Kama hii ndiyo idadi ya CHADEMA kutoka mikoa kuja kwenye kesi ya Mbowe, basi chama kimepoteza mvuto kabisa

Kijogoodi

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
1,363
2,372
Kwa wiki moja sasa Chadema walikuwa wakihamasishana kuhudhuria kwa wingi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wao Mbowe.

Kuanzia katibu mkuu wa chama John Mnyika alitokwa povu sana akiwaambia polisi liwalo na liwe maelfu ya wananchi watafurika mahakamani Kisutu siku ya tarehe 5, akaja John Pambalu mwenyekiti wa Bavicha Taifa naye akatishia nyau kuwa kuna maelfu ya wanachadema kutoka mikoa 5 watahudhuria kesi hiyo.

Leo wanachadema walioonekana wakiimba karibu na mahakama ya Kisutu hawajai hata kwenye kikanja!! Jirani yake wamachinga walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

View attachment 1880704
 
CHADEMA WANATAKIWA WAJITAFAKARI WAANZE UPYA UPINZANI HAUENDI WANAVYOTAKA WAO HUO NI MFANO TU KUWA WAMESHAPOTEZA MVUTO NA USHAWISHI KWA WATANZANIA YAANI HATA ASILIMIA MOJA YA WATANZANIA HAWASAPOTI WANAYOYAFANYA WATU WACHACHE HIVYO NDIYO WANAPONGEZANA ETI WAMEFIKA ? NI UTOTO WA HALI YA JUU SANA HUO
 
CHADEMA wameshindwa kutumia busara zao na akili za kuzaliwa wanajua nchi ilikuwa katika hali mbaya sana na mdororo mkubwa, huku wahanga wakubwa wakiwa ni wao na wanachama wao kwa kuwekwa ndani kwa kesi mbalimbali kwa rehma za Allah akatuletea mwanamama SSH.

Mma kwa utu na hekima kuu kaanza kuwatoa ndani kwanza kwa upendo wake mkuu kawafutia makesi lukuki lakini shukurani hawana kabisa kumbe wema huu chadomo wameona ni ujinga wamefanyiwa #

Sisi wanachadema wa ngazi ya chini tunayaona haya sana na tunamshukuru sana mama yetu kipenzi aliaambia ndugu zanguni vuteni kwanza subira turekebishe upande huu mabwana wale wakaona haina maana wakaona wafanye fanye tu madudu madudu yao waivuruge nchi yetu ambayo ililelewa katika misingi ya masikilizano VIONGOZI WA CHADEMA WAACHE KUWABURUZA WANACHAMA WAKE KAMA MAPUNDA KWA MASILAHI YA VIONGOZI
 
chadema wameshindwa kutumia busara zao na akili za kuzaliwa wanajua nchi ilikuwa katika hali mbaya sana na mdororo mkubwa,huku wahanga wakubwa wakiwa ni wao na wanachama wao

Kesi za kubambikiza angalau hii mpya ya ugaidi haionekani kwenye bandiko lako refu. Ni coincidental au deliberate?
 
People need money not words.. Nani atakutatulia shida zako ukiwa huna hela Kisha unautumia huo muda kuandamana..?
Hao viongozi yakiwapata wanapitisha bakuli uwachangie! Sio ccm sio chadema they are all need money ndo maana tunawekewa mitozo ya kila namna so chagua ukasikilize kesi au utafute hela.
 
chadema wameshindwa kutumia busara zao na akili za kuzaliwa wanajua nchi ilikuwa katika hali mbaya sana na mdororo mkubwa,huku wahanga wakubwa wakiwa ni wao na wanachama wao...
Da tungekuwa tuna mawazokama haya wote tungekuwa mbali sana mama ni muungwana vywa kutosha mdude katoka wanasema kashinda kesi ingekuwa kipindi kile angesota mpaka basi mama anahuruma kweli wengi wametoka lakini ndiyo wamezidisha jeuri mama endelea kuwanyoosha tu wataukubali moto wako tu hao
 
Kizazi cha laana CCM tatizo hamna akili sasa hujui kwamba kuna tishio la kuua kutoka kwa mwenyekiti mwenza wenu Kamanda uchwara Siro? Unadhani hilo tishio la kupiga na kudhuru wanaotaka kuandamana kwa amani lisingekuwepo hali ingekuwa hivyo? Tatizo hamna akili au hata kama mnazo lakini mmejazwa mapepo uovu ya CCM.
 
Kwa wiki moja sasa Chadema walikuwa wakihamasishana kuhudhuria kwa wingi kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wao Mbowe.

Kuanzia katibu mkuu wa chama John Mnyika alitokwa povu sana akiwaambia polisi liwalo na liwe maelfu ya wananchi watafurika mahakamani Kisutu siku ya tarehe 5,,,

Hawatokaa watoboe hawa

Wataishia mitandaoni tuu.... hapa naona idadi kubwa ya wafuasi 19 wa chadema kisutu🤣🤣🤣

 
chadema wameshindwa kutumia busara zao na akili za kuzaliwa wanajua nchi ilikuwa katika hali mbaya sana na mdororo mkubwa,huku wahanga wakubwa wakiwa ni wao na wanachama wao....
Kudai katiba sio kosa,ni haki ya wanaodai hata kama wasiposikilizwa bado wanahaki ya kudai kwa uhuru!

Hapa ni kama unakiri kuwa yanayotokea kwa Mbowe ni kutokana na kudai kwake katiba na si hayo aliyoshtakiwa nayo!
Yaani Rais akisema mnipe muda,vyama vikampinga na kudai mabadiliko ni sasa.

Wanakuwa wamekosea wapi?Hiyo si ndio demokrasia?Kutofautiana na kukubaliana ni sehemu ya demokrasia!
 
We Msukuma lete picha ata ya ng'ombe
Kwa niaba ya watu wa usukumani😁!.
2870094_Kwa_uoga_na_uongo_wao_pamoja_na_vitisho_vyao_kuongea_IGP_makamanda_wa_polisi_na_kuvami...jpg
 
Back
Top Bottom