Asante MMKJJ, kwa mujibu wa mtoaji habari wangu, aliyerudisha fedha za Kagoda sio Manji, mtoa habari huyo aliidefendi Kagoda kuwa kama ni fedha fedha za Kagoda zilitumika kufanikisha uchaguzi wa CCM, mtoa habari huyo akaniuliza sasa hawa Kagoda walipata wapi hiyo bilioni 40 iliyorudishwa!.Pole sana pasco. Tulishayasema haya humu. Aliyerudisha fedha ni manji kwa niaba ya kina ra. Na ndiye pekee aliyefanya hivyo kwa hiari. Hivi watu hamjajiuliza kwa nini fedha zilizorejeshwa zimepelekwa kwenye kilimo? Si inaitwa kagoda agriculture?
Jamaa he is indeed a king maker, ukiona wabunge wanavyomyenyekea hapa bungeni Dodoma utafikiri ni kimungu fulani. Niko nae hoteli moja, jamaa hupenda kukaa nje open air, basi si foloni hizo, mabalozi wa EU wako hapa Dodoma nao pia wamepiga magoti to show respectKagoda alias Rostam Aziz ni sterling hata movie ikiisha yeye bado atakuwa kasimama. Pale Ikulu tuna njemba lakini mwenye madaraka zaidi ni Kagoda 'aka' RA huyu ataendelea kula kuku zake bila kuguswa na yeyote yule.
Pole usiingie uchungu, mwenye kisu kikali ndiye anakula nyama.Sasa, mustakabali wa Taifa hili uko wapi jamani Wazalendo? inatia uchungu sana, inauma!
Usikute mteuzi mwenyewe ndiyo huyo huyo king maker, JK kazi kutangaza tuu.Hivi ile kamati ya kuchunguza EPA tiyari imemaliza kazi?
kwani watuhumiwa ndo wameibukia kwenye tenda za matrekta.
Sina imani na Kilimo Kwanza tokea yule mtuhumiwa wa EPA
kuteuliwa na mkulu kwenda TIB.
Tangu lini mwizi akirudisha alichoiba anakuwa ni msafi?
Lazima tutafsiri wezi, mwizi ni nani, na sifa zake ni zipi. Mwenye mamlaka kisheria kutangaza nani ni mwizi nani si mwizi kwa mujibu wa katiba ni mahakama pekee, kinyume cha hapo zinabaki kuwa ni tuhuma tuu.Swali zuri
Sasa macho yangu yamefunguka kwani nilikuwa najiuliza Rai walikuwa wanaikandia kauri ya kilimo kwanza na kusema inatokea South Africa na Muasisi wake ni Nelson Mandela Rais msitafu wa SA, kumbe wanajaribu kuamisha concentration kutoka kwa kagoda Ltd na kuipeleka SA.
Hapa kama hatuko macho mapesa yaliyorudishwa yote yanarudi kwa manji kwa kauri mbiu ya kilimo kwanza kwani kagoda inajishugulisha na kilimo hata wakipewa tutaambiwa tenda ilitangazwa wakashinda wakapewa mapesa hayo.
Hivi sisi watanzania tumerogwa au, na kama tumerogwa basi aliyeturoga ameshakufa hata dawa hatutaipata.
Hivi wanaboard niambieni mbona sioni chama kilichoserious katika kutetea haki za watz, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, mtaani kwetu chama cha upinzani kilikuwa CUF tu na walisimamisha mtu ambaye kwangu mimi nasema hafai kulingana na quality za uongozi na ndio kilichotokea wakashindwa vibaya sana.
Sasa tutawezaje kusimamisha ujinga wa CCM bila kuwa na uongozi mbadala wa kutusaidia?
.
Haiwezi kuwaondoa madarakani kama ni dhambi hii hii ndiyo iliyowaweka madarakani, wataitumia kuhakikisha wanatawala milele.
nenda google search engene, andika 'kagoda' click search, ingia darasani mwanangu.Mie bado nina kitendawili kagoda ni mdudu gani?
nipeni data?
Pasco mkuu, maneno yako nimeyasoma kwa uchungu mkuu sana. Sasa naanza kuamini yale yaliyosemwa humu jamvini siku za nyuma kuwa NCHI YETU IMELAANIWA. Iweje haya yote yanafahamika na hakuna linalofanyika?Lazima tutafsiri wezi, mwizi ni nani, na sifa zake ni zipi. Mwenye mamlaka kisheria kutangaza nani ni mwizi nani si mwizi kwa mujibu wa katiba ni mahakama pekee, kinyume cha hapo zinabaki kuwa ni tuhuma tuu.
Kagoda kachota bilioni 40, hakutumia hati bandia, hakufoji chochote na aliyepitisha dondoo la Kagoda na kuidhinisha malipo ni Mama Meghji baada ya kuridhika ni fedha za UWT kufanyia kazi nyeti. Pesa zikatoka wameiba vipi?.
Hiyo kazi nyeti ni pamoja na kuingiza kontena 4 40ft za scalf, fulana na kofia toka Chini, TRA ilizizuia bandarini mpaka zilipiwe kodi, oda ikatoka juu zikapita. Hivi jamani kugawa fulana, kofia na scalf kwa wananchi ili wakichague Chama cha Mapinduzi sio kazi nyeti?.
JK kachaguliwa kwa kazi nzuri iliyofanywa na Kagoda, sasa kaiba wapi?.
Haya baada ya hiyo kazi nzuri, paper work imefanyika vizuri kuthibitisha fedha zimerudishwa, sasa Kagoda hadaiwi, tatizo liko wapi?.
Ndio maana nimesema Kagoda is as clean as CCM itself, hawa wanaotaka kukichafua chama kwa kisingizio cha kupiga vita ufisadi, ndio watasafishwa ili kusafisha njia kwa 2015 atakaporejea mwana mfalme.