Kama hali ni Hii Arumeru CCM basi

Leo m/kiti wa kitongoji cha mulala na watu wengine wa ccm kata ya songoro wamerudisha kadi na kupokea za chadema
 
Mtoto wa marehemu na mgombea wa ccm ktk jimbo la Arumeru amewataka wapenzi wa magamba wasiende kwenye campeni za cdm kwa kuwa watawadanganya wa watachagua mbunge ambaye hawezi kupitisha bajeti bungeni kwa kuwa wao hawaundi serikali na hawawezi kupitisha bajeti kwa kuwa ni wachache bungeni huishia kutoka nje.

My take

Uhuru uko wapi wao wawasikilize ila wapinzani wasisikilizwe kwa kuwa watawapa maziwa watapike sumu mnazowanywesha ambazo mwisho wa siku eti mlikuwa mnatania

Source ITV habari
 
CCm itaendelea kuwa juu tu. Tanzania hakuna chama cha siasa hata kimoja vyote ni vyama vya harakati na kutangaza harakati badala ya sera. CCM oyeeeeeeeeeee!

Ukiwa Arumeru ukisema tu CCM hoyeeee nje ya mkutano wa CCM na wenye Green Guard wa kufa mtu basi ni lazima usikie Uwwiiiiiiiiiiiiiiiii kama vile akina mama waliavyo uwwwiiiiiii kuchoka hicho kitu au kutokitaka.
 
Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)

Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)

Nikweli Kipindi cha mwalimu Nyerere huenda hakuwa ameona chama mbadala, Je na wewe leo bado huoni mbadala wa CCM?
 
Hii inadhihirisha ukilaza wa huyu jamaa. Sasa ataweka ulinzi kuhakikisha hawaendi maana watu wana uhuru wa kujiamulia waende wapi. Anakimbia kivuli chake kwani jamaa wakisikiliza upande wa pili wanagundua kuwa saa ya ukombozi ni sasa.
 

Lusinde a.k.a Kibajaji amemnadi mgombea wa ubunge arumeru mashariki kupitia CCM, SIOYI kwa kuwaamasisha wapiga kura wa arumeru wamchague mgombea huyu kwa kuwa anatoka katika ukoo mkubwa ndani ya CCM.

Source ITV habari ya saa mbili usiku.

My Take:
Kuna ukoo ndani ya CCM? Zipo ukoo ngapi na ukoo mkubwa ndo upi??
Hujuma zinazosemekana dhidi ya wapiga kampeni wa CCM kuwa na nia ya kumuangusha SIOYI ndo zinajidhihirisha kupitia Lusinde, Wassira na Olesendeka na Nchemba kwani tangu wafike arumeru wanatumia hoja na siasa za kitoto ambapo sera hizi badala ya kumnadi zinageuka kumchafua na kumnyima kura mgombea huyu wa CCM.
 
Wana jf mliotazama habari startv saa mbili usiku huu mtakuwa mashaidi wangu!Hivi Huyu Siyoi hajui kweli Mwanry ni mbunge WA jimbo gani?
Duh poor SIYOI...
 
Mkuu nilifuatilia habari ya ITV vizuri.
Lusinde alisema hivi, "Mchagueni Siyoi, anatokea ukoo mkubwa wa CCM"
Yaani alimaanisha vyama vya siasa ni 'koo' na CCM ambayo ni moja ya vyama hivyo, ni ukoo mkubwa yaani chama kikubwa.

Tusipotoshe jamanijapo tunahitaji mabadiliko.
 
Wana jf mliotazama habari startv saa mbili usiku huu mtakuwa mashaidi wangu!Hivi Huyu Siyoi hajui kweli Mwanry ni mbunge WA jimbo gani?
Duh poor SIYOI...

Huyo jamaa amelazimishwa kufanya siasa,jamaa hajui kuongea kabisa,hajui hata anafanya nini,chadema jimbo letu hilo tuongeze nguvu tu.
 
Lusinde hovyo kabisa hata mpangilio wa maneno hana, matusi yasiyo na msingi anawaambia wanaume wa kimeru tusipompa siyoi kura tuna mimba! Maneno gani haya mr lusinde u r....
 
Atakuwa aliandikiwa desa na majimarefu au Lusinde wamemlisha kasa. Naskia jamaa huwa anaandikiwa usiku mambo ya kuzungumza kesho yake ili akalili usiku kucha na kugandamizia ndumu (bangi) asubuhi ili apate stimu ya kupandia jukwaani. Akipata ubunge huyo jamaa hadhi ya kuwa mbunge nchi hii itashuka sana
 
Atakuwa aliandikiwa desa na majimarefu au Lusinde wamemlisha kasa. Naskia jamaa huwa anaandikiwa usiku mambo ya kuzungumza kesho yake ili akalili usiku kucha na kugandamizia ndumu (bangi) asubuhi ili apate stimu ya kupandia jukwaani. Akipata ubunge huyo jamaa hadhi ya kuwa mbunge nchi hii itashuka sana

kuhusu kukaririshwa ni kweli kabisa.vyanzo vyangu ndani ya ccm vimeniambia hili.kashinikizwa kugombea ubunge!
 
Mkuu nilifuatilia habari ya ITV vizuri.
Lusinde alisema hivi, "Mchagueni Siyoi, anatokea ukoo mkubwa wa CCM"
Yaani alimaanisha vyama vya siasa ni 'koo' na CCM ambayo ni moja ya vyama hivyo, ni ukoo mkubwa yaani chama kikubwa.

Tusipotoshe jamanijapo tunahitaji mabadiliko.

huyu jamaa masikio yake ni sonara
 
wana arumeru chagueni ccm mambo ya ufundi wa kuongea kama mkutano wa injili itawasaidia nn? Chagueni chama chenye dollar ambacho kinaweza kutekeleza mahitaji yenu kwa wakati kuweni wajanja ishara ya kijani ni njema sana kwenu kama hamtambui hilo tambueni hvy na tarehe 1-4-2012 chagua siyoi kuwa mbunge wako
 
Back
Top Bottom