Kafulila afichua wizi wa Bilioni 200 za Tanesco BOT

Wimbo wao ushazoeleka! Ila Watanzania wenyewe ndio wanabariki uozo huu kwa kupewa kanga na pakiti ya chumvi!
Tuchukue hatua mimi na wewe kununua dawa kwajili ya kuangamiza ukoo wa panya.
 
Si kweli. Mbona mimi nashindwa kuvuna kila ninapojaribu? Kote wenye shamba wamefunga!

ulichelewa mkuu walio wahi wanaisha maisha ya kifahari.....gape la mwenye nacho na asie nacho ina zidi kuongezeka kwa kasi
 
Hoja ya Kafulila haina mashiko

Pesa imetoka BOT kwa kufuata taratibu na wizara ya fedha inajua na ndio ime confirm malipo yafanyike.

Maswala hayo yapo mahakamani na jaji ametoa amri.

Unajua kazi na utendaji kazi wa
~HAZINA
~BOT
~WIZARA YA FEDHA

Then to STK,SU, SM!

Ukinijibu nitakurudia, sasa sio wakati wa siasa ni ukweli tuu!!!
 
Kwahiyo wewe una-okey taifa liendelee kuibiwa kwasababu ya mahaba yako kwa CCM?Ningekuona una mawazo safi kama na wewe ungeunga mkono hoja ya Wenje kuhusu kuundwa kwa kamati maalum ya uchunguzi ya bunge ili hatimaye ukweli ujulikane.Sijui nani alililoga hili taifa?limejaa mazezeta wengi mno mpaka inakera.

Bunge halina uwezo wa kufanya uchunguzi wowote wa kitaalam.

Ningeunga mkono kama wangeshauri iteuliwe Auditing firm yenye uzoefu ikaangalia kama kuna makosa.

Vinginevyo hao wanasiasa ni kutafuta sifa tu hamna lolote wala hawana nia njema na nchi!!
 
Latina maisha jua ukificha mahovu jua ipo siku yatajulikana tu hata kama yatachukuwa muda ila jua yatajulikana
 
Hizo ni zilizoibwa sasa hivi..!!
Vipi miaka hiyo kipindi hamna anayeweza kutoboa siri kama hivi zilichotwa ngapi??

*Ndo ile nchi yangu*
 
Tatizo watanzania wengi ni washabiki wa siasa na c wapenzi wa maendeleo ndio maana hata jambo serious wao huponda tu
 
Tatizo watanzania wengi ni washabiki wa siasa na c wapenzi wa maendeleo ndio maana hata jambo serious wao huponda tu
Na tabia hiyo ndio inayokwamisha wachache wanaojitoa kupambana na ufisadi. Hakuna nchi imewahi kuendelea kwa kuendekeza mambo haya.
Ila mkuu ona pamoja na wizi huu wa mabilioni, deni la taifa nalo linapaa utafikiri dege la kijeshi. Kwa hiyo hela zinapigwa kotekote ndani na za nje. Ngoja tuje tuone 2016 tutakuwa na hali gani nchi hii.
 
Yaani sijui ni lini ss tutajikwamua ktk mawazo mgando yaani mawazo ya 1980s ambayo inaonekana vijana wengi wamekuwa nayo
 
Kwa mara nyingine tena serikali sikivu ya Kikwete imefanya kweli kwa kuiba fedha takribani Billion 200 za Tanesco BOT.

Gavana wa BOT amefunguka na kudai kuwa alishinikizwa ili kuzitoa fedha hizo.

CCM inaendelea kutafuna nchi hii, Kikwete mpaka aondoke lazima tutakuwa hohehahe.


Hapo ndipo tunapokosea, kila kitu Mh. baba Riz.
Ndio Ninyi mtt akikosea ni mama.
 
Mmh kafulila? Hujui kama huyo dogo ubongo wake umekreki, muda vinapanda muda. Vinashuka.


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Data and facts ni muhimu sana ktk mijadala yenye kuteka hisia za wananchi... Mkuu Mdhalendo funguka zaidi kwa manufaa ya wengi wetu...
 
Bunge halina uwezo wa kufanya uchunguzi wowote wa kitaalam.

Ningeunga mkono kama wangeshauri iteuliwe Auditing firm yenye uzoefu ikaangalia kama kuna makosa.

Vinginevyo hao wanasiasa ni kutafuta sifa tu hamna lolote wala hawana nia njema na nchi!!
Bunge halina uwezo wa kufanya uchunguzi wowote wa kitaalam

Kwani waliosababisha mpaka Waziri Mkuu wa wakati ule Bw. Lowassa akajiuzulu ni nani kama siyo kamati ya Bunge?Halafu pia hapa nashindwa kuelewa kama kweli unakerwa na huu ufisadi au unauchukulia poa tu?Utasemaje kwamba Kafulila anajitafutia umaarufu kwenye jambo linalogusa maslahi ya Nchi na Wananchi kwa jumla?Ndiyo maana nikasema Watanzania tumelogwa maana tupo tupo tu kama mandondocha vile.Si ajabu Mafisadi ndani ya Chama tawala wametudhalau nao na ndiyo maana wanatufanyia mambo kama vile sisi Wananchi hatuna akili timamu,Na kwa kauli kama hizi dhidi ya hoja nyeti kama hizi kweli tunaonekana vichwani tuna kasoro,Tuna aina flani ya mtindio wa ubongo (mentally retarded).
 
Back
Top Bottom