Kabwe wa CHADEMA awahutubia wana ccm amfagilia mbunge Filikunjombe wa Ludewa

Mar 9, 2011
33
5
IMG_3027.JPG

Mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za mashirika ya umma ,Mhe.Zitto Kabwe ambaye ni naibu katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) na mbunge wa jimbo la Kaskazini akiwahutubia wananchi wa kata ya Mdindi ambao wengi wao ni wana CCM katika mkutano wa Hadhara uliopaswa kuhutubiwa na mbunge wa jimbo hilo Mhe.Deo Filikunjombe (CCM) ambaye ni makamu wa kamati hiyo

IMG_3033.JPG

Kabwe akiwa na mtoto wa kada wa CCM akimuonyesha utajiri wa Ludewa katika milima ya Liganga

IMG_3028.JPG

Wananchi wakimsikiliza Mhe.Kabwe ambaye pia alitumia nafasi hiyo kumfagili mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe
IMG_3021.JPG

Mhe.Kabwe alisema kuwa kazi kubwa kwa sasa kwa watanzania ni kuchapa kazi na kushirikiana na wale waliochaguliwa na kuwa suala la siasa kwa sasa linapaswa kuwekwa kando na sasa ni muda wa kazi

source:Francis Godwin ni mzee wa matukio daima: KABWE WA CHADEMA AWAHUTUBIA WANA CCM AMFAGILIA MBUNGE FILIKUNJOMBE WA LUDEWA
 
Huyu jamaa natamani kumuona akirudi CCM na kuachana na CHADEMA kwa sababu haendani na CHADEMA ya sasa!!
 
Anastahili maombi baba mchungaji, au huyo mbunge aliona hatari ya wananchi kutokuhudhuria mkutano wake akamwomba ndg Zitto amsaidie, ni fikra zangu tu!
 
Mchungaji karibu, Huyo jamaa anahitaji tiba kutoka kwako amepata matatizo ya dislocation ya ubongo, hope utamsaidia maana dawa zako du , spectrum yake very wide.
 
wewe endelea kutumia ID ya mtu aliyeshukiwa na nguvu za kimungu kwa kupost upupu .... hilo jina litaku cost ..... wenzako wanaponyeshwa wewe ndo utaangamia kwa uparamama
 
Sitaki kuamini hicho kilichoandikwa na mtoa mada nadhani unahitaji kuleta vithibitisho zaidi isije ikawa ni miongoni mwa kundi kubwa la wapiga propaganda walioibuka kwa kasi hapa jf
 
Hao raia wa Ludewa walikuwa wanamsubiri mbunge wao Deo Haule Filikunjombe akiwa kwenye msafara na Mbunge Kabwe walipokwenda kutembelea mradi wa machimbo ya madini ya chuma na makaa ya mawe huko Ludewa ndani ya mkoa mpya wa Njombe.
Mbunge Deo Haule Filikunjombe ambaye alitakiwa awasalimie wanaludewa akaamua ampishe mbunge mwenzake ambaye ni Mwenyekiti wake na hivyo Kabwe kwa ustaarabu wa kawaida hata ungekuwa wewe utapaswa kuongea kwa busara katika mazingira hayo.
Hapa si kampeni za uchaguzi ila wapo katika majukumu ya kitaifa kwa pamoja.

Wanajamii forums tujaribu kuwa na mtazamo chanya si mtazamo hasi tu jamani
 
maelezo yako yanakidhi haja ya hoja mkuu.
 
Mchungaji,
Kwanza pole kwa kazi kubwa ya kuhudumu (japo siamini kama ndiwe)

Zitto ni kiongozi ktk jamii,
  • Je, alihutubia mkutano wa chama cha mapinduzi ulioandaliwa kwa ajili yake?
  • Je amekwenda kikazi akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ama kada wa chama ?
  • Anafahamika kuwa ni mtu wa Chadema na ni mbunge kupitia chama hicho, je aliombwa na wana-CCM ahutubie katika mkutano wao wa hadhara ama?
  • Je hapo alipokwenda alikuwa ni katika kuwatumikia wananchi au anafanya campaign fulani?
 
Hao raia wa Ludewa walikuwa wanamsubiri mbunge wao Deo Haule Filikunjombe akiwa kwenye msafara na Mbunge Kabwe walipokwenda kutembelea mradi wa machimbo ya madini ya chuma na makaa ya mawe huko Ludewa ndani ya mkoa mpya wa Njombe.
Mbunge Deo Haule Filikunjombe ambaye alitakiwa awasalimie wanaludewa akaamua ampishe mbunge mwenzake ambaye ni Mwenyekiti wake na hivyo Kabwe kwa ustaarabu wa kawaida hata ungekuwa wewe utapaswa kuongea kwa busara katika mazingira hayo.
Hapa si kampeni za uchaguzi ila wapo katika majukumu ya kitaifa kwa pamoja.

Wanajamii forums tujaribu kuwa na mtazamo chanya si mtazamo hasi tu jamani
Asante sana kwa maelezo yako mazuri.....
 
Wee Hi ID achana nayo wala usidhani ni ujanja!! huo ni ushamba na ujinga! Kuwa na heshima bwana! we mkwere nini?
 
Aliyekuwa anasubiriwa na wananchi hapo alikuwa ni mbunge wao Deo Haule Filikunjombe na si Zito Kabwe. Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe aliona busara ampishe mwenyekiti wake Zito Kabwe azungumze na wananchi wa Ludewa kwa vile wapo safari moja ya kikazi kwenda kukagua mradi wa machimbo ya Chuma na Makaa ya mawe huko Liganga, Mundindi na Mchuchuma Ludwa.

Wanajamii forums tuwe waelewa na wenye mtazamo mpana katika masuala ya maendeleo ya taifa na umoja kitaifa.

IMG_2898.JPG
IMG_2884.JPG
IMG_3033.JPG
IMG_2994.JPG
IMG_2969.JPG
Zito.JPG
IMG_3027.JPG
IMG_3033.JPG
IMG_3028.JPG
IMG_3021.JPG
IMG_2941.JPG
IMG_2784.JPG
IMG_2790.JPG
IMG_2779.JPG
IMG_2776.JPG
IMG_2761.JPG
IMG_1694.JPG
IMG_2707.JPG
IMG_2712.JPG
IMG_2702.JPG

MWENYEKITI wa kamati ya bunge hesabu za mashirika ya umma (POAC) Zitto Kabwe kuona wawekezaji wa miradi hiyo wakifanya kazi kwa kasi ndogo na kuonya suala la Dowans halitegemewi lisitegemewe tena.. (chadema) ameonya vikali kuwa kamati yake haitakata

Kabwe ametoa onyo hilo wilayani Ludewa wakati wa kikao cha pamoja kati ya wawekezaji wa kampuni ya NDC na kamati hiyo ya bunge yenye wajumbe 16 ikiongozwa na mwenyekiti Kabwe na makamu wake mbunge wa jimbo hilo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).

Alisema kuwa lengo la wabunge kuwachagua kuongoza kamati hiyo ni kutaka kuona kuwa kasoro mbali mbali za wawekezji katika kuendesha miradi hiyo zinafanyika kwa wakati badala ya kuendelea kuona utekelezaji wake ukienda kwa kusua q`q sau huku Taifa likiwa katika adha kubwa ya umeme.

"Napenda kipindi chetu cha miaka miwili na nusu cha kuongoza kamati hii kinapo malizika lazima suala hili la uchimbaji wa madini huku wilaya ya Ludewa liwe limeaza ….hatupendi kuona suala hili likikwama …..kweli lazima tumalize kwa mafanikio ….sio mradi umeanza kuzungumzwa kwa zaidi ya miaka 10 sasa bila kutekelezwa"

Aidha aliswema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutalisasidia taifa kuondokana na adha yha mgao wa umeme nchini kwa kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 1000 za umeme.

Hata hivyo alisema toka kupatikana kwa uhuru wa nchini imekuwa na uwezo wa kuzalisjha megaati za umeme 1034 huku mahitaji ya matumizi ya umeme yakiongezeka kila siku kwa kuwa na viwanda na watumiaji wa kawaida.

"Tukiangalia hasadi za Bunge kila imekuwa ikizungumzwa miradi ya umeme ya Linganga nas mchuchuma lkakini kumekiuwa hakuna utekelezaji sasa tunahitaji kuona kazi kuliko maneno zaidi" alisema Zitto.

Alisema katika maswala ya uwajibikaji kamati yake hatakuwa na upendeleo katika ufanyikazi kati ya NDC na Tanesco katika kuhakikisha wanafanyakazi kwa maslahi ya Taifa.

Awali itoa maelezo kwa wajumbe wa kamati hiyo Mkrugenzi Mtendaji wa NDC Gedion Nasari, alisema utafiti ulio9fanywa kuanzia mwaka 2008 unaonyesjha makaa yam awe zaidi ya tani milioni 250 zilizohakikiwa na kutegemea kuzalisha umeme kwa kutumia makaa yam awe.

"Ukiondoa Mradi wa Mchuchuma na Ngaka tunategemea kujenga mitambo ya kuzalisha umeme maeneo ya Kyela karibu na bandari y6a Itungi na mpango huo unalenga kusafirisha makaa yam awe kutoka ngaka, Mchuchu hadi Itungi kupitia Ziwa nyasa ambapo uzalishaji wa umeme unaweza kufikia megawati 1000 kwa kutumia makaa Geothermal" alisema Nasari

Umeme utakaozalishwa utaunganishwa katika gridi ua Taifa kutoka Mbeya na kuziotaja changamoto zilizopo katika utekeleza wa miradi hiyo ya mchuchuma na Liganga kuwa ni pamoja na miundombinu ya barabara,reli na umeme.

Awali makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Filikunjombe alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakati utasaidia kukuza maendeleo ya Taifa pamoja na kufungua milango ya kimaendeleo katika wilaya ya Ludewa .

Hata hivyo alisema sehemu ya changamoto ambazo wilaya hiyo inakabiliwa kama barabara upo mkakati wa serikali kutegeneza barabara ya lami kutoka Njombe hadi Ludewa japo alitaka wawekezaji hao kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuepuka ubabaishaji .
Source: Francis Godwin - Iringa
 
Hao raia wa Ludewa walikuwa wanamsubiri mbunge wao Deo Haule Filikunjombe akiwa kwenye msafara na Mbunge Kabwe walipokwenda kutembelea mradi wa machimbo ya madini ya chuma na makaa ya mawe huko Ludewa ndani ya mkoa mpya wa Njombe.
Mbunge Deo Haule Filikunjombe ambaye alitakiwa awasalimie wanaludewa akaamua ampishe mbunge mwenzake ambaye ni Mwenyekiti wake na hivyo Kabwe kwa ustaarabu wa kawaida hata ungekuwa wewe utapaswa kuongea kwa busara katika mazingira hayo.
Hapa si kampeni za uchaguzi ila wapo katika majukumu ya kitaifa kwa pamoja.

Wanajamii forums tujaribu kuwa na mtazamo chanya si mtazamo hasi tu jamani

Mkuu hapo umeiweka vyema.
 
Huyu jamaa natamani kumuona hakirudi CCM,na kuachana na CHADEMA!kwa sababu haendani na CHADEMA ya sasa!!
Hiyo ina maanisha kuwa Siasa sio chuki kama wanavyofanya ccm, kuchukia wabunge wa Chadema sasa mnafundishwa jinsi ya kuwa binaadamu sio kuwa wanyama, Pumbafu yenu wana ccm kuweni
 
Hapo pia usishangae kua muheshimiwa Kabwe alikua anakusanya kadi za CCM ambazo wanachama hao walipokua wanazingukiwa na sera za Chadema!
 
Hao raia wa Ludewa walikuwa wanamsubiri mbunge wao Deo Haule Filikunjombe akiwa kwenye msafara na Mbunge Kabwe walipokwenda kutembelea mradi wa machimbo ya madini ya chuma na makaa ya mawe huko Ludewa ndani ya mkoa mpya wa Njombe.
Mbunge Deo Haule Filikunjombe ambaye alitakiwa awasalimie wanaludewa akaamua ampishe mbunge mwenzake ambaye ni Mwenyekiti wake na hivyo Kabwe kwa ustaarabu wa kawaida hata ungekuwa wewe utapaswa kuongea kwa busara katika mazingira hayo.
Hapa si kampeni za uchaguzi ila wapo katika majukumu ya kitaifa kwa pamoja.

Wanajamii forums tujaribu kuwa na mtazamo chanya si mtazamo hasi tu jamani

Its only with Candid Scope you can look at issues from diff angles. Umesema yote Candid Scope.

Nape Nauye akienda kwenye mkutano wa Chadema mwafurahia, tatizo li wapi Zito kuhutubia wananchi ambao wengi wao ni wanaCCM.
Hayo maandamano wanafanya Chadema Kanda ya Ziwa yanahusisha wanaChadema tuuuuuuuuuu.

Badili mtazamo maana tunajenga nchi moja
 
Back
Top Bottom