JWTZ: Tutaingia Mtaani kuzisaka Sare zetu kwa Wananchi

Blender

JF-Expert Member
Mar 5, 2022
3,463
5,357
Asiesikia la mkuu huvunjika guu, hakuna marefu yasio na ncha, safari 1 huanzisha nyingine, za mwizi 40, Simba mwenda Pole ndio hula..., Za kuambiwa changanya na Zako,msije mkasema hakukumbushwa
Kula chuma hiko
---

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema siku saba zilizotolewa kusalimisha mavazi yanayofanania na sare za jeshi kwa hiari zimeisha, hivyo jeshi litaingia kuzisaka nguo hizo kwa wananchi.

Kaimu mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema jeshi halina utani katika suala hilo, kwani katazo hilo ni kwa mujibu wa kifungu cha 99 cha Sheria ya Ulinzi wa Taifa (NDA) Sura ya 192 sheria namba 24 ya mwaka 1966 yaliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 pamoja na kifungu cha 178 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 na kifungu cha 6 cha Sheria ya Usalama wa Taifa.

“Muda wao wa kusalimisha kwa hiari umeisha, kama mtu atakuwa hajasalimisha basi tutazifuata wenyewe, na mtindo upi tutatumia kuzichukua kwa wananchi tunajua wenyewe,” amesema Kamanda Ilonda.

Ameongeza kuwa sheria inakataza kutengeneza, kuagiza, kuuza na kutumia sare za JWTZ au zinazofanana na sare hizo bila kuwa na kibali kutoka katika mamlaka husika.
 
JWTZ ni moja ya Taasisi inayo heshimika na kukubalika kwa wananchi walio wengi, ziko nyengine. Kama walitoa muda, wakurudisha kesha rudisha na waoga wameshazipoteza kuepuka kukutwa na kidhibiti. Hii ya kuingia mtaani waachane nayo, waendelee na kazi yao kubwa ya kulinda mipaka, hasa kipindi hiki ambacho tunaambiwa liko lango mojawapo muhimu la nchi litakuwa na wageni wakijitafutia ridhiki langoni.
 
Back
Top Bottom