Kagera: Tunamuahidi Ndaisaba George ushindi wa kishindo ifikapo mwaka 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
"Tunampongeza Mhe. Ndaisaba George Ruhoro kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kuwakilisha Jimbo letu la Ngara. Tunamuahidi ushindi wa kishindo ifikapo mwaka 2025" - Tamko la Wazee Mkoa wa Kagera, Wilaya ya Ngara.

"Tunatamka kwa pamoja kwamba tuna uwezo wa kumchagua mwaka 2025. Lakini tunasema na wengine waje. Ubunge na Udiwani ulianza rasmi mwaka 1965 Lakini mpaka sasa tulikuwa hatujapata Mbunge bora kama Ndaisaba George Ruhoro" - Tamko la Wazee wa Jimbo la Ngara

"Mwenyezi MUNGU ambariki sana Mbunge Ndaisaba George Ruhoro, ni Kiongozi shupavu. Wengine baada ya kuwachagua wamerudi Dar es Salaam hata sura zao hatuzioni" - Tamko la Wazee wa Jimbo la Ngara

"Ile Shule ilikuwa ni gofu, alipoingia Mbunge Mhe. Ndaisaba George Ruhoro ndani akapiga na picha baada ya pale ile Shule ilibadirika, mpaka sasa ukifika pale unaweza kudhani ile ni Shule ya Sekondari kumbe ni Shule ya Msingi, imekuwa nzuri sana" - Tamko la Wazee wa Jimbo la Ngara

"Wakati wa uchaguzi 2020 tulichukua kilio chetu cha Maji. Ndaisaba George Ruhoro, baada ya mwezi mmoja tulikuwa tumeshapata Maji. Wakafanya hujumu Genereta likaibiwa tukafa mawazo ya kupata Maji lakini Ndaisaba akafanya juu chini na kuleta Genereta" - Tamko la Wazee wa Jimbo la Ngara

"Nashindwa kuelewa, Ndaisaba George Ruhoro kichwa chake kipo vipi? Naomba Wazee wenzangu katika uchaguzi mkuu mwaka 2025 tumpe Ndaisaba George Ruhoro" - Mtoto wa Chifu, Kanazi, Wilaya ya Ngara.
 

Attachments

  • img-20210409-wa0019-1024x678.jpg
    img-20210409-wa0019-1024x678.jpg
    118.7 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.13.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.13.jpeg
    25.2 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.12(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.12(2).jpeg
    12.9 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.12(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.12(1).jpeg
    22.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.12.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.12.jpeg
    12.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.11(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.11(1).jpeg
    12.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.11.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-10 at 13.45.11.jpeg
    30.8 KB · Views: 4

Similar Discussions

Back
Top Bottom