Kalogeresi M/kiti CCM mkoa wa Morogoro amefanya udalali kufikisha rushwa ya Abood na Shabiby kwa wajumbe Kamati ya Siasa Mkoa na kwa Polepole

T2020

Senior Member
Jul 15, 2020
131
328
Upo ushahidi wa wazi kuwa matajiri wa hapa Morogoro wametengeneza mtandao mkali wa kujinemesha kupitia maliasili zilizojaa hapa Morogoro.

Walitengeneza mfuko maalumu wa kuhonga viongozi wa wilaya, mkoa na mpaka taifa. Mfuko huo uko chini ya Abbod Azizi mbunge wa Morogoro mjini anayeomba kutetea nafasi yake.

Akisaidiana na Ahmed Shabiby wa Gairo. Viongozi hawa lengo lao kuu ilikuwa kuhakikisha wabunge wanaopita hapa ni wale wenye ngozi nyeupe na fedha. Sababu kuu wanazotoa ni kuwa washahili hawaaminiki katika biashara zao za kuchuma mali za umma.

Tayari wameshafanikiwa kumwingiza ubunge mhe. Innocent Kalogeresi mwenye asili yao, baada ya kuhonga wajumbe na kumwangusha Eng. Mtigumwe kwa kura nyingi wakihofia kuwa akimkaribia anaweza kupitishwa kutokana na ukaribu wake na Rais.

Upo ushahidi wa wazi kuwa walishakusanya kiasi kinono cha pesa wamekifikisha kwa mhe.Polepole na hivi karibuni kutakuwa na mabasi ya Polepole ndani ya kampuni ya Abbod, Shabiby na Al Saidy.

Kazi aliyopewa Polepole ni kwanza kuangalia uwezekano wa kuhakikisha mhe Amosi Makala anaondolewa licha ya kuongoza kura ya maoni ili aingie mwarabu mwenzao mhe.Sadiq mbunge wa awamu iliyopita.

Sumu atakayotumia Polepole ni kuwa mhe. Makala ni timu JK na anamhujumu JPM hoja aliyomwondoa u-RC . Kazi nyingine ni Polepole kumtetea Shabiby juu ya kuhonga wajumbe wote zaidi 600 kila mmoja 50,000 ili apate kura zote. Rushwa ambayo ilikuwa wazi kwani alitumia M/kiti CCM wilaya, madiwani wake wa zamani ambao wote pia waliongoza, Takukuru na OCD Gairo kufanikisha rushwa hiyo.

Licha ya kuongoza kura ya maoni kwa asilimia zaidi ya 98 wasiwasi wa Shabiby ni maeleano mabovu na kamisaa wa uchaguzi ambaye ni DC wa wilaya hiyo ambapo amekuwa anatumia wahuni kumdhalilisha mama huyo kwenye mikutano kwa matusi ya nguoni.

Mpaka sasa kaka yake Shabiby kiongozi wa wahuni hao ajulikanaye kwa jina la Salehe anatafutwa na polisi kwa kumtusi DC huyo .

Wasiwasi ya pili ya Shabiby ni sifa nzuri za mpinzani wake kielimu licha ya kumshinda kwa kura nyingi, Dr. Mmasa ambaye ni mhadhiri wa UDOM ana wasiwasi anaweza pitishwa.

Katika mkakati wao wamekubaliana kuachana na mwenzao aliyekuwa mbunge wa Kilosa mwenye asilii yao kwa kuogopa kumuwekea fitina za kueguliwa Prof. Kabudi kwani wanaelewa ukaribu wa Profesa na mheshimiwa Rais.

Rais Magufuli na Dr. Bashiru wanatakiwa kuwa makini sana na Polepole kwani anaonekana kutaka kujinemesha kutokana na uchaguzi huu siyo Morogoro tu mbali na maeneo mengine ya nchi yenye wagombea matajiri kama hawa wa Morogoro.
 
Niliwahi kusema, na sasa narudia tena Polepole hana usafi wowote.. Hata kwa Arusha huwa ana chukua pesa kwa mmoja wa wagombea walio tia nia ya ubunge Arusha mjini.. Hilo liko wazi!!! Ukimsikia ana ropoka utamuona ni mtu kumbe ni mtu nataka. Mh. Mwenyekiti asipo mwangalia vyema huyu jamaa ana kwenda kukipasua chama.. Sijui yuko wapi Nape..
 
Niliwahi kusema, na sasa narudia tena Polepole hana usafi wowote.. Hata kwa Arusha huwa ana chukua pesa kwa mmoja wa wagombea walio tia nia ya ubunge Arusha mjini.. Hilo liko wazi!!! Ukimsikia ana ropoka utamuona ni mtu kumbe ni mtu nataka. Mh. Mwenyekiti asipo mwangalia vyema huyu jamaa ana kwenda kukipasua chama.. Sijui yuko wapi Nape..
Nilimsikia mtia nia mmoja alidai atateuliwa kwa kuwa alishamalizana na Polepole. Hii ni hatari sana. Inawezekana lakini haya masuala yana ukweli wowote. Hakyamungu kuna shida
 
Hivi cheo cha UENEZI katika vyama vya siasa kina nguvu sana hadi kufikia hatua mtu kuinfluence jambo Fulani kama matokeo ya uchaguzi na mwenyekiti makamu katibu na wajumbe wa kamati kuu wakaufyata mkia

Kama n hvyo huko ccm polepole ni Mzito kushinda mwenyekiti
 
JPM hawezi kuwatosa Shabiby na Abbod nchi itatikisika. Anachofanya Polepole na yeye ni dalali tu wa kukusanya pesa za kampeni.
Juzi alipoenda kuchukua fomu niliyaona mabasi ya shabiby yamejaa wanaccm hapo ofisi ya chama
 
Ingawa hili bandiko limekaa kifitina zaidi, ndio kule kule tulipoaswa na Mwalimu kuwa Mtu yupo tayari kutumia sababu ya rangi, kabila, udini n.k ili kutafuta madaraka...ila suala la rushwa kwa Wajumbe sidhani kama ni jambo jipya tena, na viongozi wa juu kujifanya hamnazo wala haisaidii.

Na hata wakisema wanawachunguza watoa rushwa ili washughulikiwe wataishia kuwaadhibu Watu kwa sababu nyingine tofauti kabisa na wala sio suala la rushwa maana asilimia 90 ya watia nia walitia mia mia kwenye mifuko ya Wajumbe.
 
Back
Top Bottom