Kabla ya ushahidi wa Mnyika,tuelezee hii siri Mhe.Nchemba

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Leo bungeni mhe.Mwigulu Nchemba amemkumbusha Speaker kuhusu JJ Mnyika kuwasilisha ushahidi vile alimtuhumu kwamba alishiriki kwa namna moja ama nyingine katika ufisadi wa EPA. Kumekuwa na nadharia kwamba Mhe.Nchemba hakuhusika kwakuwa alianza kazi baada ya ufisadi kutokea.Namtaka Mwigulu Nchemba awaeleze Watanzania yafuatayo: 1.Kwa kuwa M/kiti wa chama chake aliwahi kukiri kwamba,fedha za EPA zilikuwa zinarudisha je,aliwajua wale waliokuwa wanarudisha? 2.Kama alikuwa hajui, je yuko tayari kukiri kwa Watanzania kwamba ana nidhamu ya uoga kwani hata pale aliposikia,hakuumuliza mwenyekiti wake wa chama? 3.Kwa kuwa Nchemba anadai hakuhusika,lakini yeye ndiye mtunza hazina wa chama cha mapinduzi ambacho M/kiti wake Rais Kikwete alikiri urudishwaji wa mali,sasa ni kwa kadri gani hakushiriki kutunza hazina za kifisadi- kwa kujua ama kutokujua? 4.Aliwasaidiaje maofisa wa TAKUKURU ili wapate ushahidi akiwa kama raia mwema?
 
kwakukumbusha tu ni kwamba kwanza alikuepo salome mbatia, then rostam, then makala na sasa nchemba ambae hata mwaka hajamaliza. EPA ilifanyika kipindi cha mkapa 2003. sijui huyu ncemba ambae hata mwaka hajamaliza anahusikaje? mnyika alisema kuwa " nchemba ni fisadi anahusika na EPA" hayo ndiyo maneno ya mnyika. ukiweka siasa pembeni, kwa wanaojua sheria, mnyika yuko kikaangoni. na nchemba hamuachi. atafukuzwa bungeni kwa miezi kadhaa kwa kusema uongo kama alivyowahi fukuzwa zitto kabwe
 
Imetulia mkuu.
Nchemba ni memba humu so tunategemea majibu yenye kujitosheleza kwa hoja hizi
 
Nchemba,

Uje huku kwenye bunge kuu na huru (wananchi), huku kuna uhuru na mizani nzuri ya haki kuliko hapo mjengoni kwa madam Speaker
 
Leo bungeni mhe.Mwigulu Nchemba amemkumbusha Speaker kuhusu JJ Mnyika kuwasilisha ushahidi vile alimtuhumu kwamba alishiriki kwa namna moja ama nyingine katika ufisadi wa EPA. Kumekuwa na nadharia kwamba Mhe.Nchemba hakuhusika kwakuwa alianza kazi baada ya ufisadi kutokea.Namtaka Mwigulu Nchemba awaeleze Watanzania yafuatayo: 1.Kwa kuwa M/kiti wa chama chake aliwahi kukiri kwamba,fedha za EPA zilikuwa zinarudisha je,aliwajua wale waliokuwa wanarudisha? 2.Kama alikuwa hajui, je yuko tayari kukiri kwa Watanzania kwamba ana nidhamu ya uoga kwani hata pale aliposikia,hakuumuliza mwenyekiti wake wa chama? 3.Kwa kuwa Nchemba anadai hakuhusika,lakini yeye ndiye mtunza hazina wa chama cha mapinduzi ambacho M/kiti wake Rais Kikwete alikiri urudishwaji wa mali,sasa ni kwa kadri gani hakushiriki kutunza hazina za kifisadi- kwa kujua ama kutokujua? 4.Aliwasaidiaje maofisa wa TAKUKURU ili wapate ushahidi akiwa kama raia mwema?

Mbona waliorudisha pesa ya EPA wanafahamika?

1. Jeetu Patel 2. Maranda 3. Farijala 4. nk
 
kwakukumbusha tu ni kwamba kwanza alikuepo salome mbatia, then rostam, then makala na sasa nchemba ambae hata mwaka hajamaliza. EPA ilifanyika kipindi cha mkapa 2003. sijui huyu ncemba ambae hata mwaka hajamaliza anahusikaje? mnyika alisema kuwa " nchemba ni fisadi anahusika na EPA" hayo ndiyo maneno ya mnyika. ukiweka siasa pembeni, kwa wanaojua sheria, mnyika yuko kikaangoni. na nchemba hamuachi. atafukuzwa bungeni kwa miezi kadhaa kwa kusema uongo kama alivyowahi fukuzwa zitto kabwe
Kwani maaneno ya Zitto kipindi kile yalikua ya Uongo?? Na wasiwasi na uelewa wako wa neno uongo
 
kwakukumbusha tu ni kwamba kwanza alikuepo salome mbatia, then rostam, then makala na sasa nchemba ambae hata mwaka hajamaliza. EPA ilifanyika kipindi cha mkapa 2003. sijui huyu ncemba ambae hata mwaka hajamaliza anahusikaje? mnyika alisema kuwa " nchemba ni fisadi anahusika na EPA" hayo ndiyo maneno ya mnyika. ukiweka siasa pembeni, kwa wanaojua sheria, mnyika yuko kikaangoni. na nchemba hamuachi. atafukuzwa bungeni kwa miezi kadhaa kwa kusema uongo kama alivyowahi fukuzwa zitto kabwe
Ni kama unakiri kimyakimya kuwa CCM ilikomba EPA vile ila kwamba Nchemba hakuhusika! Yangu macho mwisho tutauona pengine.
 
kwakukumbusha tu ni kwamba kwanza alikuepo salome mbatia, then rostam, then makala na sasa nchemba ambae hata mwaka hajamaliza. EPA ilifanyika kipindi cha mkapa 2003. sijui huyu ncemba ambae hata mwaka hajamaliza anahusikaje? mnyika alisema kuwa " nchemba ni fisadi anahusika na EPA" hayo ndiyo maneno ya mnyika. ukiweka siasa pembeni, kwa wanaojua sheria, mnyika yuko kikaangoni. na nchemba hamuachi. atafukuzwa bungeni kwa miezi kadhaa kwa kusema uongo kama alivyowahi fukuzwa zitto kabwe
Kumbe wasema uongo Bungeni wanapaswa kufukuzwa eeh! sasa Zitto kweli alifukuzwa kwa kusema uongo ambao baadae ulidhihirishwa kuwa kumbe ni ukweli.
Sasa yule bwana aliyesema uongo na Lema akadhibitisha kuwa kasema uongo kuhusu sakata la Arusha vipi Bunge likaminya shahidi ule? Au kanuni za Bunge zinalalia upande mmoja?
Sasa msiwe na moto maana Mnyika atadhibitisha uhusika wa Mwigulu katika kula njama za kuficha uhalifu (ambalo nalo ni kosa kisheria) na hatutaki majibu yake yaishie ndani ya ofisi ya spika,yawekwe hadharani na wasipoweka basi tutamwomba Mnyika atuwekee humu.
 
Kwa hiyo basi na mwizi akiiba pesa benk akakamatwa akasema atazirudisha basi aachiwe huru asipelekwe mahakamani

1. Ukimkamata ukampeleka mahakamani unakuwa umempa adhabu stahiki.

2. Lakini imagine kama utaweza ku recover pesa zako angalau kiasi, wakati huo huo ukampata confesion (indirect kwa kurudisha kwake) , na ukapata evidence kwamba alichukua halafu unamshitaki kwa makosa hayo hayo.

Ukiwa na akili timamu utachagua 1 au 2?
 
Kabla ya speaker kuweka hadharani ushahidi wa Mnyika kuhusu yule MZINZI WA IGUNGA,aweke hadharani kwanza ule ushahidi wa Lema juu ya Pinda kusema uongo bungeni juu ya mauaji yaliyofanywa na polisi kule Arusha.
 
Back
Top Bottom