Kakobe amshukia Lowassa, azungumza kuhusu Kura ya Maoni

Come on...!!! don't get carried away by this money seeker Kakobe...!!!

Kakobe ni Kipenzi cha Dr. Slaa..is known...so get the facts of his political interest, ukijua hilo hupati shida...

Utakuwa kichwa boga kubwa ukiwa mtu wa kusikiliza nakumeza BILA KUWA ANALYST MZURI WA HAWA WATU WA DUNIA HII....Huyu ni mhuni tu kakobe...

Katika mahubiri yake anasema ukweli kwa kiasi kikubwa...but himself haishi katika kweli...ni msemaji wa ukweli by 75% but he does not live on facts...!!!

Hapo kamsema EL kidogo tu, ila sbb mtoa mada nae ana Team lake la kikwere au kimaembe huko, kataka kuleta upuuzi tu, hapo ktk mahubiri kamgusa JK..etc...

Pia wananchi wanaokwenda kwa EL wanatekeleza
maagizo USHAURI WA MWENYEKITI WA CCM ALIO UTOA SONGEA....sio ushauri au maneno ya Kakobe..!!!

So shut up, and let the tough EL get going....!!!

Sikia, tafakari ukweli halisi, chukua hatua, b4 hujaandika urojo rojo..!!!
Ukisoma bila kuwa biased kiasi hicho utamwelewa kuwa analitetea taifa kama Mchungaji.
Aidha uelewa wa watu hutofautiana kutokana na ideologies zao, backgrounds, levels of education, etc.
Kwa hiyo usitegemee wote tutakuwa na mawazo kama yako juu ya tamko la Kakobe.
Uaweza kueleweka hata bila kuwatukana watu mkuu.

Kwa uelewa wangu, the man is right.
 
Angekuwa hivi miaka yt heshima ingekuwa juu sana. Lakini aliharibu sana kuingia mitaani akisema Mungu kasema Mrema awe rais wa nchi hii.
Af Mungu wake akashindwa kuzuia kile alichokiita kakobe wizi wa kura wa ccm
 
Kakobe anamgombea wake? Wengi wanamtaka Lowassa kutokana na Deliverables zake ... so what? ...
 
11146594_819821808095000_3095277516678804591_n.jpg
 
Hao viongozi wa dini wana matatizo ya akili? Si walishaambiwa mambo ya siasa waachie wenyewe?

Siasa haina mwenyewe; kila binadamu ni mwanasiasa na ndiyo maana hata wewe unashiriki kwa kuandika uzi hapa. Mwanafalsafa wa kale wa Kirumi alipata kuandika kuwa binadamu kwa asili ni mnyama-mwanasiasa. Hao wanaotaka watambulike kuwa wao tu ndio wanasiasa ni watu ambao wameamua kutumia siasa kama ngazi ya kuwafikisha wanakotaka kufika. Wengi wao wanasukumwa na tamaa za mali na uroho wa madaraka.
 
Hivi hawa maaskofu wamekuwa wanasiasa au? mtu unaenda kusali nshu ya urais inakujaje kanisani? huku naona nikwenda kubaya

Mwanzo wa mahubiri yake kaeleza majukumu yake kama mwalimu. Naona wewe sasa unataka kubadili job description ya mwalimu anayejua kazi yake.
 
Akihubiri siku ya Pasaka katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship lililopo Mwenge katika Jiji la Dar-Es-Salaam, Askofu Mkuu Zachary Kakobe alisema kwamba, inajulikana wazi kwamba Lowassa amekuwa anautaka Urais kwa udi na uvumba kwa miaka mingi, hata mwaka 1995 alijitosa hadharani kuuwania, sasa anapodai kwamba hivi sasa kuna makundi yanayokwenda kwake kumshawishi agombee Urais, kana kwamba yeye hataki Urais, anakuwa anamdanganya nani?


Ingawa katika mahubiri hayo ya saa mbili, Kakobe hakumtaja Lowassa kwa jina, hata hivyo Kakobe alisema, "Wako watu wengine ambao inajulikana wazi kwamba wamekuwa wakiutaka Urais kwa udi na uvumba, kwa miaka mingi, lakini hivi sasa wanasema kuna makundi ya watu yanawafuata nyumbani, kuwashawishi kugombea Urais; kama vile hawautaki Urais, hivi watu hawa wanamdanganya nani?

"Na wale wanaokwenda kumshawishi mtu ambaye kwa miaka mingi, anajulikana kwamba anautaka Urais, hawajui kwamba nao wanafanywa kuwa wajinga? Mtu anayejulikana kwa muda mrefu kwamba anautaka Urais, ni vema akatangaza tu moja kwa moja nia yake, bila haja ya ghiliba."

Katika mahubiri yake yenye kichwa, "UPOTOSHAJI WA UKWELI", Kakobe alieleza jinsi Gavana wa Kirumi, au liwali Pontio Pilato, alivyojiunga na Viongozi wengine kupotosha ukweli wa kufufuka kwa Yesu, na kusema kwamba wanafunzi wake waliuiba mwili wake, wakati askari walinzi walipokuwa wamelala, na kuwadanganya watu, ingawa wao wenyewe waliujua ukweli.

"Pilato aliwadanganya watu hao kwa muda tu, lakini hatimaye ukweli ulikuwa dhahiri, walipomwona Yesu kati yao kwa muda wa siku 40. Unaweza kuwadanganya watu kwa muda tu, lakini hatimaye ukweli hudhihirika, na kumfedhehesha yule aliyeupotosha ukweli huo", alisema.

Aliendelea kusema kuwa, hata leo kuna upotoshaji wa kweli mbalimbali za kiroho na kimwili. Baada ya kuelezea juu ya baadhi ya kweli za kiroho zilizopotoshwa, aliwageukia wanasiasa waongo, akianza kwa kutoa mfano wa Waziri wa Habari wa Iraq, wakati wa vita ya mwaka 2003, Muhammad Saeed al-Sahhaf, aliyekuwa akipotosha ukweli kuhusu jinsi Iraq ilivyokuwa inapigwa vibaya katika vita hivyo, na akaendelea kusema;

"Kabla sijaendelea, nifafanue kwanza juu ya watu wanaopotosha ukweli, kwa kusema kwamba eti Wachungaji hawapaswi kuwakemea wanasiasa wananapopotoka. Watu hawa hawajui Biblia. Katika MAMBO YA WALAWI 4:22-23, Biblia inasema, Mtawala akifanya dhambi, inampasa Kuhani yaani Mchungaji, kumjulisha dhambi yake."

Kakobe aliendelea kusema kwamba huu ni mwaka wa Uchaguzi, hivyo Watanzania wawe makini na wanasiasa waongo wanaofanya uongo kuwa sehemu ya siasa zao.

"Siasa, ni Sayansi, inaitwa POLITICAL SCIENCE, na "any kind of science only deals with facts". Wanasiasa hawana budi kuwa wakweli kwa kuwa siasa ni sayansi.

"Siasa siyo mchezo mchafu, bali baadhi ya wanasiasa ndiyo wachafu. Msidanganywe tena na wanasiasa ambao watakuja kwenu mwaka huu na ahadi za uongo za kuibadili miji na kuifanya kuwa kama New York, kwa miaka mitano; na wengine hawana AIBU, wanaweza hata kuwaambia wakazi wa Dodoma kwamba watawaletea meli! Hamna budi kuyachunguza kwa makini maneno yao, na kuona kama ni ya kweli."

ENDELEA HAPA: Kakobe Amshukia Lowassa, Awataka Watanzania Kususia Kura Ya Maoni Kwa Madai Kuwa Katiba hiyo ni ya Kishetani na Mwandishi Wake Ni "Nyoka Wa Makengeza" ( Shetani) | UDAKU SPECIAL
 
namuombea aendelee kuwa KAKOBE.. maana siku mungu akimpandisha na kuwa KOBE kamili itakuwa sheeedah. huyu ndiye aliyetuaminisha kuwa eti AUGUSTINO LYATONGA MREMA NI chaguo la mungu!!!!
hahahahaaaaa mungu wa kakobe ni full MAGUMASHI kama ilivyo elimu ya MBOWE
 
Kwa taarifa yako umeme huo haujapita mpaka leo. Hivi ulisha chunguza umeme huo ulikopita kuna majengo makubwa makubwa na watawala kwa kuwaogopa wawekezaji uchwara wa mlimani City ambapo umeme huo ulipaswa upite, eneo toka Ubungo hadi Mlimani City upande huo hakuna watu bali ni pori tupu kwa nini umeme huo usingepita huko?Lakini wawekezaji hao walikataa na ndiyo maana sehemu au upande wenye maendeleo nguzo za umeme huo zilipitishwa. Mpaka leo umeme huo toka ubungo uligoma kupita kanisani hapo. Uongo umetumika, Ngereja na mawaziri wote waliopita baada wanajua kuwa umeme haupiti pale. Ndiyo maana mradi huo umeshindikana kuuzindua. Nenda kaulize TANESCO kama umeme huo unapita pale Kanisani!
 
Kwa taarifa yako umeme huo haujapita mpaka leo. Hivi ulisha chunguza umeme huo ulikopita kuna majengo makubwa makubwa na watawala kwa kuwaogopa wawekezaji uchwara wa mlimani City ambapo umeme huo ulipaswa upite, eneo toka Ubungo hadi Mlimani City upande huo hakuna watu bali ni pori tupu kwa nini umeme huo usingepita huko?Lakini wawekezaji hao walikataa na ndiyo maana sehemu au upande wenye maendeleo nguzo za umeme huo zilipitishwa. Mpaka leo umeme huo toka ubungo uligoma kupita kanisani hapo. Uongo umetumika, Ngereja na mawaziri wote waliopita baada wanajua kuwa umeme haupiti pale. Ndiyo maana mradi huo umeshindikana kuuzindua. Nenda kaulize TANESCO kama umeme huo unapita pale Kanisani!
 
Hao viongozi wa dini wana matatizo ya akili? Si walishaambiwa mambo ya siasa waachie wenyewe?

wakuachie wewe ma mama yako waongo na Baba yenu shetani, hivi unafuraia nini kuhusu ccm yako inayofanya mambo kwa kulazimisha bila kujali vizazi vijavyo. Hivi huyu kikwete Ni lini atatambua kuwa Mungu hadhihakiwi na mbegu upandayo ndo utavuna?????
 
wakuachie wewe ma mama yako waongo na Baba yenu shetani, hivi unafuraia nini kuhusu ccm yako inayofanya mambo kwa kulazimisha bila kujali vizazi vijavyo. Hivi huyu kikwete Ni lini atatambua kuwa Mungu hadhihakiwi na mbegu upandayo ndo utavuna?????

Ya ngoswe mwachie ngoswe...sio busara viongozi wa dini kujiingiza kwenye siasa
 
Hongera kakobe.waambie ukweli na wala usimung'unye mane no.
Shetani ni shetani tu no matter wewe mwislam alma mkristo
 
safi sana mtumishi wa mungu , unakusanya wachuuzi wa samaki wa feri halafu unadai ni mashehe wa bagamoyo ! huu ni utapeli wa kiwango cha chini sana , iko wazi kwamba 1995 uliomba urais ukatimuliwa na Nyerere halafu eti leo ndio unaombwa !
 
Maneno ya busara kabisa kutoka kwa mtumishi wa Mungu. Endelea kuwafundisha waumini mambo yaliyo makuu mteule wa Mungu.
 
Tunawataka watumishi wa mungu kama hawa,ni fahari kuwa na mtumishi kama kakobe katka nchi yetu hii,mungu ambariki huyu mtumishi.
 
natamani lowassa asipite apite hyo Bernard membe muon kam nchi itakalik
wakati mwingne tumia akili kidog kuliko nguvu hizo juhudi huo uongo na uzushi hizo nguvu unazotumia kumkandamiza lowassa mteule wa Mungu ipo siku utalia machozi ya damu na kujilaani mwenyw kwa kulihadaa taifa
time always is the best judge
 
Back
Top Bottom