Kagame cup mshindi wa 3: Yanga waingia mitini

Wakati wa kuwachukulia poa watu umeisha, Yanga wame break the rule, uwezi kuendelea bila ya kubreak the rule. Hata Nyerere alibreak the rule ili kudai uhuru na ndio maana alichukuliwa kama muarifu na watawala wa kikoloni. Ni bora watu waseme yaani tunaenda uwanjani uwanja unajaa mapato ni zaidi ya milioni 100 kwa mechi halafu timu inaambulia milioni nane tena inaambiwa ni privelege.

Pongezi Yanga kwa kuchukua hatua, manake maamuzi magumu kuchukuliwa bongo ni adimu. CECAFA na TFF wajifunze kuwa mpira uwanufaishe zaidi wachezaji kuliko viongozi wa vyama. Mbona Yanga walishawahi kuchukua ubingwa na zawadi mpaka leo wanadai USD 30,000 karibu miaka 10.

Lion share siku zoke inaenda kwa Lion, itakuwaje watu wagawane sawa wakati kuna ambao wanachangia zaidi? Mpira ni biashara sasa hivi, kama charity kwanini watu wasiingie bure uwanjani na tulilalamika viingilio ni vikubwa lakini si TFF wala CECAFA waliochukua hatua stahili na bado kuna sponsors wa mashindano.

Bravo Yanga kwa kufanya maamuzi magumu, lazima kuna watu wa kawaida sana watawapinga lakini eventually watawaelewa nini mnamaanisha. Heshima kama kupotea haiwezi kupotea, ni sawa sawa na wabongo wanavyotawaliwa kwa nyimbo ya amani na utulivu ili wasiwachague wapinzani. Ni swala la muda tu, msg sent kwa Musonyi na wenzake wanaonufaika kwa expenses za vilabu.
 
Ukifuatilia sakata zima la Yanga kuingia mitini ndio utahakiki kuwa TZ soka kuendelea ni mbaka simba na yanga ZIFE!!, maoni ya wengi ni damn subjective bila kujali hoja za msingi!!

TFF wamewadekeza vibaya sana SIMBA na YANGA na hicho kiburi cha Yanga ni matokeo ya mfume dume wa U-simba na U-yanga ambao pamoja na nusru karne kuwa nao si FAT/TFF wamejifunza au sisi wadau wengine tumejifunza kuwa hatuwezi kuendelea kwa soka la simba na yanga kamweee!!

Kama ningeweza basi hizi timu mbili i wish ziwe vyama vya siasa ili nivifutiliee mbaliii...and i play to lord ZIFEEE!!, coz hamna cha maana wanachofanya zaidi ya politiks tu za majuwani wakahamishia uwanjanii!!

Then for those who were looking at Maxio as a culprit kwa performance this is the roght time to sue them!!

Kwa mtindo huu ndugu zangu, mafanikio ya soka TZ ni ndoto za Alinacha!!, there is a very long way to go!!
 
Jamani haya yaliyotokea kwa kweli matunda ya uzembe na tabia ya kuzidekeza Simba na Yanga ambayo tangu enzi za FAT mpaka sasa TFF haka katabia kanaendelea.

TFF wanapaswa kulaumiwa kwa hili lililotokea. Mashindano ya CECAFA yanakanuni zake kuwa timu shiriki hazipati malipo yoyote zaidi ya zawadi kwa mshindi wa 1-3, lakini kwa kuwa TFF wana kale katabia ka kusubiri kuzikutanisha Simba na Yanga ili wavune mapesa walidiriki mpaka kufanya vikao kujadili suala la mgao hata kabla ya mchezo. Na hapa Nicolas Musonye katibu mkuu wa CECAFA nae akaingizwa mkenge na TFF kukubali ujinga wa kuwasikiliza Simba na Yanga kuhusu mapato.

Hivi jiulize swali, kwani haya mashindano kama yangefanyika nje ya Tanzania kama ni Kenya, Uganda au Rwanda Simba na Yanga wangepata wapi ujasiri wa kudai mgao kabla ya mechi?

Lakini kwa kuwa TFF wanajulikana kuwa mavuno yao ya pesa ni kwa Simba na Yanga, that's why wakakiuka mpaka kanuni za mashindano ili kuzishawishi Simba na Yanga wakubali kucheza kwa makubaliano ya kuwapa 50ml kila timu...Ni kichekesho sana kama package ya zawadi ya mashindano ni karibu 64ml, halafu timu mbili tu zichukue pesa zaidi ya zawadi zilizotolewa. So mtoto umleavyo ndivyo akuavyo atakutia aibu mbele ya wageni na ndicho kilichotokea kwa TFF na Yanga ingawa Magori anadai aibu ni Yanga eti klabu kubwa nchini....

Nadhani next time CECAFA wataepuka kuburuzwa na vyama wenyeji katika kuandaa haya mashindano. Nina imani CECAFA waliburuzwa na TFF katika mambo mengi sana ikiwemo kulazimisha mechi zinazohusisha Simba na Yanga zichezwe kwenye uwanja mpya wakati serikali ilishaweka wazi kuwa uwanja haujakamilika na kukabidhiwa rasmi kwa serikali. Na Musonye nae anazungumza tu kwenye vyombo vya habari kuomba serikali iruhusu uwanja mpya eti itayapa mashindano hadhi.

Yanga nawapongeza kwa hili...Nikiwa mnazi mkubwa wa Simba sizungumzii ushabiki bali ukweli na halisi ya watendaji katika TFF kuwa ni wababaishaji wakubwa na wamejaa ulafi na tamaa ya pesa na haya ndio malipo waliyostahili nahata mashindano yenyewe ya KAGAME yanaoneka yanaendeshwa kihuni tu kutokana na personal interest za watu fulani. Uliona wapi timu inapochelewa kutokea uwanjani inasubiriwa dakika 45??

Tenga na wenzake hapa ameprove failure ya aina yake....Bravo Yanga!!!!
 
Mimi siamini kuwa Yanga wameikimbia simba.Wacheaji walikuwa na morali 100% kumvaa mnyama.Tatizo ni maamuzi mabovu ya viongozi wa Yanga.

Yanga ndio waliotangulia kutoa wazo la kupewa mgao wa mechi na wakawashirikisha wenzao wa Simba nao wakakubali.

Makubaliano ilikuwa kuwa timu zipewe mgao wa milioni 50 jumapili asubuhi kwenye pre-match meeting kitu ambacho hakikutekelezwa na CECAFA.Makubaliano ya awali kati ya simba na yanga ni kuwa wasipopewa fedha wagomee mechi.Wenzao Simba wakakiuka makubaliano batili waliyokuwa wamekubaliana na yanga.

Wanachodai akina madega ni kuwa wao wameheshimu makubaliano waliyofikia kabla ya mechi ila CECAFA wameshindwa kuheshimu makubaliano na Simba wamewasaliti wenzao jangwani.

Hiyo ndiyo habari ya yanga.Hatahivyo ni msimamo wa kipuuzi kwa kuwa yanga hawana shida ya milioni hamsini.Hata wangepewa kabla ya mechi zingewasaidia nini kabla ya kupambana na simba?.Madega na wenzake waliamua kuingiza U-YANGA NA U-SIMBA kwenye michuano ya CECAFA kwa lengo la kuikomoa CECAFA na simba.Kiini cha kugomea mechi ilikuwa kuikosesha CECAFA mapato stahili ya mechi ya mshindi wa tatu.Ndiyo maana habari za yanga kutokucheza na simba zilisambazwa kama moto wa nyika na viongozi wa yanga kila kona kusudi wapenzi wao wasiende uwanjani.

Hatuwezi kuwa na viongozi wa aina ya Madega tukafika mbali.

TUSUBIRI TUONE MIGOGOROITAKAYOFUMUKA YANGA.NASIKITIKA ENZI YA YANGA KUNG'ARA IMEFIKA UKINGONI.Madega anawajibika kuizika Yanga.

Mwana Yanga DAMU NA NYAMA!
 
kama hilo kombe yanga walishalichukua enzi zile lina umaarufu...
achana na sasa hivi lipolipo tu kama kinesi.
na waliweza kulichukua nje ya ardhi ya tanzania na kuleta heshima kwa taifa, mpaka ikafika kipindi watoto wa uganda wakawa wakiulizwa "unataka kucheza mpira kama nani?"
wanajibu kama lunyamila.

so sioni cha ajabu dar es salaam young african kujitoa kutokana na uharo wa TFF.

Mrishiriki ili iweje?, acha ushabiki wa kipuuzi wakati wametuabisha Taifa zima, na kwa taarifa yako jana kama Yanga wangeingiza timu ilikuwa mwisho wa Madega na wezake (baada yakuwafungia ivo na sajigwa ulitegemea wangemfungia nani safari hii kaseja?) maana kibano ambasho Yanga angekipata, mme wenu manji sijui mnge mweleza nini kama ni pesa kawapa ya usajiri na mkaleta Makocha lukuki kutoka ulaya + mchezaji kutoka ulaya lkn bado humna jeuri ya kuifunga Simba...simba wana weza soka lote(yaani la ndani ya dimba na nje ya dimba) hasa kukiwa na friends of simba pembeni sahau kuifunga simba, tutafungwa na Manyema lkn siyo Yanga....nakushauri mjipange lbd 2011 mtaanza kushinda vinginevyo nikibano na sare...
 
Hapa wakuu ni kwamba CECAFA pamoja na TTF walitaka kujineemesha kimapato kwa kuzitumia mnyama na watoto wa jangwani sasa tukawashtukia tukawaambia watupe chetu mapema mil.50 maana wao wangepata zaidi kama mil.300 wakawa wanakataa.Mnyama na njaa zake akatuzunguka mlango wa nyuma akapeleka timu uwanjani wkt msimamo wetu ulikuwa mmoja.
 
yanga Wanashiriki Mashindano Makubwa Msimu Huu, Yaani Wanatazamia Kupambana Na Timu Kama Al Ahly, Enyimba Musica Ambayo Last Season Ilwapiga Simba Jumla 7-1.
So Hatuwezi Kukimbizana Na Simba Ambao Wanawasubiri Villa Squad, Jkt Ruvu, Afc, Polisi Moro Na Nyingine Za Hadhi Yenu Katika Ligi Yenu Hiyo Ya Tff Ambayo Rufaa Zinakubaliwa.

unaumwa Njaa...
 
Katika jamii yoyote unapokuwa na wanachama wasio na vision na uongozi ambao ufanisi wao unapimwa kwa vigezo holelaholela ndiyo matokeo yake yanakuwa kama ya Yanga kukimbia mechi. Ni matunda ya utamaduni wa hizi klabu zetu ambapo Kiongozi anapimwa ameongoza vizuri kwa kutengeneza mazingira ya kutofungwa na Simba au Yanga badala ya kuangilia amekuza vipi kiwango cha mpira. Klabu inapopata nafasi ya kucheza kwenye competitive environment ndiyo unajipima ubora wake ukikwepa mazingira hayo kwa kufikiria unamkumoa mtu/TFF au CECAFA ni ufinyu wa mawazo. Hatua yoyote itakayoichukuliwa itakuwa na athari kwa maendeleo ya mpira na dignity (kama wenye klabu yao wanajali kuwa nayo) katika Yanga. Kwa hiyo viongozi wa aina hii ndiyo haohao wanategemewa wakuze wachezaji kwenye timu zao ili wawe wa timu ya taifa sijui tutajenga vipi soka? Kwao wao mpira ni secondary hoja ya msingi ni ubabaishaji na wachezaji wanajengwa kwa mazingira hayo. Tunategemea tuone hoja zisizo na substance ambazo manazi wa YANGA na wale wote wasiopenda maendeleo ya mpira wataendelea kuzitoa.
 
Jamani Hali Ilkuwa Ngumu.sangoma Kapiga Ramli Kaona Simba 7 Yanga 0.sasa Ili Kumkimbia Ilikuwa Lazima Itafutwe Sababu Mbadala.
Kama Ingekuwa Ni Mambo Ya Fedha Mbona Simba Alikubali Kucheza?bila Shaka Alikuwa Na Uhakika Wa Kumshinda Yanga Kwa Hiyo Alikuwa Akijiamni 100%.
Upande Wapili Woga Ulikuwa Umeshatanda Tangu Mashindano Yaanze.mambo Ya Kinajimu Yaligoma Na Hapo Ndipo Sababu Za Tff Na Cecafa Zikawa Scape Goat.poleni Watani..kama Mtakuwa Hivi Katika Enzi Hizi Mtajikuta Mnacheza Soccer La Maharage.
 
Hapa wakuu ni kwamba CECAFA pamoja na TTF walitaka kujineemesha kimapato kwa kuzitumia mnyama na watoto wa jangwani sasa tukawashtukia tukawaambia watupe chetu mapema mil.50 maana wao wangepata zaidi kama mil.300 wakawa wanakataa.Mnyama na njaa zake akatuzunguka mlango wa nyuma akapeleka timu uwanjani wkt msimamo wetu ulikuwa mmoja.

Mfa maji haishi kutapatapa. Kwa mantiki ipi CECAFA ikubali kutoa pesa zaidi ya zile anazozawadiwa mshindi labda kama inaongozwa viongozi wa aina ya Yanga. Kwa madai ya kiasi hicho Yanga ilikusudia kukwepa kucheza kwa kudai kisichowezekana
 
madega pamoja na kuwa amesoma ameonyesha kiasi gani ni mswahili kama mganga aliwaambia waingie kwa kuruka ukuta na ukuta wenyewe ndio ule haurukwi
 
Yaani Manji alishindwa kuwapa hizo pesa atimize malengo yake?

Ngoja nitafute makala moja hivi. Aibu kubwa ya KARNE


Mimi naona Yanga imefanya jambo zuri sana kuwapa somo CECAFA na TFF kutafuta mbinu zingine za kupatia fedha badala ya kutegemea mapato ya milangoni. Kwanza ilikuwaje watu wasomi kama Magori na Mwakalebela kuamua kupindisha kanuni ili tu wapate pesa za mlangoni. Ama kweli wameingizwa mjini, na mimi sioni kwamba ni fedhaeha kwa Yanga bali kwa TFF. Yanga ina timu nzuri isingeweza kukimbia kwa kuogopa matokeo ya uwanjani, ni fitina mbele kwa mbele.

Ndiyo bila hivi viongozi wetu hawatajifunza kutokuwa tegemezi.
 
Yanga Wamechemsha,nadhani Wanaogopa Kufungwa Mara Nyingine Kwani Mara Hii Mdosi Alwaambia Wakifungwa Anawafukuza Wote. Ndo Tatizo La Kuikabidhi Timu Magabacholi.pia Mzungu Yaani Kocha Wao Aliwaambia Wapeleke Timu Wakamdanganya Kwamba Hapa Bongo Timu Ya Yanga Ikifungwa Na Simba Au Simba Kufngwa Na Yanga Kocha Uwa Anapoteza Kazi Mzungu Wa Watu Akaweka Mkia Matakoni
 
Duh naona Michuzi anatoa nyepesi kwamba Yanga tumeingia mitini.... Nimetokea sipo mjini na kila ninayempigia naye ni amezima simu!! Asalale, hii ni kuwapa wanyama cha kuongea manake si utani hii ndio inaitwa aibu ya karne, heri kulipa faini kuliko aibishwa na mnyama!!

Teh Teh Teh...

Mulikula ya mbuzi, sasa mumeota mapembe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom