Kafulila, Hashim Rungwe waanzisha chama cha Siasa

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Wanaharakati wa kisiasa ambao wametoswa katika vyama vyao wako katika hatua za mwisho kuanzisha chama cha kisiasa kitakachoitwa Chama cha Ukombozi wa Umma kwa lengo la kuendeleza harakati hizo.

Wanaharakati wanaotajwa kuanzisha chama hicho ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila ambaye amefukuzwa uanachama NCCR- Mageuzi, Hashim Rungwe ambaye aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR Mageuzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na Hamad Tao aliyetimuliwa TLP.

Chama hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti wa muda Mwalesi Mayunga kinatarajia kupata usajili wa muda kesho Jumanne Julai 3,2012

Akizungumza na Sema Usikike Tao alithibitisha uwepo wa chama hicho lakini hakutaka kuingia kwa undani.

Source: Gazeti la Sema Usikike la leo Julai 2,2012

My Take:
Huu utitiri wa vyama vya siasa utatufikisha wapi? Kafulila na Rungwe wanaweza kupima ubavu wa ushindani uliopo? Nahisi yunaongeza utitiri wa vyama vya mfukoni kama alivyosema Mh.Tendwa
 
Hee!Chama kingine hicho kitaishia kusambaratika kwani wahusika wamethibitisha tayari kuwa ni wapenda madaraka!Fikiria Kafulila kwa mfano,kila anapo kwenda anaishia kufukuzwa!!!
 
Vije hata mia moja lakini watanzania wameshaamua chama chao ni CDM

samahani.... si watanzania wote! ingekuwa watanzania wote CDM wangelikuwa madarakani sasa hivi na nchi ingelishakuwa vitani kwa sera zao za udini.. ukabila na ukanda
 
samahani.... si watanzania wote! ingekuwa watanzania wote CDM wangelikuwa madarakani sasa hivi na nchi ingelishakuwa vitani kwa sera zao za udini.. ukabila na ukanda
Kama sio wizi wa kura wa CCM unadhani CDM isingelikuwa madarakani hivi sasa??? CCM wanaiba kila kitu fedha kura, dhahabu zetu, uranium, EPA, RADAR, RICHIMOND, sasa Uswiz imewaumbua USD$ 300= billion mmezificha hoko!!! Mkisemwa mmnataka kuuwa watu Dr ,Mwakyembe, Dr Ulimboka, sasa mkuu anataka kufukuza madaktari woote nchi nzima eti wasidai haki zao wagonjwa waendelee kufa!!!! Sera za CCM zimefika ukingoni si mjihudhulu kama alivyosema Tundu Lisu juzi kwenye bunge????

Kama sio wizi wa kura wa CCM unadhani CDM isingelikuwa madarakani hivi sasa???
Leteni ushahidi kwamba mliibiwa kura zenu! ... kujaa watu kwenye mikutano sio kwamba wote ni wapiga kura.. wengine wauza maji.. pipi.. wengine wanakuja kushangaa pumba zinazoongolewa mkutanoni...

Lisu ni dhaifu na mropokaji.. tushalizoea vuvuzela lile
 
hii ni mbinu mara nyingi inatumiwa na system kupunguza kura kwa chama pinzani kilicho hatarishi, baada ya uchaguzi huwa havina mashiko tena, na viongozi wake huhamia kwenye shughuli zingine (Fami Dovutwa na wenzake 2010)
 
samahani.... si watanzania wote! ingekuwa watanzania wote CDM wangelikuwa madarakani sasa hivi na nchi ingelishakuwa vitani kwa sera zao za udini.. ukabila na ukanda

you must be a woman with no exposure...la sivyo we ni anti...udini na ukabila unaujua wewe! mimi nakusikitikia watu mnao olewa kwa maneno rahisi kwa miaka 50 ya mateso bado mnakuwa migando tu
 
Hizo zinaitwa Politician Projects!! acha wazianzishe hata mia wataungana wenyewe, subiri mambo yatakapobadilika kupitia katiba mpya.
 
you must be a woman with no exposure...la sivyo we ni anti...udini na ukabila unaujua wewe! mimi nakusikitikia watu mnao olewa kwa maneno rahisi kwa miaka 50 ya mateso bado mnakuwa migando tu

Wacha assumptions idiot ...
 
Vije hata mia moja lakini watanzania wameshaamua chama chao ni CDM

Usizungumze kwa niaba ya Watanzania wote, kama mmeamua kuchagua CDM ni wewe na Wakaskazini wenzako sio Watanzania wote wanakitaka..
 
samahani.... si watanzania wote! ingekuwa watanzania wote CDM wangelikuwa madarakani sasa hivi na nchi ingelishakuwa vitani kwa sera zao za udini.. ukabila na ukanda

Mbona watanzania walishaiweka cdm madarakani tiss na nec wakachomoa!? Na hizo sera mbona zinaitafuna nchi wakati cdm hawapo madarakani? Iweje sera kama ni za cdm zitekelezwe ndani ya uongozi wa ccm? Kama ni watu wa cdm ndio wenye sera hizo mbona hawakamatwi na tumeona makanisa yakichomwa moto?
Tafakari....!
 
niliipenda kauli ya Tendwa kuwa kuna mpango wa kutunga sheria ya kuvipukutisha vyama visivyo na tija kwa taifa au ushindani..chama hakina mbunge lakini bado kinakula ruzuku tuuu ..
 
Utitiri wa vyama vya siasa vimezidi sasa Tanzania. Vyama vimekua kama bendi na wanasiasa wamekua kama wanamziki, ukitoswa unahama bendi au kuanzisha bendi yako.
 
Back
Top Bottom