Jussa aishukia serikali ahadi ajira milioni moja

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,127
Ladhu%284%29.jpg

Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Ismail Jussa Ladhu (CCM)



Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, Ismail Jussa Ladhu (CCM), ‘ameishukia’ serikali bungeni akisema imeshindwa kutekeleza malengo yaliyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ikiwamo kutoa ajira milioni moja, badala yake imeishia kutoa ajira 200,000 kwa Watanzania katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2005.
Jussa alitoa madai hayo mazito wakati akichangia hoja katika mjadala wa hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge ya Mwaka 2010/11, bungeni juzi.
Alisema katika ukurasa wa 157 (26) na 159 wa Ilani hiyo ya mwaka 2005-2010, CCM ilitangaza vita ya kuutokomeza umaskini nchini kwa kutekeleza majukumu makuu mawili; ikiwamo kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea na kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Alisema haikuishia hapo, bali CCM iliendelea kuahidi kwenye Ilani hiyo kwamba, kama ingechaguliwa tena, ingeongoza mapambano dhidi ya umaskini na utekelezaji wa hilo ungepaswa kuwa wa vitendo. Hata hivyo, alisema taarifa ya hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2009 na malengo ya uchumi katika kipindi cha muda wa kati (2010/11-2012/13), iliyosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, Juni 10, mwaka huu, inathibitisha hoja yake kwamba, takwimu zilizotolewa na serikali kuwa ajira milioni moja kwa Watanzania katika kipindi hicho, kwamba zimefikiwa na kuvuka kiwango, si za kweli.
Kauli ya ajira milioni moja kuvuka kiwango, ilitolewa kwa nyakati tofauti na aliyekuwa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Kapteni John Chiligati na Waziri wa sasa wa Wizara hiyo, Profesa Juma Kapuya.
Hata hivyo, Jussa alisema katika ukurasa wake wa sita, taarifa hiyo ya hali ya uchumi wa taifa, imenukuu utafiti wa Nguvukazi na Ajira (ALFS) wa Mwaka 2005/06, ambao umeeleza kwamba, watu 760,000 wanaingia katika soko la ajira kila mwaka na kwamba, kati ya hao, 40,000 wanapata ajira.
Alisema ukweli huo ulidhihirika katika hotuba zilizowasilishwa bungeni hivi karibuni katika sekta zote, kama vile uvuvi, madini, miundombinu, ambapo alisema hali imeharibika kabisa na kutolea mfano wa jinsi reli ilivyokwama kufanya kazi katika miaka mitano
Alisema zaidi hivyo, Shirika la Ndege Tanzania (ATC), halijawahi kufa tangu mwaka 1977 lilipoanzishwa, lakini katika miaka mitano ya sasa limedhoofika na kwamba, ukienda katika Bandari, kila siku serikali imekuwa ikilalamikiwa kwamba, hali imekuwa mbaya.



CHANZO: NIPASHE

Jussa aishukia asema hivyo Mbunge Jussa wakati wa Uchaguzi umeshafika? Watu wampe kura nini?
 
Back
Top Bottom