GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Kenya wanaonekana wapo vizuri sana upstairs! Wakati jirani zao wakibweteka kwa kuwa na ardhi kubwa na idadi kubwa ya watu, wao na viongozi wao wanachangamkia fursa zilizopo ng'ambo.
Kwa jicho la haraka haraka, inaonekana Kenya, Rwanda na Uganda zimeipita mbali sana Tanzania kwa raia wake kufaidi vya ughaibuni!
Ni nani aliyewaloga watawala wa Tanganyika wasijue umuhimu wa kwenda "nje?"
Angalia takwimu ya mwaka 2021. Hizi ndizo dola za Kimarekani zilizoingia nchi husika kutoka kwa raia wao wanaoishi ughaibuni:
1. Kenya, dola 3,718,000,000
2. Uganda, dola 599,300,000
3. Tanzania, dola 569,500,000
4. Rwanda, dola 246,000,000
Usije ukajisifia kuwa tumeipita Rwanda! Ukilinganisha ukubwa wa Rwanda na idadi ya raia wake, hicho kiasi ni kikubwa sana. Ingawa sijaangalia, lakini inawezekana na sisi tumeipita Burundi.
Kwa takwimu hiyo, unafikiri Dual citizenship ina faida au haina?
Nitarejea baada ya muda mfupi.