Kairuki: Uhamisho wa watumishi wa umma uzingatie vigezo

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amezitaka Taasisi za Serikali kuratibu suala la uhamisho wa watumishi wa umma kwa makini pale inapohitajika kufanya hivyo Ili kuepuka kero na usumbufu kwa watumishi.

Waziri Kairuki (Mb) amesema hayo jana katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala eneo la Segerea, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki alisema uhamisho lazima ufanyike kwa mtumishi wa umma endapo kukiwa na sababu za msingi sana. “Naomba ieleweke kuwa uhamisho una taratibu zake hivyo kila mwajiri ni bora akazifuata.” Mhe. Kairuki alisisitiza.

Aliongeza kuwa imebainika wapo baadhi ya watumishi wa umma wanawasilisha sababu mbalimbali kwa waajiri kuomba kuhama wakiwa na nia ya kukwepa kukaguliwa sifa zao za elimu.

Waziri Kairuki alisisitiza kuwa uhamisho usifanyike kwa mtumishi ambaye anaonekana kuwa na matatizo.

“Baadhi ya waajiri wamekuwa na tabia ya kuwahamisha watumishi wa umma ambao wameonekana kuwa na tatizo na kuwahamishia sehemu nyingine, uhamisho wa namna hii haukubaliki, tatizo la mtumishi linatakiwa kufanyiwa kazi kwenye kituo chake cha kazi na sio kupeleka tatizo sehemu nyingine.” Mhe. Kairuki aliongeza.

Mhe. Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama ambapo leo ni siku ya tisa akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala-Segerea kwa kukutana na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.

Waziri Kairuki katika vikao kazi alihimiza watumishi wa umma nchini kubadili mtindo wa maisha, kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi, kujiepusha na ugonjwa wa UKIMWI, na Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa (MSY).

Lengo la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.
 
mbona hazungumzii uhamisho uliosimamishwa? kuna matatizo yashughulikiwe kituoni je matatizo kama maradhi yatashughulikiwa kituoni? toeni nyongeza ya mshahara na majibu juu ya watumishi walioomba uhamisho tokea mwaka jana uwe na utu we mama
 
Hao watumishi aliokua anaongea nao lazima ni mazwazwa...

Sijaona key ishuuzz zikijibiwa..

Madaraja
Ajira
Uhamisho
Arrears


..,..... Ziara haina maana kabisa. Wanaume wa Dar bhana..
 
Haya yetu subira, ngoja tusubiri utatuzi wa hizo kero anazozisikiliza......
 
Sisi tumejaribu na mwenzangu kutafuta uhamisho kutoka halmashauri ya wilaya ya Mbulu kuja babati manyara. Yote na ndani ya mkoa lkn tumekuwa tukikutana na kikwazo cha kuambiwa mwenzangu atafute mwalimu mwenzake wa kubadilishana naye. Tunapitia kipindi kigumu kama wanandoa, ndoa ni changa, watoto ni wadogo lon tumeshindwa kuwa pamoja hata kimalezi. Serikali inaandaaje taifa lenye watu wasiopata malezi ya wazazi wakati wa utoto wao. Najisikia vibaya mno tunanyanyasika kwa kweli
 
Back
Top Bottom