Kahangwa aachana na NCCR!

Kaka, nakumbuka tuliwasiliana last time June last year.

Bado upo NCCR? Una mpango gani na NCCR? Unazionaje siasa za sasa?

Mkuu Invisible,
Mwaka wa tatu sasa siko nchini. Hata hivyo najitahidi kufuatilia kwa karibu yanayojiri huko nyumbani. Siasa za sasa hazina afya, japo matatizo ya msingi yanayoikabili nchi yanajadiliwa sana lakini hakuna linalotatuliwa. Najiuliza sana tunafanya nini... au tunazunguka mlima kama waisrael walivyouzunguka Sinai wakidhani wanasafiri kumbe hawaendi popote, mpaka waliposhtuliwa kwamba; 'mmezunguka sana hapo, songeni mbele'. Nafuu pekee ninayoiona ni kwamba wanamageuzi wanaeleweka zaidi kwa wananchi kuliko tulikoanzia. Yamkini tufuate kwa utimilifu hatua alizopendekeza Paulo Freire, yaani kuwaonesha watu kwamba wako katika ukandamizwaji, kuwafundisha kwamba mabadiliko yanawezekana, kisha kuwaongoza katika hatua za kuleta mabadiliko hayo. Tanzania tunayo mengi ya kufanyia mabadiliko... ufisadi, yes, lakini yapo na mengine ambayo uzito wake ni sawa na wa ufisadi. (Nimejaribu kuandika muhtasari)
 
bila kutoa sababu na kusema umejitahidi kuzitatua kwa kiwango gani na vikwazo vilivyokuzuia kufanikisha mipango hiyo hutufai....NCCR mageuzi cyo chama makini labda uunde chako...au uende SISI M....sisi CDM tunahitaji watu wanaokwenda na wakati na wasiogopa jela wala bunduki unaweza? na je yakitokea unakwenda bado utahama?...NAfuu uunde chako kaka

Ndugu Mchaichai, sikufai wewe na nani? Hii thread ni ya siku nyingi. Aidha aliyeleta taarifa aliambiwa mayai, yeye akasema kuku. Fununu tu ya unachotaka kusikia; sheria za Tanzania haziruhusu watumishi wa umma kuwa viongozi katika vyama vya siasa.
 
Mkuu Invisible,
Mwaka wa tatu sasa siko nchini. Hata hivyo najitahidi kufuatilia kwa karibu yanayojiri huko nyumbani. Siasa za sasa hazina afya, japo matatizo ya msingi yanayoikabili nchi yanajadiliwa sana lakini hakuna linalotatuliwa. Najiuliza sana tunafanya nini... au tunazunguka mlima kama waisrael walivyouzunguka Sinai wakidhani wanasafiri kumbe hawaendi popote, mpaka waliposhtuliwa kwamba; 'mmezunguka sana hapo, songeni mbele'. Nafuu pekee ninayoiona ni kwamba wanamageuzi wanaeleweka zaidi kwa wananchi kuliko tulikoanzia. Yamkini tufuate kwa utimilifu hatua alizopendekeza Paulo Freire, yaani kuwaonesha watu kwamba wako katika ukandamizwaji, kuwafundisha kwamba mabadiliko yanawezekana, kisha kuwaongoza katika hatua za kuleta mabadiliko hayo. Tanzania tunayo mengi ya kufanyia mabadiliko... ufisadi, yes, lakini yapo na mengine ambayo uzito wake ni sawa na wa ufisadi. (Nimejaribu kuandika muhtasari)

Bado ni muhtasari, na hasa ukijua ilikuwa 2008!
 
Unamaanisha wewe ni mtumishi wa serikali? Na hii ndo sababu uliamua kujiuzulu uongozi NCCR?
Ndugu Mchaichai, sikufai wewe na nani? Hii thread ni ya siku nyingi. Aidha aliyeleta taarifa aliambiwa mayai, yeye akasema kuku. Fununu tu ya unachotaka kusikia; sheria za Tanzania haziruhusu watumishi wa umma kuwa viongozi katika vyama vya siasa.
 
Dah, wakuu hapa walimvaa kwelikweli.

Kahangwa, c'om brother. Hebu tuabarishe nini kimekusibu! The last topic nakumbuka ilikuwa challenge kubwa kwako ni ile ya NCCR na Maslahi ya Taifa

dah,
Siasa bana ni Kama harusi, mnapokua mnaoana vigelegele vinakua viiingi kwelikweli.
Siku mkija kuachana ndio utasikia Mara "halikua chaguo langu",
sijui "mtu mwenyewe Malaya",
utasikia "kanipotezea muda wangu",
Mwingine "Sikua najua kamandio yuko hivyo"
Kwani hukuyajua hayo yote?
Ulishikiwa bunduki ujiunge nae?
 
Juzi uko NCCR ukawaita wenzio Maadui,
Leo unjifikiria mara mbilimbili kama ujiunge nao AMA vipi.
 
Kila lenye mwanzo lina mwisho, naamini hata Mbatia sio m/kiti wa maisha wa nccr. Wakati wa mabadiliko ukifika, hakuna atakayezuia.

Demokrasia ya kweli inavumilia uhuru na utashi wa mtu mmoja mmoja, ila inapofikia maamuzi magumu si lazima kudai eti wengi wape. Tuiachie nguvu ya umma ifuate mkondo wake, na misingi ya demokrasia itaimarika nchini mwetu.
 
kama alichukua mda mrefu hivi kuelewa ukweli hafai chama chochote

Hapa mnajadili kitu ambacho sicho. Naomba niwaweke wazi
1. Nilijiunga na NCCR-Mageuzi mwaka 1995
2. Mwaka 2007 niliajiriwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
3. Hiyo 2008 (mwaka ambao hii thread ilianzishwa hapa) nilijiuzuru uongozi katika chama kwa sababu ya huo utumishi wa umma, na mchagizo wa safari ndefu iliyokuwa mbele yangu.
4. Tangia wakati huo siko nchini (ila mara kwa mara nakuja likizo)
5.Kadi yangu ya uanachama wa NCCR-Mageuzi ingali hai. Naendelea kushirikiana na katibu mkuu katika masuala ya falsafa na itikadi ya chama.
6. Uanachama wangu katika chama hiki si wa kufuata mdundiko, bali misimamo ya kiitikadi.
 
Mkuu mimi husema pale penye ukweli ingawa unauma sana. Siasa nchini ni siasa za kuchumia tumbo, hakuna itikadi isipokuwa tunaiga majina kujenga chama. Vyama vyote viongozi wake wengi ni Opportunist, wachumia tumbo na ndio maana unaona wao wakiishi maisha ya juu kuwaongoza maskini. Hakuna mgombea Urais aliyepitia maisha ya umaskini, udhalilishwaji na kadhalika hivyo naweza tu kusema siasa za Bongo ni Unafiki mtupu.

Viongozi wote wanagombania vyeo, na hakika akipatikana Che Guevara mmoja tu na kupigania kweli haki za kundi la watu anaowawakilisha ndipo tutapata Itikadi ya kweli maana katiba sio itikadi bali ni mwongozo wa watu kama ilivyo Biblia. Usipoifuata biblia ktk maisha yako na kuamini uloyasoma na ukaishi kama unavyoagizwa,huwezi kuwa mcha Mungu bali muumini mwanachama wa dini ama dhehebu hilo! Hii ndio sababu ilonishinda na siasa za Bongo!
 
Napenda sana ninapoona thread za zamani hapa Jf!
Hasa zinapofanyiwa mapitio mara ya kadhaa.
Nadhani inalazimu kuheshimu misimamo yako binafsi.
Ndio hili lilikuwa suala lako binafsi na labda sana na chama chako.
Tena kama bado una mahusiano na chama hcho basi hii inatosha kabisa kufifisha mjadala. Labda kama ntasaidiwa kuonyeshwa mantiki ambayo sijaiona..
Agenda endelevu mpaka sasa kwa huku nyumbani ni MABADILIKO CHANYA KWA KIZAZI HICHI NA KIJACHO
 
Ahsante Ndugu yangu Mkandala. (Kumradhi, napenda sana tuitane ndugu kuliko mkuu, binafsi mimi sio mkuu katika chochote). Ni wapi tumtafute 'Che Guevara' wa Tanzania? Nadhani kwa kuwa mimi na wewe ni watanzania, tuanzie hapo katika seti ya memba mbili. Aidha masikitiko yako kuhusu siasa kuvamiwa na watu wanaotafuta maslahi yao binafsi, ndio masikitiko na ya wengine wengi; kumbe tufanye nini? Busara ziliishatufundisha cha kufanya; nuru ilishinde giza, wema uushinde uovu. yamkini tatizo si tu kuongezeka kwa wanasiasa wanaotafuta maslahi binafsi bali pia uwepo wa watu wema wasiotaka kufanya chochote.
 
Napenda sana ninapoona thread za zamani hapa Jf!
Hasa zinapofanyiwa mapitio mara ya kadhaa.
Nadhani inalazimu kuheshimu misimamo yako binafsi.
Ndio hili lilikuwa suala lako binafsi na labda sana na chama chako.
Tena kama bado una mahusiano na chama hcho basi hii inatosha kabisa kufifisha mjadala. Labda kama ntasaidiwa kuonyeshwa mantiki ambayo sijaiona..
Agenda endelevu mpaka sasa kwa huku nyumbani ni MABADILIKO CHANYA KWA KIZAZI HICHI NA KIJACHO

Mabadiliko, yes. Hiyo ndio imekuwa ajenda yetu wanamageuzi tangu mwanzo. Tuliona jinsi mifumo iliyokuwepo miaka ya 90 (na mingine inaendelea kuwepo) kwamba ilikuwa haifai. Tulianza na suala la katiba, hatua kidogo ikapigwa, mfumo ukabadilika toka chama kimoja hadi vingi.Lakini hilo halikuwa na maana kwamba ndio tumemaliza, jitihada bado zinaendelea na matumaini yapo, kwamba hatimaye katiba mpya itapatikana. Wakati huo huo tunashughulikia uondoaji wa mifumo mingine mibovu, matharani mfumo wa ufidadi (katika hili Chadema nawapigia saruti), ipo mingine ... aruta continua! Bahati mbaya wakati fulani jitihada zetu zinakwamishwa na misigishano yetu sisi wenyewe; wanamageuzi. Laiti kama tungeendelea kutambua kwamba sisi wanamageuzi ni ndugu katika siasa na katika uraia. Mageuzi kama dini, NCCR, CHADEMA, CUF na wengine ni madhehebu ya dini hii. Historia ya Tanzania ina ushahidi wa hilo. (CCM ni dini nyingine tofauti kabisa)
 
Hapa mnajadili kitu ambacho sicho. Naomba niwaweke wazi
1. Nilijiunga na NCCR-Mageuzi mwaka 1995
2. Mwaka 2007 niliajiriwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
3. Hiyo 2008 (mwaka ambao hii thread ilianzishwa hapa) nilijiuzuru uongozi katika chama kwa sababu ya huo utumishi wa umma, na mchagizo wa safari ndefu iliyokuwa mbele yangu.
4. Tangia wakati huo siko nchini (ila mara kwa mara nakuja likizo)
5.Kadi yangu ya uanachama wa NCCR-Mageuzi ingali hai. Naendelea kushirikiana na katibu mkuu katika masuala ya falsafa na itikadi ya chama.
6. Uanachama wangu katika chama hiki si wa kufuata mdundiko, bali misimamo ya kiitikadi.
mkuu kahangwa,
samahani kama nilikuelewa vibaya, samahani pia kwa JF. Na heading nimeedit; iwe kahangwa na NCCR
 
Hapa mnajadili kitu ambacho sicho. Naomba niwaweke wazi
1. Nilijiunga na NCCR-Mageuzi mwaka 1995
2. Mwaka 2007 niliajiriwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
3. Hiyo 2008 (mwaka ambao hii thread ilianzishwa hapa) nilijiuzuru uongozi katika chama kwa sababu ya huo utumishi wa umma, na mchagizo wa safari ndefu iliyokuwa mbele yangu.
4. Tangia wakati huo siko nchini (ila mara kwa mara nakuja likizo)
5.Kadi yangu ya uanachama wa NCCR-Mageuzi ingali hai. Naendelea kushirikiana na katibu mkuu katika masuala ya falsafa na itikadi ya chama.
6. Uanachama wangu katika chama hiki si wa kufuata mdundiko, bali misimamo ya kiitikadi.

Samahani nisaidie kwenye namba mbili hapo juu.
Nijuavyo mwanachama mwenzio na kiongozi katika NCCR bwana Sengondo Mvungi ni mwajiriwa pia wa Chuo Kikuu cha Dsm,
Unamshauri nini juu ya utumishi huo?
 
Dr. Adrian Sengondo Mvungi, kwa sasa ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (sio cha serikali). Pili, katika nafasi za uongozi wa kisiasa zinazozuiliwa kisheria kwa watumishi wa umma, Dr.Mvungi hajawahi kushika hata moja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom