Wanabodi,
Baada ya figisu figusu za uchaguzi wa marudio wa madiwani, nimebahatika ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima, yaliyofanyika ofisini kwake jioni hii, kuhusu uchaguzi huo, katika kipindi cha Habari Zaidi ya Habari na PPR, ambacho kinarushwa kupitia Vituo 5 vya TV, TBC, ITV, STAR TV, Channel Ten, Azam TV, Clouds TV na kwenye Youtube.
Hizi ni Baadhi ya Dondoo za Mahojiano Hayo.
My Take.
- Zoezi la Uchaguzi limekwenda vizuri kwa asilimia 95%, hakukuwa na kasoro yoyote kubwa kuathiri uchaguzi huo, hivyo uchaguzi umekamilika na taarifa rasmi, itatolewa punde itakapokamilika.
- Uchaguzi huo ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki, licha ya kutokea mapungufu madogo madogo, lakini matokeo ni matokeo halali, aliyeshinda ameshinda kihalali kwa haki, aliyeshindwa, pia ameshindwa kihalali kwa haki.
- Hakuna hata chama kimoja, kilicholalamikia jambo lolote kuhusu uchaguzi huo, mpaka sasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, haijapokea malalamiko yoyote, kutoka chama chochote, au mgombea yoyote kwa mujibu wa utaratibu wa kujaza fomu za malalamiko.
- Hakuna chama kilichojitoa rasmi, ila kama ilivyo kushiriki uchaguzi ni hiyari, vivyo hivyo vyama viko huru kujitoa wakati wowote, lakini mpaka zoezi la uchaguzi linamalizika, hakuna chama kilichojitoa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kujitoa.
- Mawakala wa vyama, wanapatikana kwa mujibu wa sheria, taratkanuni, mtu ambaye hajakidhi taratibu za uchaguzi, hawezi kuruhusiwa
- Ameelezea kuwa Tume yake ni Tume huru, inayoendesha chaguzi kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, hakuna chama chochote, kimewahi kulalamikia kipengele chochote cha uchaguzi kinachonyima haki, kitakachoifanya tume isiwe huru.
- Amesisitiza Tume yake haijawahi kuingiliwa na chombo chochote, wala kupokea maagizo au maelekezo kutoka kwa yeyote.
- Tume yake haijawahi kufanya upendeleo wowote kwa chama chochote, hata CCM nayo pia inailalamikia tume yake, hata uchaguzi wa Madiwani CCM Arusha wamelalamika.
- Pia nimeuliza kuhusu Mkurugenzi, Mwenyekiti wa NEC na makashna kuteuliwa na rais ambaye ni mwenyekiti wa chama kimoja, wataweza kutenda haki?, pia amelijibu.
Its high time vyama tuanze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, tukubali kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani, badala ya kutafuta visingizio.
Kama hali ya uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania, jee hali itakuwaje uchaguzi wa 2020?. Kama wapinzani hawatabadili strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye sanduku la kura, kuna hatari ya CCM, kuyarejesha majimbo yote ya upinzani mwaka 2020, hivyo Tanzania kuanza safari ya kuelekea kuwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini ukweli tunaelekea kuwa nchi ya chama kimoja.
NB. Kipindi kikiwa tayari, nitakipandisha humu umsikilize mwenyewe.
Wasalaam.
Paskali
Nakubaliana na wewe asilimia zote!Kwa hivyo wangejitoa wakati vitimbi vimeanza baada ya uchaguzi kuanza? Shameless kabisa
Ninyi stahiki yenu ni hii
20 Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!
Isaya 5 :20
Kwenu mtu akifa huwa mnasubiri daktari aandike ripoti kuwa huyu kafa? Si we mwenyewe unaona tu mtu kweli kafa na dokta anakwambia tu kafa then taarifa baadae?
Ninyi ndiyo waandishi mnaotuharibia nchi hii sio siri.
Nimeongea nikiwa huru sina kadi ya chama hapa
Hivi Ile Ripoti Maalum Ya Kamati Ya Ulinzi Na Usalama Ya Bunge Kuhusu Kushambuliwa Kwa Mh. Tundu Lissu Tuliyoambiwa Itasomwa Kwenye Bunge La Mwezi Wa 11 Ilipotelea Wapi? Mbona Hiyo Ripoti Hatujaisikia?Inasikitisha sana wewe hoja ya msingi kwako ni BUNGE LIVE na mikutano, watanzania hawataki kusikia hoja za kijinga namna hii. Endeleeni kupasha benchi joto mpaka mtakapopata akili.
Pascal Mayalla unapaswa uelewe kuwa Tume iliratibu uhuni uliofanyika jana. Huu sio uchaguzi wa kwanza kufanyika Tanzania. Figisu tulizoziona jana kimsingi zinafuatia agizo la Rais la kutaka Wagombea wa CCM watangazwe hata kama hawajashinda. Mana alisema "inashangaza watu tunawalipa mishahara, tunawapa magari na tunawawekea Mafuta halafu mnawape ushindi wapinzani". Hii kauli ndio iliyopelekea Polisi kuwa eyes off, hands on katika kuhakikisha CCM inashinda kwa dhurma hata ikibidi kuua. Hakuna siri tena kuwa figisu za tume za kutokuwaapisha wasimamizi kwa wakati na kwa utaratibu ulio wazi ilikuwa ni sehem ya mkakati huo.Mkuu BAK, uchaguzi ni process yenye sheria, taratibu na kanuni, zikiwemo taratibu za kuripoti malalamiko yoyote, kama hayo yote yametokea na hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, hadi uchaguzi unakamilika, hakuna yoyote aliyelalamika!, na hata kule kujitoa kwa Chadema, haikujitoa bali ilisusa tuu, kama ilivyo kanuni, unakuwa mgombea kwa kujaza fomu, na kujitoa ni kwa kutoa taarifa rasmi ya maandishi, na sio kuwaambia tuu waandishi wa habari. Tangazo lile ya kujitoa, lilipaswa kufuatiwa na kujaza fomu ya malalamiko, na kutoa taarifa rasmi ya kujitoa. Kama hakuna malalamiko yoyote registered, then tume iko right, no one complained!.
Paskali
Mauaji yapi kwenye uchaguzi yametokea? Jana na leo nimeangalia taarifa za habari chanel 10, azam na itv sijasikia taarifa ya mauaji.kama wewe umeshindwa kukemea mauaji kwenye uchaguzi siwezi kushangaa kwanini unapinga hoja hizo
Matendo yapi??Hii kitu chukulieni maguzi lakini madhara yake sio kwa mihemko tujione kwa kuwa ni ccm basi haina madhara kwetu. Madhara yetu ktk chama yako wazi yaani hatujuamini kutokana matendo yetu ndo yanatutafuna
Unaniuliza mimi kama nani??Hivi Ile Ripoti Maalum Ya Kamati Ya Ulinzi Na Usalama Ya Bunge Kuhusu Kushambuliwa Kwa Mh. Tundu Lissu Tuliyoambiwa Itasomwa Kwenye Bunge La Mwezi Wa 11 Ilipotelea Wapi? Mbona Hiyo Ripoti Hatujaisikia?
ila pia kutokukubali kushindwa kwa vyama tawala ni tabia ya hili bara la giza, kwa kutumia vyombo vya dola vinavyomilikiwa na serikali ya chama tawala ilikuendelea kuwepoKutokubali kushindwa ni tabia ya vyama vya upinzani vya hili bara la giza
So sijashangazwa na taarifa za CHADEMA za kutokubali matokeo
Kama.sheria ya kujenga kwenye mita zisizokubalika imepelekea sehemu jengo la Tanesco kubomolewa,kuwq na cheti feki ni kosa la jinai na wafanyakazi wa hivyo wameondolewa kwenye nafasi zao.Inasikitisha sana wewe hoja ya msingi kwako ni BUNGE LIVE na mikutano, watanzania hawataki kusikia hoja za kijinga namna hii. Endeleeni kupasha benchi joto mpaka mtakapopata akili.
Mku ss ni watanzania yaani ni wamoja sio mpaka mtu afe ndo tuone kunashida imetoka mtu awe amezuiwa kutimiza haki yake ya kikatiba kama amezuiwa kwa virungu au kwa uonevu hii ni mbaya hata kwa amwaccm mkomavu haiwezi kutusapoti chama kwani hawezi kujitetea chama mbele ya jamii kwa maswali yatakuwa mengi kutoka ktk hiyo jamii .Mauaji yapi kwenye uchaguzi yametokea? Jana na leo nimeangalia taarifa za habari chanel 10, azam na itv sijasikia taarifa ya mauaji.
Alafu hayo 'mauaji' ndo yangezuiliwa na bunge live unalotaka??
Ufipa mnasomeshwa ujinga.