Kadhia ya waandishi wa habari Tanzania

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Wasaalamu wana jamvi, hongereni kwa majukumu ya mwisho wa wiki katika kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafikiwa. Tunapojiandaa kukumbuka siku alipotutoka muasisi wa Taifa hili napenda kujadili nanyi juu ya taaluma hii muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote duniani.

Taaluma ya uandishi wa habari ukitumiwa vizuri unaweza kufanya nchi kupiga hatua kubwa hasa katika sekta ya utalii na viwanda. Taaluma hii pia inaweza kuleta uwepo wa amani na utulivu katika nchi yoyote au kinyume chake.
Kwa Tanzania elimu hii ama haijapewa kipaumbele au umuhimu wake umesahaulika kabisa.

Inaonekana wanafunzi wengi wanaenda kusoma degree ya uandishi wa habari kwa sehemu kubwa ni wale ambao walipata marks zisizoridhisha na hata baada ya kuhitimu uwezo wao huendelea kuwa mdogo kwa kiwango kikubwa. Ninasema haya kwasababu waandishi wa habari wa tanzania hawana uwezo ku-reason kitu hasa wanachokipokea kutoka kwa wanasiasa na viongozi wa nchi. Wamekuwa vipofu wa fikra ama kwa makusudi au kwa kukubali kununuliwa.

Hii ni mifano michache nitakayosimamia
1. Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na malalamiko ya uhaba wa madawa muhimu za binadamu na vifaa tiba. Waandhishi wetu hawa wanahoji wananchi na kupata malalamiko ya madaktari halafu kesho yake waziri anawaita kisha anawaambia hakuna uhaba wa madawa na habari hizo zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki kwa nchi, halafu hawa wasomi wetu wanakaa kimya hata bila kumhoji waziri tena kwa kumpa mifano halisi ya aina ya madawa na vifaa vinavyokosekana na Hospitali au maeneo husika ( yaani mwandishi wa habari unaenda kukutana na waziri wa afya halafu huendi hata na data za maana huku unajua huyu anaenda kuzungumzia nini), hii ni aibu.

2. Katika kipindi fulani waziri fulani aliulizwa na muongoza kipindi namna pesa za kuhamia dodoma zitakavyopatikana mwaka huu, majibu ya waziri huyo yalinifanya nijihoji juu ya hii taaluma ya uandishi wa habari hapa tz maana muuliza swali aliridhika na majibu ambayo hata mwanafunzi wa form two asingeyakubali. Nasema hivyo kwasababu kama asingeridhika nayo angetaka majibu ya uhakika zaidi kutoka kwake ila hakufanya hivyo.

3. Wakati wa uchaguzi wa mwaka jana, Mheshimiwa fulani alipoita waandishi wa habari nyumbani kwake katika harakati za kuwania kugombea urais, moja ya swali aliloulizwa na jopo la waandishi wa habari ni hili " mheshimiwa ulipokuwa jeshini ulikuwa na cheo gani?". Hili ndilo swali ambalo jopo la wasomi hao waliona linamfaa mgombea na si mambo ya tuhuma dhidi zake pamoja na kujua namna atakavyotekeza ahadi zake

Najua nanyi pia mna mengi juu ya waandishi wetu hawa wa habari, si kwamba kila wanachokifanya ni kibaya hapana. Najua wanachangamoto nyingi kutoka serikalini na wamiliki wa vyombo vya habari ila wajaribu kuutendea taaluma yao haki.

Kwa kumalizia napenda kuwaambia waandishi wa habari kuwa watanzania wengi wanatamani sana kukutana na viongozi wao wa juu ila wanashindwa, wanapopata nafasi hizo wazitumie kutuulizia maswali ya msingi yenye kuleta majibu ya changamoto zetu.

Pili kuwepo na bodi ya kudhibiti taaluma ya uandishi wa habari, maana kuwa na waandishi wa habari wasio na ueledi, uaminifu ni janga kwa taifa. Leo magazeti yote ya tanzania hayako huru, yako maalumu kusifia akina fulani na kuwachafua akina fulani.

Hakuna habari za maana ni siasa uchwa, matusi ,sifa za kijinga na kukomoana. Wapi habari za hatima ya polisi waliouwawa mbande, watafiti wa Arusha, wapi habari kuhusu vyanzo vya moto kwenye shule zetu, wapi habari za kiuchunguzi juu ya kadhia ya madawa ya kulevya na mauaji yasiyo na msingi?

UANDISHI WA HABARI HAUPASWI KUWA TAALUMA YA VILAZA NA WALIOKOSA PA KWENDA.
 
Back
Top Bottom