Kagera: Ratiba ya kuaga miili ya waliofariki ajali ya ndege ya Precision Air, Waziri Mkuu anazungumza, leo 07-11-2022

Hapo sasa !!

Mimi huwa nawaza hivyo hivyo!! Hii dunia usiipapatikie saaana mtu ukajiona kama vile umefika !! Hapa ni mapito tu tena hakuna muda maalum tutaondoka tu , haijalishi wewe ni nani na unamiliki vitu gani!! One way ticket inatuhusu sote. !! Tusinyanyase na tusidhalilishe wengine ! Hapa sio Home. !!
Kwa kweli

Maandiko matakatifu yanasema Mungu anaujua mwisho wetu kabla hata hatujazaliwa. Hivyo hatuna budi kutenda mema kadri tuwezavyo na tusiache kufanya Toba

Mungu atusaidie tuwe na mwisho mwema hapa Duniani.
 
So sad 😢

Kuna wakati huoni faida ya maisha, tunahangaika na maisha ili iweje wakati pumzi ikitolewa hapo unabaki mpweke kaburini 🙆😢😢😢
Mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Kwa maana ingine, Mwili ni vazi tu; akivua vazi Hilo la mwili anaendelea kuishi ktk VAZI la kiroho.

Got it?
 
Mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI.

Kwa maana ingine, Mwili ni vazi tu; akivua vazi Hilo la mwili anaendelea kuishi ktk VAZI la kiroho.

Got it?
Kwahiyo wale wapendwa wetu tuliokuwa tunapiga nao vyombo na wakatutoka wanaweza kutuJoin kumwagilia Moyo?

Jambo hili linafikirisha sana Kwa kweli 😢
 
Kwahiyo wale wapendwa wetu tuliokuwa tunapiga nao vyombo na wakatutoka wanaweza kutuJoin kumwagilia Moyo?

Jambo hili linafikirisha sana Kwa kweli 😢
Acha mambo hayo.

Kuzimu Kuna mateso yasiyoelezeka ROHO zinateseka balaa,

Waliotangulia hutamani warudi kuwambia muache mambo hayo msijeenda wao walipo bt hawawezi maana SHIMO la kuzimu ni Refu sana, huwezi toka.

Wasikie wahubiri wasemacho maana ndo wanawakilisha ujumbe wa Mungu.
 
Mbona hawa ndugu zetu huku barabarani na hizi ajali za mabus wanakufa mara kwa mara idadi ya kutisha kuanzia 20 - 30 mara kwa mara...
 
Leo ni hafla yenye majonzi Kwa watanzania wote tukio la Jana kupoteza maisha watu 19 kwenye ndege ya precision air.

Baadhi waliokolewa na wavuvi pamoja nawananchi wenye maisha ya umasikin wa kutupwa pamoja na hii nchi kuwa namandege lundo yasiokuwa na faida Mara nyingi huwa yanaonyeshwa kwenye maadhimisho ya uhuru.

Mandege mengi ya kijeshi ya rescue and savior Lakin kumbe hayana maajabu, aibu Kwa jeshi letu hili lakisiasa.

Sasa ajabu Leo watakaokaa kwenye kivuli kwenye kuaga hii miili ni wanajeshi na viongozi wa kisiasa huku masikini na wavuvi wakiwa kwenye mavumbi na jua Kali.

1667812415584.jpg
 
SIo kwa Bongo hii. Yani hapo wapaka piko na wavaa mawigi kama viota ndio utawaona wamejazana tena ndio watakuwa woangeaji wakuu kama vile wao ndio walikuwa wanaokoa.

Hao wavuvi washasahaulika na usishangae kesho wakaitwa wavuvi haramu na kuchomewa moto nyavu zao.

Hapo ni subiri uje kusikia budget iliyotumika kuaga miili kama hujaambiwa ni Bil 20.
Viongozi wamejawa na roho za wizi na tamaa kiasi cha kuona fursa kila sehemu.
 
Hivi ndivyo mambo yalivyo leo Novemba 7, 2022 kuhusu utaratibu wa kuaga miili 19 ya watu waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea jana Noveba 6, 2022 Mkoani Kagera

Hivi mbona Ccm mna tuletea siasa kwenye mambo ya msingi?
Sisi tuliona walio jitoa kuokoa ni wananchi. Hapa hata kutambua uwepo wao hamna. Ila viongozi wa Ccm wamo. Hii laanaita wamaliza kenge nyie.
 
Back
Top Bottom