Kaimu Kamanda wa Polisi Arusha: Uhalifu wa wana CCM si Uhalifu!

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
Kufuatia kukamatwa kwa Dr. Slaa, Lissu Pamoja na Wanachama wengine wa CDM waliokuwa kwenye mkesha wa Amani, Kamanda Mpwapwa jana alishindwa kueleza sababu za jeshi hilo kushindwa kuwachukulia hatua vijana wa CCM, walioandamana na kufanya mkutano wa hadhara bila kibali licha ya jeshi hilo kuyapiga marufuku."Pamoja na matukio haya kufanana na eneo la tukio kuwa sawa, lakini polisi tunashughulikia kila shauri kulingana na mazingira yake. Kisheria mtu huwezi kutenda kosa kwa sababu mwingine naye ametenda kosa kama lako," alisema Mpwapwa baada ya waandishi kuhoji kwa nini Chadema wamekamatwa kwa kosa linalofanana na lililotendwa na vijana wa CCM ambao hawakuguswa?

Hapa kamanda anadhihirisha kuwa humu nchini CCM wakifanya kosa Sheria si lazima kufuatwa na si lazima hatua kuchukuliwa dhidi ya uhalifu wa wanaCCM. Anataka kuueleza umma kuwa Polisi wapo makini zaidi na makosa ya baadhi ya watu/chama fulani. Kama vivyo ndivyo basi mishahara nayo kwanini msilipwe na CCM??Mbona mnatubagua wakati ni kodi zetu ndizo zinazowapa maisha?? Hivi utendaji huu wa kipuuzi kabisa utaisha lini????Kwanini sheria za nchi zinawabana watu au kikundi cha watu wachache tu???Hii nchi kweli inafuata utawala wa sheria au ni ushenzi mtupu??


Source Mwananchi 09/11/2011
 
Yuko right kisheria, ila nadhani hana busara kwa sababu anatengeza mazingira magumu ya nchi kutawalika kisheria kwa vile anasahahu kuwa jambo analushughulikia ni la kisiasa zaidi ya kisheria. Anazidi kuchafua jeshi la polisi lionekana kuwa linatumiwa kisiasa: kuwa wahalifu wa chama fulani hashughulikiwi kabisa na polisi
 
Kamanada ana AKILI nzuri na timamu, lakini anatatizo la Utu na Ubinadamu katika kutumia Hekima na Busara. Mambo ambayo hayaendi kwa misukumo ya Kiakili na lililotazo la vinogozi wengi kwa sasa. Tatizo hili hatimaye lianakuwa shina la Usugu wa Matatizo megi ya Kijamii na kKtaifa.
 
Kamanada ana AKILI nzuri na timamu, lakini anatatizo la Utu na Ubinadamu katika kutumia Hekima na Busara. Mambo ambayo hayaendi kwa misukumo ya Kiakili na lililotazo la vinogozi wengi kwa sasa. Tatizo hili hatimaye lianakuwa shina la Usugu wa Matatizo megi ya Kijamii na kKtaifa.

Mtu mwenye akili hawezi kutoa maelezo ya aina hiyo!
 
Mtu mwenye akili hawezi kutoa maelezo ya aina hiyo!

Mtoboasiri, Hujaona mtu ana PhD ..anafika nyumbani wa kwanza anakula chakula cha Watoto na anakuwa wa kwanza kulala, watoto wanakuja wanalia njaa yeye anakoroma ...! Si unajua hilo halimuondolee Digirii zake tatu eh! ..lakini ..UTU na UBINADAMU ...Bureee kabisa ..0%. Huyo huyo Mpe uwaziri atasaini mikataba feki ya mamilioni kwa hasara ya taifa, yeye akipewa rushwa ya bajaji ...Huyo huyo mpe ukamanda wa Polisi ... Lol!!
 
police tz akili zao zote wameshikiwa na magamba......wasubiri siku wanabaki wenyewe na akili zao waone tukavowafanya mbaya
 
Chanzo cha yote ni kukataa dhamana,majuto ni mjukuu
Nimeshindwa kukuelewa, kwani dhamana inapokuwa wazi inakataliwa kwa sababu aliyekuwa anapewa aliikataa? Maamuzi yalibadilika lini? kwanini? na yalibadilishwa na nani kwa ajili ya nini? Kama dhamana ilikuwa wazi mahakamani, kesi haikutajwa tena dhamana ilifutwa lini nje ya mahakama? Kwanini dhamana ilitufutwa bila kuwepo mlalamikiwa. Kesi ilitajwa tena nje ya siku dhamana ilipotajwa kuwa ipo wazi? Mahakama ya Arusha haikufuata sheria imefuata ilani ya CCM kutekeleza amri haramu
 
Back
Top Bottom