Si kweli. Mbona mimi nashindwa kuvuna kila ninapojaribu? Kote wenye shamba wamefunga!
Hoja ya Kafulila haina mashiko
Pesa imetoka BOT kwa kufuata taratibu na wizara ya fedha inajua na ndio ime confirm malipo yafanyike.
Maswala hayo yapo mahakamani na jaji ametoa amri.
Umeandika nini sasa?? Hebu soma alafu uone kama utaelewa. Ifute uandike upya.
Kwahiyo wewe una-okey taifa liendelee kuibiwa kwasababu ya mahaba yako kwa CCM?Ningekuona una mawazo safi kama na wewe ungeunga mkono hoja ya Wenje kuhusu kuundwa kwa kamati maalum ya uchunguzi ya bunge ili hatimaye ukweli ujulikane.Sijui nani alililoga hili taifa?limejaa mazezeta wengi mno mpaka inakera.
Na tabia hiyo ndio inayokwamisha wachache wanaojitoa kupambana na ufisadi. Hakuna nchi imewahi kuendelea kwa kuendekeza mambo haya.Tatizo watanzania wengi ni washabiki wa siasa na c wapenzi wa maendeleo ndio maana hata jambo serious wao huponda tu
Kwa mara nyingine tena serikali sikivu ya Kikwete imefanya kweli kwa kuiba fedha takribani Billion 200 za Tanesco BOT.
Gavana wa BOT amefunguka na kudai kuwa alishinikizwa ili kuzitoa fedha hizo.
CCM inaendelea kutafuna nchi hii, Kikwete mpaka aondoke lazima tutakuwa hohehahe.
Nchi ipi hiyo mkuu?
Bunge halina uwezo wa kufanya uchunguzi wowote wa kitaalam.
Ningeunga mkono kama wangeshauri iteuliwe Auditing firm yenye uzoefu ikaangalia kama kuna makosa.
Vinginevyo hao wanasiasa ni kutafuta sifa tu hamna lolote wala hawana nia njema na nchi!!
Bunge halina uwezo wa kufanya uchunguzi wowote wa kitaalam
Kwani waliosababisha mpaka Waziri Mkuu wa wakati ule Bw. Lowassa akajiuzulu ni nani kama siyo kamati ya Bunge?Halafu pia hapa nashindwa kuelewa kama kweli unakerwa na huu ufisadi au unauchukulia poa tu?Utasemaje kwamba Kafulila anajitafutia umaarufu kwenye jambo linalogusa maslahi ya Nchi na Wananchi kwa jumla?Ndiyo maana nikasema Watanzania tumelogwa maana tupo tupo tu kama mandondocha vile.Si ajabu Mafisadi ndani ya Chama tawala wametudhalau nao na ndiyo maana wanatufanyia mambo kama vile sisi Wananchi hatuna akili timamu,Na kwa kauli kama hizi dhidi ya hoja nyeti kama hizi kweli tunaonekana vichwani tuna kasoro,Tuna aina flani ya mtindio wa ubongo (mentally retarded).