Kalamu ya Askofu Bagonza: Kwaheri Ole Mushi

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,839
38,736
Nimeumizwa sana na kifo cha ndugu Thadei Ole Mushi. Aliwahi kutetea hadharani haki yangu ya kuishi ilipotaka kudhulumiwa. Sikuwa nakubaliana na hoja zake nyingi isipokuwa moja ambayo ni: haki yake ya kusema na kutoa maoni yake kwa uhuru.

Alikitetea sana chama chake na alikipinga pia kwa hoja. Niliumia mno alipojitokeza hadharani kukanusha tuhuma za mchezo mchafu (kuwekewa sumu) juu ya kuugua kwake. Kama tuhuma hizo zilikua na ukweli hata robo, basi watesi wake walimtumia kujisafisha. Hakuna wa kuwachafua tena kwa sasa.

Kwa msimamo wake wa kutetea uhuru wa maoni, alitengeneza maadui ndani ya chama alichokuwa anakitetea. Chama chake kinawaheshimu na kuwavumilia wanaokikosoa wakiwa nje lakini hakina ubavu wa kuwavumilia wanaokikosoa wakiwa ndani.

Katika ombwe la fikra pevu kwa vijana wanaojihusisha na masuala ya siasa, alikuwa miongoni mwa wachache wenye kuandika na kujadili bila kutukana. Hatunao wengi.

Familia imempoteza mtu muhimu mapema. Chama chake kimempoteza Mwenezi mwenye akili na uwezo wa kujenga hoja kuliko mwenye cheo cha Mwenezi. Wizara ya elimu imempoteza mwalimu hodari aliyeipenda na kuitetea kazi yake.

Kwa heri Ole Mushi. Umeacha nchi gizani, unaenda kaburini penye giza. Yawezekana hakuna ulichopoteza, japo sisi tumepoteza. R.I.P Ole Mushi.
 
Back
Top Bottom