Elections 2010 Kadi mpya za kupigia kura bado zinagawiwa, majina yatokea mara mbili

kasyabone tall

JF-Expert Member
Sep 13, 2009
254
59
Habari nilizo nazo ni kuwa kadi mpya za kupigia kura Tarehe 31-10-2010, bado zinatolewa kwa wapiga kura ambao sio rasmi( ambao hawatambuliwi na NEC). Lakini pia kuna tatizo kubwa sana,watu waliojiandikisha katika kituo kimoja na kufanya marekebisho ya kujiandisha upya sehemu nyingine alizohamia, majina yao yametokea sehemu zote mbili. Licha ya kasoro hizo kutokea, bado kadi mpya zinatolewa na bila shaka ni hayo majina ambayo yanatokea sehemu mbili. Je kwingineko hilo jambo likoje?
Wale waliojiandikisha na wakabadili vituo waangalie majina yao kule walikokuwa wamejiaandikisha awali. Pia wafanye uchunguzi wa kina juu ya kutolewa kadi mpya za kupigia kura kipindi hiki katika maeneo yao, japo zatolewa kwa siri mno.
 
Mnakumbuka lile swali alilouliza BAREGU kuwa kwa nini TUME imetoa idadi tata ya wapiga kura???
Sasa nimepata mantiki ya dukuduku la baregu.

CCM jamani si mkubali kushindwa kihalali??? mbona mnaipeleka nchi shimoni??????
 
Kilugha tunaita hii UPOMPONI,...YAANI INAMAANISHA HALI INAYOZIDI UPUMBAVU!
Utawala wa shetani unaendeshwa kishetani tu!..nimemaliza!
 
Kwa hali ilipofika napendekeza mambo mawili:- 1) Uchaguzi ufutwe na nchi hii isiwe tena JMT badala yake iwe Falme ya Kikwete, JK awe mfalme Kikwete wa I. 2) Jeshi lichukuwe madaraka kuwe na serikali ya mpito, vyama vyote vya siasa vifutwe na rasilimali zoote za vyama zichukuliwe na serikali halafu, iandikwe katiba mpya, viandikishwe vyama vya siasa upya visizidi vitatu.Baada ya miaka miwili ufanyike uchaguzi huru na wa haki. Wote walio na tuhuma za ufisadi wasiruhusiwe kujishughulisha na mambo ya siasa mpaka watakapo kuwa cleared na tuhuma hizo na mahakama.JK TUMECHOKA NA MAMBO YENU YA KIHUNI, TANZANIA SIYO MALI YAKO NA GENGE LA MAFISADI WENZAKO.
 
Back
Top Bottom