JWTZ: Tutaingia Mtaani kuzisaka Sare zetu kwa Wananchi

Samahani naomba kuuliza, haya ni majukumu ya jeshi au Polisi? Kadri ya maelezo yako.
unavyosikia jeshi wataingia mtaani kukagua sare zao unadhani polisi hawatuwepo,
kuna muda itifaki inavunjwa kulingana na mazingira jeshi anapewa sehemu kubwa ya kufanya kazi yake
 
Kama mtu anakutwa na VAZI linalosemekana ni la Jeshi, ni mahakama pekee, ndio yenye mamlaka kuamua vazi hilo ni la Jeshi au la. JWTZ hawana mamlaka KUTAIFISHA vazi (mali) ya raia pasipo IDHINI ya sheria. Kama mtu amekutwa na vazi ya aina hiyo, sheria inataka utaratibu ufuatwe.

Kama mtu huyo anaaminika kutenda kosa, basi sheria inataka akamatwe, afunguliwe mashtaka kisha mahakama itamke wazi kuwa mtu huyo amekosa au la. Mahakama ndio hutoa adhabu kwa mkosaji au kutoa amri ya KUTAIFISHA mali na si JWTZ ama Jeshi la Polisi.

Angalizo:
Ni jambo gumu mno KUTHIBITISHA mahakamani vazi la Jeshi, hata kama yanafanana vipi na vazi RASMI! Kuna VIELELEZO vinavyotofautisha vazi rasmi kati ya Majeshi ya nchi moja na nchi nyingine. Vielelezo hivyo ni lazima viwepo kwenye vazi lenyewe ili lifanane na vazi la Jeshi.

Lakini, ufanano si wa mwonekano tu! Ukisoma sheria za PENAL CODE, The National Defence Act, 1966 & National Security Act, zote nimeeleza vyema. Kuna "key words" zimetumika kwenye sheria ili kusaidia utambuzi wa mavazi RASMI ya Jeshi.

Sio kwa namna ambavyo wengi wenu mnaaminishwa! Ni vyema sana sheria zikasomwa na KUELEWEKA vizuri. JW kisiwe chombo cha kuleta taharuki kwa raia. Mwisho, mahakama & sheria za nchi hii haziwezi kumkuta mtu na hatia endapo atakutwa na vazi RASMI la Jeshi la nchi nyingine.

Sheria ya Tanzania, inalinda "VAZI RASMI" & "SINAZOFANANA NA VAZI RASMI" tu. Hapa "zinazofanana" ndio imekuwa KIZUNGUMKUTI kueleweka JWTZ au labda wameamua KUPUUZA tu! Hili neno "zinazofanana" lina maana TOFAUTI kabisa na wanachowaambia raia. Sheria zisomwe vyema, zieleweke.

#BabaMwita
20230910_053539.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#BabaMwitaView attachment 2744493

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mkuu we tinga tu na dunda mtaani wakikukamata waambie hizo nguo ulizo vaa ni za jeshi la Bukina faso na hazina logo ya TPDF ukiwashinda mpaka mahakamani na sisi tuta anza kuvaa tukikuchukulia wewe kama reference.
 
Mi nitavaa za Burkina Fasso, halafu nione watanifanyaje. Yaani badala ya kulinda mipaka ya nchi, wao wanakalia tu kuwaza mavazi yanayofanana na sare zao! Aliyetoa hilo wazi ni kiazi sana na ni aibu kwa nchi wametuletea hawa jamaa. Lindeni mipaka ya nchi, hilo ndo lengo lenu kuu. Mipaka ya nchi inajumuisha Bandari, Airport, n.k.
Msiingilie majukumu ya polisi. Au mnatamani kuwa mapolisi mlinde raia na mali zao?!
 
Mnaoandika hovyo msifikiri JF haina limit ya kuwalinda.

Nawashauri muwache kuongea kijinga, wakimtaka mtu hapa JF wana uwezo wa kumpata ndani ya muda mchache sana.

Eleweni kuwa hii mitandao hakuna pakujificha na hakuna kinachofutika hata wewe ukifuta.

Chezeeni vingine, msichezee watu wanaojitolea maisha yao kutulinda.
Una matisho ya kitoto na ya kishamba.

Canada ipi ulienda kusomea unanga??
 
Mnaoandika hovyo msifikiri JF haina limit ya kuwalinda.

Nawashauri muwache kuongea kijinga, wakimtaka mtu hapa JF wana uwezo wa kumpata ndani ya muda mchache sana.

Eleweni kuwa hii mitandao hakuna pakujificha na hakuna kinachofutika hata wewe ukifuta.

Chezeeni vingine, msichezee watu wanaojitolea maisha yao kutulinda.
Hakuna mtu anayejitolea maisha kuilinda nchi, wote wanalipwa vizuri sana n wengine huzitafuta hizo kazi hadi kwa koneksheni na vimemo.
 
Hayo ni mawazo yako lakini kazi ya kijeshi inaeleweka lengo lake ni nini. Au wewe huelewi?

Siongelei mtu kaipataje hiyo kazi, naongelea mtu anaifanyaje hiyo kazi.
 
Back
Top Bottom