Kama huu mkataba (IGA) ulikuwepo zaidi ya mwaka, HGA pia ipo zaidi ya mwaka sasa, kinachofanyika ni maandalizi muafaka ili uanze HGA iingie kazini!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,664
18,039
Kuna hoja dhaifu kuwa kwa kuwa IGA katika mkataba wa bandari una matatizo, basi tuje tuwe macho kwenye maandalizi ya HGA ili yale madhaifu ya kwenye IGA yarekebishwe na HGA. Kwanza kwa faida ya baadhi yetu ni kwamba HGA (Host Government Agreement) ni makubaliano ya msingi kati ya mwekezaji wa kigeni na serikali mwenyeji kuhusu HAKI NA WAJIBU/MAJUKUMU YA LAZIMA (rights and obligations) kwa mwekezaji wa kigeni na serikali mwenyeji unaohusiana na uendelezaji, ujenzi na utekelezaji wa mradi unaofanywa na mwekezaji wa kigeni. Itiliwe maanani kuwa hii haki na wajibu/majukumu ya lazima ndiyo yanayomwezesha mwekezaji kutekeleza programu yake ya uwekezaji na si vinginevyo!! Ni mazingira wezeshi!! Bila haya uwekezaji hautekelezeki!! Kutokutimiza hayo majukumu ni sawa na kuvunja mkataba!!

Kuhusiana na mkataba wa bandari ni dhahiri kuwa ili utekelezeke kwa mujibu wa IGA ni lazima sheria zetu zibadilike ili kuruhusu mwekezaji kumiliki ardhi, lazima tutunge sheria ya kuzuia mwekezaji mwingine kwenye bandari zetu zaidi ya DP World nk. Ndiyo maana tayari kuna minong'ono ya kubadilisha baadhi ya sheria zetu zilizokiukwa ili ziendani na huu uwekezaji (mimi nauita ukwapuaji) wa mwarabu!! Na kubadilisha hizi sheria itakuwa ni moja ya majukumu ya lazima ya serikali mwenyeji ili "mwekezaji"aweze kutekeleza mradi wake!!

Kusema ukweli hizi haki na wajibu/majukumu ya lazima tayari yameshaandaliwa ila ni SIRI-KALI na itabakia kuwa ni SIRI-KALI na hayatafika hata bungeni!! (kwa kawaida HGA huwa ni SIRI). Kama mkataba wa bandari ulikuwa tayari zaidi ya mwaka, ninaamini hata HGA iko tayari na wahusika serikalini wanajua kila kitu, halafu tunadanganywa kuwa makubaliano hayo ya HGA yatakuja baadaye na yatazingatia hoja zetu!! Tutakachokishuhudia maana hakiwezi kuwa siri (maana kitafanyika bungeni) ni ubadilishaji wa sheria na utungwaji wa sheria ili sheria zilazimishwe kukubaliana na wizi huu wa mchana kweupe!!.

Host Government Agreement (HGA)​

An agreement between a foreign investor and a local or host government governing the rights and obligations of the foreign investor and the host government with respect to the development, construction, and operation of a project by the foreign investor. Many HGAs include a stabilization clause designed to minimize the financial and political risks posed to foreign investors as a result of sudden changes in national law.

Mwana jamvi mwenzetu Mayala anaomba eti HGA ziwe transparent ili tujiridhishe kama mapendekezo yetu yamezingatiwa, kitu ambacho anajua kabisa kuwa hakiwezekani!! Hapo ndipo ninapomtilia mashaka Mayala!! Yaani tuukubali mkataba, ila tukaze kwenye HGA!! Hii ni sawa na kukubali kufunga ndoa na mke ambaye amedhihirika kuwa ni mchawi na kudai kuwa nikimwoa nitamshauri aachane na uchawi!! Kilichofanywa na DP World Djibouti na kwengineko, tukitegemee kitatokea Tanzania!! Tuvunje mkataba sasa kabla ya HGA haijaingia kazini!! Kisha mchakato wa kumtafuta mwekezaji uanze upya kwa kufuata sheria, na waarabu wakitaka waombe pia!!
 
Mnavyopenda Tanzania iendelee kuwa maskini nyie wapuuzi! Eti tuvunje IGA.

Mtasubiri sana embe chini ya muarobaini.
 
Mnavyopenda Tanzania iendelee kuwa maskini nyie wapuuzi! Eti tuvunje IGA.

Mtasubiri sana embe chini ya muarobaini.
Sasa huyo mkwapuaji ndo atakupa utajiri!! Kama ni mwekezaji kweli itabidi akubali kufuata sheria zetu na si kutulazimisha sisi tubadili sheria zetu!! Au unataka atufanye kama alivyowafanya wale wa Djibouti?
 
Back
Top Bottom