...Jumatatu Natoa talaka kwa Mke wangu....Yamenishinda

Tualike party ya kuachana.

Hauna haja ya kumpeleka Kilimanjaro, nipe namba yake ya simu, mimi ntamtunza hapahapa Dar na ukorofi wake. Natamani nipate mke mkorofi sijapata.

Kwako wanini kwa wenzako, ntampata lini.
 
Kuacha sio suluhisho? Tafadhali tafakari na fikiri sana maisha ya kesho ya hicho kiumbe ulicho changia kukileta Duniani?
 
I think Ngoswe unahitaji kuona wataalamu wa maswala ya ndoa na pengine therapy. Kwanza pole kwa yote, mara nyingine si rahisi kuelewa hali halisi mpaka yakukute. Sisi tunasikia upande mmoja, pengine mkeo nae anayo tele! Si ajabu yamemzidi mpaka hajui pa kuanzia na wewe unaona ni kisirani. Niliwahi kumwambia rafiki yangu ukiona mtu anaanza na wazo la talaka yeye ana shida.

Kama nakumbuka vizuri ulipoleta hili swala tangu mwanzo uliuliza, je, nimwache? na sasa unasema ndio unamtwanga talaka...ndoa inataka moyo. Wewe una matarajio yako nae ana yake...je yanakutana mahali? Ubabe unasaidia? Hayo usemayo umemtimizia ndio alitarajia? Umekaa kimasimango simango hivi...si ajabu ukifika ukikuta kanyamaza...si kanuna...unauliza "hivi wewe nikupendeje? nini umekosa hapa?" na hapo inategemea sauti yako inapanda na kushukaje. Mwingine anaona bora nikae mbali, bora nisiseme nae ili niepushe shari. Oooh! inaelekea hii ni tabia yake...ulioaje bila kujua tabia? au ndio yale ya chap-chap? Maana tena hapa hata ndoa yenyewe huiheshimu unasema...ndoa yenyewe ya serikali! Kwako ndoa ni kile cheti? Hivi bado unaamini wanawake wa leo wanataka cheti? Ili apate mali zako? Is that what you think she needs?

1. Kawaone watu wa zima wakwenu - waeleze wakusaidie. By the way kama wanaitambua ndoa yenu ya serikali...si ajabu pana issue hapa
2. Mfahamu mkeo zaidi - maana humfahamu hata kidogo!
3. Futa wazo la talaka - ukapera haukifai
 
pamoja na ushauri wote mzuri uliopata - NAONGEZEA:

1. Chukua muda wa kumwomba Mungu - fanya maombi ya kufunga kama wiki moja hivi - huku ukimweleza Mungu tatizo lako
2. Ongeza upendo kwa mkeo - KAMNUNULIE ZAWADI NZURI - TENGENEZA TRIP NA MKEO - MWENDE SOMEWHERE NA MTOTO WENU - HALAFU UONE KAMA ATAENDELEA KUNUNA - Mkeo kajifungua - hata zawadi???? yaani mradi unampa msosi tu?? Be loving mr. Ngoswe
3. Mshirikishe mipango yako - yawezekana umemweka kama furniture tu - hajui lolote - BADILIKA na YEYE ATABADILIKA
4. JIPANGE KUFANYA IBADA NA YEYE - UNLESS MNA IMANI TOFAUTI - POLE KAMA NI HIVYO - na labda ndio maana ndoa ilikuwa ya Serikalini????
 
The expected bachelor from monday.....Ngoswe.120

Hey NDOA its about maturity and love... if you don't have that U'll NEVER MAKE IT... sijasoma past complains about ur marriage but from what I got of Ur explanation is U dont talk of your problems.. U need to sit down and talk, Bora Divorce wakati hamna mtoto but tayari mna mtoto na sijui kama umesha fikiria maisha yake baada ya nyie kuachana!!! Hebu ita wasimamizi wenu wa ndoa wawasaidie ikishindikana nenda above to the elder of Ur and Her famiy and try to solve this things, Wanawake wakisha jifungua huwa na mood swing zao wengine hujisikia tayari wamepoteza usichana wao na wanajiona wamezeeka au humpi credit za kutosha ajisikie bado naye yumo na bado wampenda coz NDOA sio hela, chakula, wala nguo its feelings U two have for each other.... na have U consider that U MIGHT BE A PROBLEM on that marriage???? jaribu kutafuta TATIZO MLITATUE sio kutoa SULUHISHO TU!!!! TALAKA.... MAISHA YA huyo baby girl yatakuwa ya ajabu na anaweza kuwa kama wasanii wetu wa kike wasio jiheshimu wa tanzania asipolelewa na wazazi wote wawili... SHE NEEDS YOU TWO TO GROW UP TO A FINE LADY...
 
Vunja ukimya, kuachana sio last resort.....kutoa maamuzi baada ya siku 11 za mnuno sio sahihi,fikiria mara mbili mbili kabla ya kutoa maamuzi,tafakari!
 
aaaaaah
kwanza elewa unaweza kuwa wewe tatzo au mkeo tatizo au wote ni matatizo kwa maana hiyo ni vyema umrudishe kwako upate wasaa au muda wa kutafakari na kujirekebisha na naamini nae atajirekebisha , mpe nafasi tena baada ya miez hiyo nadhani mtaweza kuyamaliza
 
wewe unamatatizo, kubali yaishe ujana umeshakupa mkono kuwa kama baba wa familia mambo ya utoto na ujana yameisha kubali majukumu.............mtu mzima hovyo kabisa unapenda kuchezea vibinti vya watu .....ndoa si kunanihii tu lazima ukubali yote, mkeo amekuona wewe ndio umebdilika hasa kwa hao chokoraa zako wanao kukeep busy hovyoooooooooooooooooooooooooooo
 
Hapa mie ngoja nipite maana Bishanga aka Bepari la kihaya achelewi kunambia nimetoka povu
 
umeridhia mgawane mali japo hajachangia chochote!!!!!!! kwa kweli huo ni unyanyasaji kabisa na hapo nilichonote mimi ww ndio mwenye matatizo si huyo dada na swala la talaka umelifurahia kweli.sasa cjui hapa unataka tukushauri nn wakati umeshasema j3 ndio unampa talaka.lkn usisahau kumwangalia mtoto pia kwani bado mdogo sana.
 
duuh pole bro,
1.umeisha ita watu wazima (ndg wa karibu) wakakusikilizeni.
2.muanja asali haonji mara moja. una hakika kuwa hutohitaji tena mwanamke
3. makuzi nayo yanachangia we una tabia yako, naye ana tabia yake , ni kazi yenu wote kulielewa hilo kisha kusaidiana kuchanganya ili mpate tabia ambayo kila mmoja atamuelewa mwingine kabla ya hatua hiyo.
 
duuh pole bro,
1.umeisha ita watu wazima (ndg wa karibu) wakakusikilizeni.
2.muanja asali haonji mara moja. una hakika kuwa hutohitaji tena mwanamke
3. makuzi nayo yanachangia we una tabia yako, naye ana tabia yake , ni kazi yenu wote kulielewa hilo kisha kusaidiana kuchanganya ili mpate tabia ambayo kila mmoja atamuelewa mwingine kabla ya hatua hiyo.
 
baaada ya miezi miwili utajua for sure nini ufanye
hiyo idea ya kutengana miezi miwili ni safi
talaka sio mbaya lakini usikimbilie hebu peaneni space kwanza
Mkuu lakini kumbuka kwamba maji huwa hayasahau ubaridi wake hata kama utayachemsha mwaka mwaka mzima, ni bure tu..!
 
Mambo ya gubu ndani ya ndoa we acha tu. Inakubidi uwe na hekima ya hali ya juu ktk kutatua tatizo la kununa kwa mwanamke,na ni vyema ujue hii tabia ni karibu kila mwanamke anayo.
 
Ningekuwa mimi hako ka kisirani kake ningekavumilia tu au kukatafutia dawa ya mruturutu kukatibu kwa faida ya huyo mtoto aliyezaliwa ili aweze kupata malezi ya pande zote, baba na mama.
 
ndoa ngumu ona tu tunacheka ndani ya nyumba ili inahitaji ujasiri na uvumilivu wa hali ya juu............
 
Jaribu kumshirikisha kujua nini tatizo na pia kupata ushauri kwa Watu wa karibu na Familia yako pia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom