hapo misri ambavyo hivi vitukio vimetokea juzi tu miaka ya 5000 before the fake Christ namely jesus(B.C kwa kalenda ya kipuuzi ya wakolon wa Vatican).

Kwanini vitabu vyenu havielezi nini kilitokea miaka 20, 000 iliyopita? Kwann vitabu vyenu na Miungu wenu mmebase ktk historia moja ya jamii za waarabu na hao waisrael feki ilhali dunia ina jamii nyingi dunian na ina maelfu ya matukio nje ya uongo wa hao manabii wenu wa mchongo?

Wanaopinga uwepo wa Mungu siwashangai maana kiuhalisia dunia haijaumbwa na Mungu kuna chanzo kilichoiumba lakini sio Mungu maana Mungu/Miungu ni nadharia za watu na wazungu kwa waarabu walitunga ili kutawala jamii za wajinga, unaposema Dunia imeumbwa na Mungu dhihirisha kuwa Yesu sijui Allah ama jehova ndie kaumba dunia mwaka fulan kipind fulan kwa ushahidi unaomake sense, na onesha shahidi hizo nje ya kitabu chako cha imani maana kiutaratibu jambo lolote huwa na ushahidi ambao unasapoti jambo hilo kiimani na nje ya imani pia huwa na shahidi za uwepo wake wa mabaki, muda wa uwepo wake dunian, matukio yanayosapoti uwepo wake nakadharika.

Nje ya Qur'an na Biblia hakuna jambo lolote ama tukio lolote lililotokea ktk hivi vitabu unaweza kulikuta ktk vitabu vya kihistoria na kisayansi kwanini? Kwa sababu hivyo vitabu vimedanganya na vimetungwa.

Niishie hapa.
Ndugu nafikiri una hasira sana na Mungu.Labda una sababu zako yumkini kila ukijaribu kumwamini unajikuta Ana sheria zake ambazo wewe yawezekana huzipendi.Najaribu kufikiri tu lakini.Sasa ndugu umejitahidi kuongea uongo mwingi mara matukio ya kwenye biblia hayapo kwenye historia.Uongo 100%.Pili Dunia haikuumbwa na Mungu bali kuna chanzo.Upo serious kweli?Hicko chanzo ndo kipi hebu kielezee walau tukuelewe maana navinavyoonaona unamzungumzia Mungu pasi mwenyewe kujua.Umewahi kujiuliza Dunia,Anga, hewa,gravity,maji,ardhi nk nk vyote vimewekwa kwa namna ambayo inasapoti uhai especially wa binadamu?Hivi hicho chanzo unafikiri kipo smart kiasi gani kujua na kutawala yote hayo yasikosee?Kwa sasa Acha niishie hapa ila tafakari nn maana ya chanzo ulichozungumzia uje na majibu ya kina.
 
Kuwa organized haimaanishi dunia imeundwa na Mungu, weka ushahidi kuwa Mungu kaumba dunia, usitumie Bible wala Qur'an maana hata ningekuwa mimi nmezaliwa kabla ya karne hii ningeweza kutunga kitabu changu cha kiimani na kusema ama kuandika kwa msisitizo kuwa mimi ndie Mungu niliumba dunia, na watu wa kipindi changu wangebisha maana wanajua kuwa nmetunga, bahati mbaya ninyi msio wa kipindi changu mngekubali maana hamjawai kuniona na mmeamin maandiko yangu na hamtaki kuyathibitisha maandiko yangu ijapokuwa kuna maandiko yalokuwepo kabla yangu.

Sasa prove kuwa dunia imeumbwa na Mungu na umtaje Mungu gani, ole wako umtaje Yesu maana Yesu hakuwepo miaka laki 5 iliyopita huyu kaundwa na wakatoric miaka 1700 iliyopita kwa kucopy nadharia za Mungu mwana wa jamii za mashetan kutoka kwa imani za wamisri/wakemet ama waafrika wa kale, pia usiseme Allah kaumba maana huyu nae katungwa miaka 1400 iliyopita kwa kucopy stor za Mungu mke ama Mungu mwezi kutoka ktk stori za mashetani waloabudu mababu wa zaman.

Prove mungu fulan kwa jina fulan mwaka fulan aliumba kitu fulan na sio vitisto na uongo uongo wenu...

Dawa yenu tukiwaomba ushahidi mnakimbilia matusi, vitisho na hasira,
Kabla ya kuprove ni Mungu yup kwanza tukubaliane kuwa Mungu yupo,baada ya hapo ndo tuanze kujadili ni Mungu yupi.Kinyume na hapo ni ushindani tu na blabla.
 
Kama kweli Mungu hayupo ni Nani aliye organized haya mambo duniani na mbinguni

Mfano kuna wakati wa jua na wakati wa mvua. Kuna wakati wa Giza na wakati wa mwezi. Kuna wakati wa baridi na wakati wa joto.

Tutoke uko twenda kwa mwanadamu
Angalia jinsi organ’s zake zinavyo jipangilia mwilini. Kama waya za umeme hivi.

Kwa wanyama, kuna wanyama wa angani na wanyama wa mwituni. Kuna nchi kavu na bahari.

Maswali ni mengi. I want to know who organized haya mambo duniani.

Kama sio Mungu kweli au kama hakuna mtu ambaye ali organized haya je, ilikuwaje mambo haya yakakaa kama vile yamepangiliwa?
Believe you me: Mungu hayupo.
 
Huwezi sema Mungu yupo na humjui je kama ni hisia zako? Dunia kwel imeumbwa je swal nan kaumba?? Maana ukisema Mungu kaumba dunia ujue kuwa nadharia za UMUNGU za kuabudu zimekuja juzi tu na dunia ina maelfu ya miaka je kwann hawa Miungu hawajawai kuwepo kipind cha miaka ile maelfu iliyopita? Ushahid unao hata babu zako hawakujua kuwa kuna kitu kinaitwa Allah wala Jehova wao waliamin kuna mizimu, na kuna viumbe wa kiroho lkn hawakutambua hiyo Miungu je ninyi mmepata wapi ujasiri wa kusema dunia imeumbwa ba Mungu ilihali Mungu huyu hakuwai kuwepo afrika kabla ya ujio wa dini? Pia imani za babu zenu hazimtambui?
Tatizo lako hueleweki.Unataka tumzungumzie Mungu au mizimu.Kwani Mungu kama alikuwepo tangu hiyo miaka millions whatever, na babu zako hawakumjua itaondoa uwepo wake?Fikiri tu miaka kadhaa nyuma hao babu zako hawakujua duniani kuna Jamii nyingine kama wazungu ,wasia nk.Je hiyo inamaanisha hizo jamii hazikuwepo?
 
Evolution, mchakato ambao umechukua mabilioni ya miaka
Hiyo evolution imesimama Leo?Jaribu kujiuliza kwa nn nyani hawaendelei kuwa watu?Kama walipatwa na hiyo Evolution ni kwa nn bado wapo? uongo mkubwa.Na hata KAMA ilikuwepo lakini kuna stating point,mfano nyani yeye alitokea wapi ndo sasa aka change kuwa mwanadamu?Tunapozungumzia Mungu tunamaanisha chanzo cha yote.
 
Sasa swala la mvua si ukajisomee how rain forms.

Swala na viungo vya mwili mbona simple go and read evolution of species. Utaelewa why ipo hivyo.

Je nikupe fact nyingine kuwa. Huyo Mungu unayemuamini hakuwahi kuumba mbwa, au cabbage au ndizi. Zote hizo ni binadamu alizitengeneza
Sisi hatuzungumzii man-made,tunamzungumzia aliyemtengeneza mwanadamu.
 
Back
Top Bottom