Kama dharau ikatokea - huko huko wanakofanya dharau hizi - Mh. Naibu Spika

Hii kauli ya Mh. Naibu spika imebeba ujumbe mzito sana![/QUOTE ]

Huyu ndugai ni kigeugeu sana!! kama utakumbuka kweli mdahalo kati yake na Tundu Lissu mwezi uliopita, akijibu moja ya maswali ya washiriki wa mdahalo alisema ' Kazi ya bunge ni kuisaidia serkali iliyoko madarakani iweze kutawala nchi...' sasa unajiuliza hivi hajui kweli kwamba kazi ya muhimili wa bunge si kuisaidia serikali bali kuisimamia?? Sasa anashangaa nini serikali ilikikejeli bunge wakati ni wao walioilea (mtoto umleavyo...). Pia sijawahi kuona serikali yenye vituko kama hii: Kwanza swala zito kama lile lilihitaji tume huru na makini, wao wakampa hilo gunia zito la misumari CAG alibebe mwenyewe (unategemea nn?); pili baada ya kupata ripoti wangepima effects zake kwa kauli ya Pinda (kimsingi alishamhukumu ila alikuwa anangojea kibali cha raisi!!); tatu maamuzi hayo yangeathiri vipi bunge kwani suala hilo lilianzia bungeni. Mimi nilitarajia wangepeleka matokeo ya uchunguzi bungeni badala yake huyu Luhanjo akakurupuka!!. Huu utakuwa mtihani mwingine mkumu sana kwa JK; tusikilize yatakayojiri.

Macho yako makavu sana kiasi kwamba unashindwa hata kusoma alama za nyakati. Kwa taarifa yako harakati na wabunge wa CCM ni mkakati madhubuti wa kuwapoteza wapinzani ili wasisikike tena. Ndiyo maana hoja nyingi siku hizi zinaibuliwa na wabunge wa CCM halafu CHADEMA wanabaki kupiga mayowe kwa nyuma. Tafakari bwana mdogo.

Na ile taarifa ya kwamba THT walichukua nyumba na studio ikiwa ni vitu alivyovitoa Rais kwa wasanii wote aliibua CCM?

jamaa anakuja kwenye sense sasa ameona dharau imezidi coz hata yeye ameitwa ze comedy na Jairo

Kwani Jairo/Luhanjo/CAG etc, wameonesha dharau gani kwa waziri mkuu/bunge kupitia mitandao ya kijamii?

mi nadhani msamehe bure huyu nahisi hapa alitumia masabuli kufikiri na kama ni kweli adhibitishe kauli yake tena si kwa maneno bali kwa vielelezo

Kwani Jairo/Luhanjo/CAG etc, wameonesha dharau gani kwa waziri mkuu/bunge kupitia mitandao ya kijamii?

Kaka naungana na wewe hakuna dharau yeyote iliooneshwa bali waliojidharau wanajidharau wenyewe kwakuwa wanatoa matamshi pasipo bila utafiti na consultation kwa wahusika...sasa ona na huyu nae ndungai anatoa matamshi gani sijui na kwa manufaa ya nani sijui....wakijibiwa kwa sheria wanasema wamedharauliwa....mie naomba tv au wanaharakati waandae midahalo ya vijana hasa wa humu JF tuwetunajitokeza na kujadili hoja kama hizi na walioko nje ya nchi siku hizi technology ipo juu wanaweza kuchangia pia kwa screen na kusikilizwa utaona kama watu watajitokeza..wanajua kuongea kwenye net tu.....matokeo yake nchi haieleweki...hata nyerere wakati anapambana na wakoloni alijitokeza na kujenga na kuelewwesha watu hoja za msingi......Nilichangia jana kuwa wakiruhusu kamati ya bunge watataka na CAG,Luhanjo,mawaziri na waziri mkuu wajiudhuru......na mwisho watataka rais naehajiudhuru...mie nafikiri serikali iangalie hoja na sio maneno ya wanao sema sana bungeni na nje ya bunge sijui.

serikali ni watu na watu ni sisi sasa serikali inapofikia mahali inataniwa a watu wasio na hoja mie inaniuma sana sanaa tena sanaa namuheshimu sana Dr. Slaa kwa kujenga hoja kwa vitu vya msingi kwa taifa na ndio maana Dr. Slaa hajazungumza juu ya jambo ka hili la JAIRO nashhangaa CCM wanariruhusu kuwa la kitaifa kweli na hiyo kamati kabla ya kutoa majumuhisho ishirikishe jamii kuchangia sio kutuletea matokea badae yawe malalamiko tena ka ya Richmond mpaka sasa wananchi hawajui kipi ni kipi na kipi si kipi..maana siasa its a game..tusichezee nchi kwa personal political affairs

Bunge letu likiamua linaweza! Sasa wanatakiwa waamue kwenye mambo ya msingi yenye maslahi ya wananchi wengi, Madini, Umeme, Maji na Huiduman za Afya siyo kushabikia kutukanwa kwa Bunge, sisi kila nsiku tunatukanwa through kukosekana huduma muhimu watusimamie

Aliposema dharau huko huko hakumaanisha kwenye mitandao ya kijamii Luhanjo,CAG, Jairo huwa wanatukanwa kwenye mitandao???na wewe hapa jf unatukanwa kwasababu huwa unaongea pumba unafikiri kwa kutumia masaburi ndio maana radio yenu(clouds) umbea mtupu.

Natamani ningekuwa na umaarufu kama Jairo, unapewa likizo ya malipo, uchunguzi wa kishkaji kisha unarudi kwa kishindo Wizarani. Kila kitu kiliandaliwa hata waziri wake Ngeleja aliacha Bunge kwenda kumpokea wizarani. This is Tanzania You want

Baba Eno; hiyo kauri haina ujumbe wowote nakuhakikishia ni maneno ya hasira ya mtu hasiyejuwa la kufanya kama angekuwa Mhehe wa wazamani angeishia kujingonga tu!

Kama Pinda amedharauliwa popote waseme ni wapi, mi naona yeye mwenyewe ndie anajidhalilisha zaidi na kujidharaulisha mara dufu. Pinda ana fanya nini ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu? Kama hata kumfukuza Jairo kazi alisubiri Kikwete aje kusema la kufanya! Unataka kusema Jairo angefanya hayo Mbele ya Sokoine, Mbele SAS! Mbele ya Lowasa!? Thubutu wasinge subiri protocol, Rais angeuta pamewaka moto ambao hasingeweza kuuzima milele labda aangue na yeye.

Ndugai ni zoba hana kitu na ndio maana wanaunda kamati kupoteza muda kwa jambo ambalo jibu lake tayari lipo, kinachotakiwa hapa sio uchunguzi tena ni maamuzi! wao wanataka kuchunguzaa nini? Kwani Bunge ni chombo cha uchunguzi au maamuzi?

Kama wao ni chombo cha maamuzi wanataka kuchunguza nini kama si kutuongezea gharama zisizo na maana wala ulazima, wachukue maamuzi kama wanaweza wakianziasha uchunguzi nitaendelea kusema Bunge ni hovyo kuliko kawaida na ndilo linalotuletea matatizo siku zote limejaa vilaza, watoto, wazinzi, walevi, na wapenda madaraka ambao kichwani mwao hakuna kitu.

Hili swala haliitaji uchunguzi tena na hata kama linahitaji Bunge si wataalam wa uchunguzi wanataka fedha za posho tu! Jibu wanalo waliseme kama wanaweza uchunguza gani hapo.

Bunge likiamua linaweza hasa heshima yao inapoingiliwa, lakini wajue sisi wapigakura wao tunanyanyasika kila siku kwa kukosa Maji, Umeme, Huduma za afya, barabara mbovu, usimamizi mbaya wa raslimali zetu kama madini, wanyama pori, misitu, uvuvi nk. Ombi langu kwao waamue na kushikia bango9 mambo yenye maslahi kwa wananchi / watanzania

Macho yako makavu sana kiasi kwamba unashindwa hata kusoma alama za nyakati. Kwa taarifa yako harakati na wabunge wa CCM ni mkakati madhubuti wa kuwapoteza wapinzani ili wasisikike tena. Ndiyo maana hoja nyingi siku hizi zinaibuliwa na wabunge wa CCM halafu CHADEMA wanabaki kupiga mayowe kwa nyuma. Tafakari bwana mdogo.

Yawezekana!lakini mkakati wao waweza kuwa kaburi lao,maana sasa wanavuana nguo mbele ya watoto,na wanapingana wakati wao ni wamoja.kwa hali hii tutapata Ccm A,ccm B, c,d nakadhalika.Hiyo ndo itakuwa kifo cha chama cha mafisadi(CCM)

Back
Top Bottom