Kama kuendesha mradi wa DART umetushinda, miradi ya SGR na uendeshaji wa ATCL ndio tutaiweza?

mleta mada mzee wa matukio naona ushapata pa kukesha kuongelea.Huo mradi unaendeshwa Na mtu binafsi.Wewe ukiagiza gari si unalipa kodi? Hata uagize magari Mia mbili.Eti Hela anapata kodi ya kulipia magari bandarini hana!!!!!!mmmmmmm
Kwanza huu mradi serekali ina ubia. Pili tunazungumzia uhai wa watu kwa vile lolote linaweza kutokea kama hakuna improvement. Mwezi ulipotita watendaji wamewekwa rumande kwa kuzidisha watu kwenye mv Nyerere sasa hili suala la mwendokasi mbona dalili za janga zipo wazi? Tunangojea kutuma rambi rambi na kurundika watu ndani.

Tatu serekali imefaidi nini kwa kuzuia magari ya mwendokasi kwa karibu miezi 10 sasa? Wangeweza kuruhusiwa kutoa magari ili walipe kodi kwa makubaliano. Hii ingeingiza mapato kwa serekali na vile vile watumiaji wa huu usafiri wangelikuwa more productive hivyo kulipa kodi zaidi badala ya kupoteza muda vituoni. Kumbuka kuwa hata sasa hivi serekali imetoa nafasi kwa wanaodaiwa kodi kuja na mpango wa kulipa hivyo hili suala mabasi mapya kuzuiliwa ni la utashi wa kisiasa tu.
 
Kuna jambo la kujifunza jinsi tunavyoendeaha mambo yetu. Mwendo kasi mi nilitegemea muda wa majaribio uliwapa mwanga wa namna ya kuendesha na kila siku zilivyokwenda ilikuwa ni fursa ya kujifunza kwa lengo la kuboresha huduma.
Lakini hali inazidi kuwa tete kila iitwapo leo. Vituoni watu wanatumia mpaka masaa mawili kusubiria huduma ya magari, mrundikano wa abiria ndani ya gari si salama kiafya kwa mtu mmoja mmoja na hata kwa usalama wa gari husika. Fikiria kama mtu ana ebola na hali ya joto la dar na ndo amebanana na wengine kiasi ambacho hata kufungua mlango wa gari husika ni kazi, je ni wangapi wataondoka na tatizo hilo.
Wakati mwingine pale Kimara unakuta mabasi zaidi ya 7 yameegeshwa na madereva wamo ndani ili hali abiria wapo kituoni wa kuweza kujaza magari hata mawili.
Yaani, kwa ujumla kama kuna mtu alituroga daaa angepatikana aondoe huu uchawi.
BRT ilitegemewa iwe mkombozi wa watu, imegeuka kuwa shubiri.
Leo ITV wamewatembelea kuonesha uregevu uliopo ktk uendeshaji wa hiyo huduma.
Yaani ni tabu ya hali ya juu na jitihada za kupunguza foleni inakuwa haijatimia.
Mi nilitegemea kwa kuwa yalikadiriwa kutumia dk 45 mpaka City Center, then yangekuwa na ratiba ya utenda kazi ambayo ingesaidia watu kupanga maandalizi yao ktk utendaji kazi. Yaani kama mtu anataka kufika saa tatu asubuhi, then atajipanga ili aweza kupanda basi la saa 2:15 asubuhi ili saa 3 asubuhi awe amefika City Center. Kumbe laaaaaaa, unaweza kufika kituoni saa kumi na moja alfajiri na ikafika saa mbili ikakukuta haujapanda gari.
 
Kwanza huu mradi serekali ina ubia. Pili tunazungumzia uhai wa watu kwa vile lolote linaweza kutokea kama hakuna improvement. Mwezi ulipotita watendaji wamewekwa rumande kwa kuzidisha watu kwenye mv Nyerere sasa hili suala la mwendokasi mbona dalili za janga zipo wazi? Tunangojea kutuma rambi rambi na kurundika watu ndani.

Tatu serekali imefaidi nini kwa kuzuia magari ya mwendokasi kwa karibu miezi 10 sasa? Wangeweza kuruhusiwa kutoa magari ili walipe kodi kwa makubaliano. Hii ingeingiza mapato kwa serekali na vile vile watumiaji wa huu usafiri wangelikuwa more productive hivyo kulipa kodi zaidi badala ya kupoteza muda vituoni. Kumbuka kuwa hata sasa hivi serekali imetoa nafasi kwa wanaodaiwa kodi kuja na mpango wa kulipa hivyo hili suala mabasi mapya kuzuiliwa ni la utashi wa kisiasa tu.
Awamu hii hawaelewi chochote
 
Kila kitu hakikosi changamoto zake,kama ulivyo wewe na maisha yako ,nawewe katika maisha yako una changamoto zako na hata miradi mingi mikubwa ina changamoto zake,kama hukosi changamoto basi umekuwa jiwe

Usiwe mfia nchi kwenye ishu za kipuuzi km hzu. Wenzio wanafia vitani na mitutu wewe unataka kufia JF kuwatetea UDART. Ishu sio changamoto hakuna anayekataa challenge ishu ni namna gani mamlaka husika zinapaswa kutatua hizi changamoto. Umeshawah kutumia huu usafiri kweli ktk maisha yaisha yako?
 
Leo nami nimepata pa kusemea jamani. Ni hivi, mimi ni mmoja kati ya wapanda mwendo kasi zetu. Ni bonge la project na ninaishukuru sana serikali kwa kuanzisha hii kitu. Ukweli mchungu ni kwamba wafanyakazi wa UDART wanaiba sana kwa sasa. Mfano mmoja nipale Kimara mwisho. Baada ya kuhakikisha wameshaiharibu system ya ticketing basi imekuwa rahisi sana kupiga pesa kwa hawa watu. Wanasubiri basi la kwenda Mbezi mwisho likianza kuondoka basi hata vile vi ticket hawavichani tena kwa maana hiyo wanavirudisha madirishani ambako napo huwa tunakuta receipts zishatolewa kwenye machines. Ukitoka mbezi mwisho tena kuna baadhi ya madereva wanasanya kama daladala na nauli wanachukuwa wao. Wanahakikisha gari ikikaa level seat tu wanaluondoa na huko vituoni anachukua hela bila receipts na hivyo kutia mfukoni. Kuna babu mmoja wa kichaga ndiyo zake kila siku. Sasa kama wanakwiba hivyo, mishahara itatoka wapi? Nilisema hili juzi tu kuwa hili Mh. Jaffo anahifadhi bomu na muda si mrefu litamlipukia. Hii ya leo ni dalili tu. Kunatakiwa kuwe na ufuatiliaji wa karibu sana na kama system za ticketing zimetushinda basi tuwarudishe maxmalipo mpaka hapo tutakaposettle. Kwa sasa wafanyakazi wanaiba mamilioni kwa siku. Muda ni msema kweli.
 
mleta mada mzee wa matukio naona ushapata pa kukesha kuongelea.Huo mradi unaendeshwa Na mtu binafsi.Wewe ukiagiza gari si unalipa kodi? Hata uagize magari Mia mbili.Eti Hela anapata kodi ya kulipia magari bandarini hana!!!!!!mmmmmmm

Hiyo miundombinu imejengwa na mtu binafsi au serikali?!

Kama serikali imewekeza kwenye miundombinu kwa nini iachie watu ambao hawana uwezo wauendeshe?!
 
Naunga mkono hoja, huwa hakuna miujiza, tunashindwa hata ustaarabu tu wa kuhakikisha watu wanapanda kwa mstari, tutaweza nini? I mean Meya wa Dar/ Ubungo kazi yake nini? Hawezi hata kusimamia hili?
Ubungo kwa sasa hakuna meya, alisema ole milya akihamia ccm nae anahamia ccm. Keshahama bado kuandika barua tu.
 
Ni kama Mbowe alivyoshindwa hata kujenga ofisi ya chama alafu anakomaa chadema ichukue dola na kuongoza nchi .
Ataweza??

Huenda kaona kujenga ofisi sio jambo la msingi, maana wenye ofisi wao kila uchaguzi wanategemea polisi na tume ya uchaguzi kushinda. Hivyo kaona ofisi sio suluhisho la kupata kura.
 
Tatizo la mtu mweusi anapenda sana kufanya kazi ya unabii wa majanga. Kwa hiyo mleta mada unaifurahia hii hali ya mashirika kuendeshwa kwa hasara!!?.

Kwa fikra za namna hii ndio maana washirikina bado wana soko barani Afrika.
 
Leo nami nimepata pa kusemea jamani. Ni hivi, mimi ni mmoja kati ya wapanda mwendo kasi zetu. Ni bonge la project na ninaishukuru sana serikali kwa kuanzisha hii kitu. Ukweli mchungu ni kwamba wafanyakazi wa UDART wanaiba sana kwa sasa. Mfano mmoja nipale Kimara mwisho. Baada ya kuhakikisha wameshaiharibu system ya ticketing basi imekuwa rahisi sana kupiga pesa kwa hawa watu. Wanasubiri basi la kwenda Mbezi mwisho likianza kuondoka basi hata vile vi ticket hawavichani tena kwa maana hiyo wanavirudisha madirishani ambako napo huwa tunakuta receipts zishatolewa kwenye machines. Ukitoka mbezi mwisho tena kuna baadhi ya madereva wanasanya kama daladala na nauli wanachukuwa wao. Wanahakikisha gari ikikaa level seat tu wanaluondoa na huko vituoni anachukua hela bila receipts na hivyo kutia mfukoni. Kuna babu mmoja wa kichaga ndiyo zake kila siku. Sasa kama wanakwiba hivyo, mishahara itatoka wapi? Nilisema hili juzi tu kuwa hili Mh. Jaffo anahifadhi bomu na muda si mrefu litamlipukia. Hii ya leo ni dalili tu. Kunatakiwa kuwe na ufuatiliaji wa karibu sana na kama system za ticketing zimetushinda basi tuwarudishe maxmalipo mpaka hapo tutakaposettle. Kwa sasa wafanyakazi wanaiba mamilioni kwa siku. Muda ni msema kweli.
Kwa maelezo haya,umewasaidia sana wahusika kujua nini cha kufanya kama wanasoma maoni ya watu humu mitandaoni.

Tunakushukuru.
 
Tatizo la mtu mweusi anapenda sana kufanya kazi ya unabii wa majanga. Kwa hiyo mleta mada unaifurahia hii hali ya mashirika kuendeshwa kwa hasara!!?.

Kwa fikra za namna hii ndio maana washirikina bado wana soko barani Afrika.
Maoni yaliyotolewa humu mpaka sasa ni msaada mkubwa sana kwa serikali kama wanafuatilia yanayoandikwa.

Kwahiyo,ni bora kuyasema ili solution ipatikane na si kuyaficha kama unavy-suggest.
 
Hakuna aliyesema tuyafiche, ujumbe ni kuwa muwe mnaanzisha nyuzi hata kuhusiana na yale mashirika yanayopeleka serikali magawio makubwa mwaka baada ya mwaka.

Yapo mashirika kwa sasa yanayopata faida, na yenyewe yanayo mambo mengi muhimu ambayo jamii inapaswa kuyafahamu.
 
Hilo gawio una uhakika nalo?Mwenendo wa hii serikali kila mtu anaujua.
 
Back
Top Bottom