Kaliba zinazoongoza kwa wizi (kuwaibia wananchi)

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Serikali makini ingeweza kusisimamia kwa ukamilifu ingeweza kuokoa mabilioni ya wananchi maskini wenye matatizo ya kila aina. Lakini iko kimya kabisa! Je kuna namna serikali inanufaika na hizi kaliba zilizojaa wizi, utapeli na upigaji?

1. Shule za binafsi
Hizi zikijulikana kama ENGLISH MEDIUM. Ada kubwa isiyoendana na ubora wa elimu zinazotoa. Walimu vihiyo wa bei poa wasio na uwezo wa kufundisha masomo tarajiwa na waliokosa uzoefu. Ni walimu pasipo elimu
Kinachofanyika ni kuwakaririsha watoto kiingereza kuwapa maswali na kuwaandikia majibu kisha watoto wananakili halafu mwalimu anasahihisha na kuwapa alama kati ya 80 mpaka 100. Wanaokosea kidogo hupewa chini ya hapo.

Licha ya karo kubwa isiyolingana na ubora wa elimu lakini wana miradi mingine inayowaingizia pesa ya kutosha tu: miradi ya sare za shule, miradi ya usafiri, miradi ya chakula, miradi ya picnic, school day graduation nk.

2. Hospitali za binafsi
Zikijulikana pia kama private hospitals huku nako ni habari nyingine kabisa.. Yaani ni kama vile wametumwa kuuza sawa na vifaa tiba.. Na (ukubwa wa gharama haulingani kabisa na ubora wa matibabu yatolewayo.
Sehemu kubwa ya madaktari wao ni hawa hawa wa serikali, wait watoke kwenye shift zao halali na kwenda kupiga day worker.. Wengine wote ni interns ama madaktari wanaoanza Kazi.

Huwezi kwenda hizo hospitali na utoke bila kuambiwa huumwi chochote licha ya kwamba tayari umeshabamizwa ndefu kwenye vipimo. Kwenye hizi hospital ukitoka na hili ndogo kabisa ni elfu hamsini, pesa halali ya Kitanganyika.

3. Manabii na mitume
Chaka lingine la upigaji. Huko hakuna cha bure kwenye hayo makanisa yao wanayoita ya Kiroho na wengine wakiyaita vituo vya huduma. Samson aibu hata kuviita makanisa. Huko lugha ni moja tu - pesa! Hicho kinachoitwa huduma unakilipia ndefu:
  • Iwe Kuombewa
  • Iwe kubatizwa
  • Iwe ndoa
  • Iwe cheti cha safari nknk
  • Sadaka zinatolewa kwa mafungu- wale wa elfu kumikumi, wale wa elfu tanotano. Wale wa buku 2 na buku moja moja ndio kiwango cha chini kabisa cha kutoa.
Manabii na mitume hawapokei sarafu m na kwenye makanisa na vituo vyao wana miradi mbalimbali inayolipiwa:
  • Cash money
  • Mafuta ya upako
  • Udongo wa bahati
  • Maji ya baraka
  • Leso zenye upako wa mtumishi
  • Chupi za ndoa nknk
Tunafunga dimba na waganga wa kienyeji. Almaarufu kama wataalamu.. Huku kumejaa siri na watu huku wanapigwa kimya kimya lakini ndefu ndefu Huku wakipewa masharti ambayo baadhi yanawadhalolisha sana

Wanapigwa wengi ila kwakuwa haya mambo yamejaa usiri na binafsi sana husikiii wakipiga kelele hata siku MOJA na huku viongozi na wanasiasa wanaongoza kubamizwa.

Nimalizie tu kusema kuna namna serikali inanufaika na hizi kaliba ndio maana haichukui hatua thabiti kuzidhibiti. Kilichobaki ni wananchi kujiongeza

Neno la mwisho kwenye kaliba zote nilizotaja kuna wachache kiduchu ni weledi, wakweli na wasiotanguliza pesa mbele ... Hawa hawahusiki hapa na Mungu awabariki sana

Good morning Tanganyika!
 
Ila bongo urahisi ni kutafuta sehemu ambayo hakuna wizi ila sio sehemu zenye wizi

Hiyo kariakoo inanuka wizi tena wa wazi wazi na sidhani nchi hii kama kuna sehemu wizi na utapeli umehalalishwa kama kkoo. Ukiacha kule ambako mabadiliko ya nchi huanzia "sijataja ni wapi, jiseemee at your own risk" 😁😁
 
Serikali makini ingeweza kusisimamia kwa ukamilifu ingeweza kuokoa mabilioni ya wananchi maskini wenye matatizo ya kila aina. Lakini iko kimya kabisa! Je kuna namna serikali inanufaika na hizi kaliba zilizojaa wizi, utapeli na upigaji?

1. Shule za binafsi
Hizi zikijulikana kama ENGLISH MEDIUM. Ada kubwa isiyoendana na ubora wa elimu zinazotoa. Walimu vihiyo wa bei poa wasio na uwezo wa kufundisha masomo tarajiwa na waliokosa uzoefu. Ni walimu pasipo elimu
Kinachofanyika ni kuwakaririsha watoto kiingereza kuwapa maswali na kuwaandikia majibu kisha watoto wananakili halafu mwalimu anasahihisha na kuwapa alama kati ya 80 mpaka 100. Wanaokosea kidogo hupewa chini ya hapo.

Licha ya karo kubwa isiyolingana na ubora wa elimu lakini wana miradi mingine inayowaingizia pesa ya kutosha tu: miradi ya sare za shule, miradi ya usafiri, miradi ya chakula, miradi ya picnic, school day graduation nk.

2. Hospitali za binafsi
Zikijulikana pia kama private hospitals huku nako ni habari nyingine kabisa.. Yaani ni kama vile wametumwa kuuza sawa na vifaa tiba.. Na (ukubwa wa gharama haulingani kabisa na ubora wa matibabu yatolewayo.
Sehemu kubwa ya madaktari wao ni hawa hawa wa serikali, wait watoke kwenye shift zao halali na kwenda kupiga day worker.. Wengine wote ni interns ama madaktari wanaoanza Kazi.

Huwezi kwenda hizo hospitali na utoke bila kuambiwa huumwi chochote licha ya kwamba tayari umeshabamizwa ndefu kwenye vipimo. Kwenye hizi hospital ukitoka na hili ndogo kabisa ni elfu hamsini, pesa halali ya Kitanganyika.

3. Manabii na mitume
Chaka lingine la upigaji. Huko hakuna cha bure kwenye hayo makanisa yao wanayoita ya Kiroho na wengine wakiyaita vituo vya huduma. Samson aibu hata kuviita makanisa. Huko lugha ni moja tu - pesa! Hicho kinachoitwa huduma unakilipia ndefu:
  • Iwe Kuombewa
  • Iwe kubatizwa
  • Iwe ndoa
  • Iwe cheti cha safari nknk
  • Sadaka zinatolewa kwa mafungu- wale wa elfu kumikumi, wale wa elfu tanotano. Wale wa buku 2 na buku moja moja ndio kiwango cha chini kabisa cha kutoa.
Manabii na mitume hawapokei sarafu m na kwenye makanisa na vituo vyao wana miradi mbalimbali inayolipiwa:
  • Cash money
  • Mafuta ya upako
  • Udongo wa bahati
  • Maji ya baraka
  • Leso zenye upako wa mtumishi
  • Chupi za ndoa nknk
Tunafunga dimba na waganga wa kienyeji. Almaarufu kama wataalamu.. Huku kumejaa siri na watu huku wanapigwa kimya kimya lakini ndefu ndefu Huku wakipewa masharti ambayo baadhi yanawadhalolisha sana

Wanapigwa wengi ila kwakuwa haya mambo yamejaa usiri na binafsi sana husikiii wakipiga kelele hata siku MOJA na huku viongozi na wanasiasa wanaongoza kubamizwa.

Nimalizie tu kusema kuna namna serikali inanufaika na hizi kaliba ndio maana haichukui hatua thabiti kuzidhibiti. Kilichobaki ni wananchi kujiongeza

Neno la mwisho kwenye kaliba zote nilizotaja kuna wachache kiduchu ni weledi, wakweli na wasiotanguliza pesa mbele ... Hawa hawahusiki hapa na Mungu awabariki sana

Good morning Tanganyika!
Namba 3 ndo umemaliza mkuu.
 
Hapo kwenye shule nilistajabu kwamba walimu wanataja RIM kila mwanafunzi aje na yake,harafu wanazichukua wao nikapiga hesabu kama shule ina wanafunzi 200,huu si mtaji kabisa?
 
Back
Top Bottom