Juliana Shonza: Mimi bado ni Makamu Mwenyekiti BAVICHA...!

Status
Not open for further replies.
TAMKO LA KUTOA UFAFANUZI DHIDI YA TAARIFA BATILI ZILIZOZALISHWA NA MWENYEKITI WA BAVICHA
BWANA: JOHN HECHE [WEGESA CHARLES SUGUTA] KUHUSU KUVULIWA UANACHAMA WA BAVICHA, NA KUSHABIKIWA NA MH. FREEMAN MBOWE, MWENYEKITI CHADEMA TAIFA



Nawashukuru sana wanahabari, kwakuchukua muda wenu kuja kunisikiliza. Natambua mnakiu ya kusikiliza mambo mengiya kuwaeleza kutokana na taarifa zilizosambaa kuhusu hiki kichefuchefukinachosambazwa kwa makusudi na virusi vichache vilivyojivika ngozi yaukombozi.

Nimepokea simu nyingi kutoka kwawatu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakitaka kupata ufafanuzi baadaya kupata taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa nimevuliwa uanachama naU-Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.Kama mlivyo ninyi, nami pianimeyasikia hayo kupitia vyombo vya habari, maana sijapata barua au mawasilianoyoyote toka kwa Mwenyekiti wa BAVICHA, Ndugu Wegesa Suguta (John Heche)aliyetoa tamko hilo.Kwanza kabisa naomba kuweka wazikwamba sijawahi pewa shutuma zozote au mashitaka yoyote yale yanayohusiana nahicho alichokiongea.

Niliamua kupuuzia kwa sababunamjua Heche ni mlopokaji, kiongozi asiyejua wajibu wake, anayetumikiawasiomchagua, mtu asiye na malengo na mtegemezi wa siasa ili kuendesha maishayake na ya familia yake. Pia nilimpuuza kwa sababu najuasio Mwenyekiti aliyechaguliwa kidemokrasia, aliwekwa kwa matakwa ya wakubwazake ambao wanamtumia kwa malengo yaliyokusudiwa, ikumbukwe kuwa vijana watatu,Habibu Mchange, Mtela Mwampambwa na Grayson Nyakarungu walienguliwa kimizengweili Heche ashinde, hivyo kwetu sisi yeye ni sawa na Mwenyekiti wa kuteuliwa.Hivyo sikumjibu mtu asiyekuwa na sifa sawa na zangu katika harakati za kusakademokrasia ya kweli.

Lakini kitendo cha Mwenyekitiwangu, Mh. Freeman Mbowe kujitokeza kupitia gazeti mojawapo na kudai madaiyangu ni ya kitoto,

kwanza kimenifedhehesha, ni dharau kwa vijana walionionanina sifa na ukomavu na kunipa kura nyingi ili niwe Makamu Mwenyekiti waBAVICHA Taifa.

Pili ni kama anahalalisha kikaobatili, kilichokiuka kanuni na katiba ya CHADEMA ili kuhalalisha matakwa yaoyenye lengo la kuminya demokrasia na uhuru wa kujieleza ndani ya chama.

Tatu anahalalisha hoja za vijana,ambazo ndio uhalisia kuwa Heche hakuwa na sifa, na uwezo, hivyo alibebwa na Mh.Mbowe ili akae pale kwa malengo yake.Ndio maana nilisema ukionakifaranga kimepanda juu ya figa ujue mama yake yuko chini, hivyo mama yakekifaranga kajitokeza kuhalalisha kifaranga chake kupanda juu ya figa.

MADAI YAALIYODAI MH. MBOWE KUWA NI YA KITOTONiseme wazi kwamba nimesikitishwamno na madai aliyoyatoa Mwenyekiti wangu wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe kupitiagazeti la Mtanzamia la tarehe 12/01/2013 kwamba madai yangu ni ya kitoto .

Kwanza niweke wazi kabisa kwambanamuheshimu sana Kiongozi wangu huyu mkuu ambaye ndiye alipaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwambahaligawi baraza la Vijana na chama kwa ujumla, ahakikishe kuna utawala borandani ya chama, na utendaji haki, lakini cha kushangaza ameibuka kumtetea Hechekwa hoja za mwegemeo wa upande mmojabila kuangalia maelezo ya upande wa pili.

Niweke wazi kabisa kwamba kaulialiyoitoa dhidi yangu ni yakiushabiki maana kama ni madai yangu kuhusu namna ninavyohujumiwakupitia kwa Katibu Mkuu yeye anayo nakala ya malalamiko [ushahidi upo], lakinihakuna hatua ambayo ameichukua.

Namshangaa Mwenyekiti kudai madaiyangu ni ya kitoto sasa sijui ni madaiyapi anayazungumzia ? madai ya kitoto ni yapi? na madai ya kikubwa ni yapi ? naje madai ya kitoto ni haya mimi kuhoji kwanini hatuweki akiba kwenye akauntikwa ajili ya uchaguzi 2015 kama tulivyokubaliana kwenye baraza kuu mara baadaya uchaguzi wa 2010.Naombaniwajulishe wanachadema kuwa, nimejitahidi sana kushauri juu ya

1; Uanzishwaji wa chuo chamafunzo ya uongozi kwa makada wa CHADEMA , badala yake ni matumizi mabaya yafedha za ufadhili wa wadau tofauti na hasa mfadhili mkuu ndugu SABODO. Hiiingesaidia pia kulea ki-mfumo wa maadili ya uongozi kwa vijana wa umoja wawanafunzi wa CHADEMA wa vyuo vikuu yani “ CHASO” ambapo mimi ni mwasisi wamkakati huu nchini.

2; Chama kwa ujumla kutokuwa na jengo letu na hasa makao makuu yetu. Niaibu kwa chama kikubwa kama CHADEMA kuwa na ofisi tulizopanga na kulipa mamilioni ya fedha za ruzuku na misaada kwa manufaa ya Mwenyekiti Freeman Mbowena Mkurugenzi wa fedha wanaomjua mmiliki wa jengo la makao makuu. Kimsingi mimi natambua chama kina uwezo mkubwa wa kuwa na majengo yetu.

3; Kupunguza mshahara wa katibumkuu Ndugu Dk. Slaa ambao ni zaidi ya milioni saba kwa mwezi na marupurupu kibao ili pesa hizo na mamilioni zielekezwe kujenga chama mikoani kama kweli tunataka2015 tuingie Ikulu.

4; Kuhakikisha pesa zilizochangishwa kwenye M4C zinatumika ipasavyo na si kama zitumikavyo kipindihiki ambapo ni kama tumelewa wingi wa watu kwenye mikutano ya hadhara.

5; Kitendo cha Mwenyekiti wa chama kufumbia macho hatua ya ndugu Slaa (katibu mkuu) kujikopesha pesa ya ruzuku ya watanzania zaidi ya shilingi milioni mia na arobaini.

6; Hatua ya mwenyekiti ndugu Heche kulipwa mshahara na marupurupu hali kanuni za chama haziruhusu huku Mbowe akifumbia macho wakati viongozi wa mikoa na wilaya hawapewi pesa na vifaa vya uenezi.

7; Kitendo cha mchumba wa Dk.Slaa, Josephine Mushumbusi kuzunguka mikoani na kulazimisha kupokelewa kama mke wa mfalme na kuendesha vikao vya ndani na mikutano ya hadhara yenye kulenga kuwajenga wagombea ubunge anaowataka yeye na katibu mkuu kwa mwaka 2015.

Ndugu wanahabari, je hizi ndo hojaza kitoto anazodai Mh. Mbowe? Hivyo basi namtaka Mh. Mbowe sasa asikimbiliekujibu hoja kiushabiki. Ajitahidi kuwa na fikra na Busara ili kukisaidia chama kuvuka kwenye daraja la sasa la pepo kufukuzana. Atambue Baraka anazozitoa wanachama wafukuzwe hovyo na kunyanyaswa ni hatari kwa kuwa anaandaa kundi kubwa nje ambalo litageuka mwiba siku za usoni.

UHALISIA ULIOPO:

Ndugu waandishi wa habari,
Naomba kuweka wazi kwamba mimi Juliana Shonza ni Makamu Mwenyekiti halali wa baraza la vijana (BAVICHA). Taarifa zozote zile mlizozisikia kuhusu kuvuliwa kwangu uanachama, naomba kwa nguvu moja kupitia taaluma yenu muwaambie watanzania kwamba wazipuuze. Ni taarifa zilizotolewa na kikundi cha kihuni kilicholenga kutimiza matakwa ya wakubwa wao. Kikundi hicho hakina mamlaka ya kikatiba yoyote yale ya kunivua uongozi huunilio nao.

Kuthibitisha hilo kuwa ni kikundimufilisi, hadi ninapoandika waraka huu kwenu sijapewa barua yoyote ile inayonitaarifu kuwa nimevuliwa uongozi wangu. Hii ni wazi wanatambua kuwa wanachemka, wanatengeneza makundi kwa maslahi wanayoyaona yanawafaa.

Sikuchaguliwa ili niwe chombo cha kuwatumikia watu, na badala yake nilichaguliwa ili niwatumikie vijana waCHADEMA na watanzania kwa ujumla, na pale nilipoona kuna ukiukwaji na kuhoji ndio chanzo cha mizengwe na matamko ya Ndugu Wegesa (John Heche).

Nimekuwa nikiwasumbua viongozi wenzangu kuhusu kutengeneza kadi za BAVICHA na kusajili wanachama katika mfumo mzuri (database) ili tuwe na kumbukumbu ya wanachama wetu lakini yote yameshindikana kwasababu amekuwa akiendeshwa na mfumo dume kandamizi kwa mwanamke, mara nyingi nimemshauri kwa ajili ya maendeleo ya Baraza na nimekuwa nakwamishwa na Mwenyekiti na Katibu na hata leo sisi wote ni wanachama kwa kufikirika (imagination), kwa kuwa bado hatuna kadi za uanachama kwa vijana wa BAVICHA zaidi ya kutambulika na katiba ya chama.

KUKIUKWA KWA KATIBA

Ndugu wanahabari, ni wazi kuwakatiba pamoja na mwongozo wa baraza letu la vijana bavicha ulikiukwa katikakikao walichokiita kamati tendaji iliyokaa tarehe 05/01/2012 ambayo iliongozwa na Bwana Wegesa Suguta (John Heche) kama Mwenyekiti, hali inayonilazimu kusema wazi, bila kumung’unya maneno kwamba maamuzi yaliyotolewa na kikao hicho yalikwishapangwa na viongozi wa kitaifa hayakuwa halali. Nasisitiza kwamba ni ukweli ulio wazi kwamba agenda na maazimio ya kikao hicho yalikwisha amuliwa hata kabla ya kikao hicho kwasababu kubwa mbili:

1; Taarifa za kufukuzwa kwetuzilikwisha anza kusikika kwenye mitandao ya kijamii kama vile jamii forum nafacebook mwezi mmoja kabla ya kikao cha kamati tendaji batili.

2; Pili ushahidi wa kimazingirakwa maana ya ukiukwaji mkubwa wa kikatiba na mwongozo wa Baraza letu la Vijana uliofanyika siku ya kikao.

Ndugu wanahabari,
Ikumbukwe kuwa pamoja na uwepo wa taarifa za kikao mwezi mmoja kabla binafsi nililetewa taarifa hizo siku mbili kabla ya kikao, tena kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi {sms} na baadae kupigiwa simu na Katibu wa Baraza Bwana Munishi ikinitaka kuhudhuria kikao hicho kutokana na kuwa nje ya Dar-es –salaam kwa mambo ya kifamilia zaidi niliwataarifu viongozi wenzangu kwa utaratibu maalumu wa mawasiliano ya kiuongozi kwa maana ya kuwatumia barua ya udhuru wa kutohudhuria kikao.

Lakini cha kushangaza na kustaajabisha kwa viongozi wenzangu hawa ambao kwa namna moja ama nyingine napata ugumu wa kuelewa kama kweli wana sifa za kuitwa viongozi tena wa idara nyeti sana katika ustawi wa chama chetu, kwa makusudi kabisa ama kwa kutumwa kufanya hivyo ama kwa utashi wao mdogo wa kiupembuzi yakinifu waliamua kuvunja na kukiuka katiba ya chama na kujipa vyeo vya kiunyampara kwa kuamua kuchukua maamuzi ya kutuvua uanachama wa kufikirika wa baraza mimi na vijana wenzangu Ndugu Mwampamba na Mchange ambao nao hawakupewa nafasi ya kusikilizwa, ambao moja kwa moja tunapoteza sifa yakuwa wanachama wa CHADEMA.

Ndugu wanahabari,
Naomba sasanijikite katika katiba ya chama changu na mwongozo wa baraza la vijana sura ya sita kipengele cha 6.5 ambacho kinasema taratibu zifuatazo lazima zifuatwe katika kuchukua hatua za kinidhamu. 6.5.2 kwa mujibu wa ibara 5.4.3 na .4.4 ya katiba, mwanachama yeyotehatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza

{a} kujulishwa makosa yake kwamaandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
kupewa nafasi yakujiteteakatika kikao kinachohusika.
{c} Mwanachama atajulishwa kwamaandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.

Ndugu waandishi wa habari,Nisemewazi kwamba hakuna kifungu kilichofatwa kati ya hivyo niliyoviainisha hapo juu,hakuna barua yeyote niliyojulishwa ya hayo waliyoyaita mashitaka yangu zaidi ya kuyasoma na kuyasikia kwenye vyombo vya habari baada ya wao na kikao chaoharamu kuchukua maamuzi yakunivua uanachama wa Bavicha .

Sikupewa nafasi yakujitetea maanasikuwepo kwenye kikao, barua ya udhuru wakutohudhuria walikuwa nayo. Na vilevile mpaka leo hii sijajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao hicho batili badaa yake viongozi wenzangu hawa wameamua kuujulisha umma wa Watanzania na wanachadema kwa ujumla pasipo kunijulisha mimi kwanza. Ukiangalia pia kifungu cha 6.5.6 cha katiba kinasema KIONGOZI YEYOTE hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu kwa maandishi.

Sasa basi namtaka Bwana Wegesa Suguta awaeleze umma wa watanzania kama alivyokurupuka kuwaeleza kwamba Shonza amevuliwa uanachama wa Chadema ni wapi na lini yeye kama Mwenyekiti nilipewa barua ya hayo wanayoyaita mashitaka, na ni lini niliwapa majibu ya mashitaka hayo.

UHALALI WAKIKAO CHA KAMATI TENDAJI

Ndugu wanahabari,
Ikumbukwe kwambakikao cha juu kuliko vyote kwenye ngazi ya chama husika ni Mkutano Mkuu ambao ndio ulioniweka madarakani kutokana nakuwa na imani na mimi na kikatiba ndiohaswa ulipaswa kuniandikia mashitaka, kunijadili, kunihoji na kutoa maazimio ambayo yangepelekwa kamati kuu ambao kimsingi ndiyo yenye mamlaka ya mwisho yakumvua mtu yeyote uanachama wake baada ya kujiridhisha na taarifa na uchunguzi kutoka kwenye kikao husika kilichomwandikia mwanachama mashitaka na kumuhoji.

Ndugu wanahabari ifahamike wazikwamba kikatiba kuna ngazi mbili tu zinazoweza kumvua mtu uanachama wake ambazoni ngazi ya tawi na ngazi ya kamati kuu.

Hivyo basi namtaka sasa Bwana Wegesa Suguta auambie umma wa watanzania kwamba ni lini kamati tendaji ya vijanailigeuka ama kukaimishwa madaraka ya ngazi ya tawi, ngazi ya mkutano mkuu amakamati kuu yakuwa na uwezo wakumvua kiongozi uanachama wake?

Ndugu waandishi wa habari,
Wajumbe wa kamati tendaji kikatiba ni makatibu wa kamati za uratibu za mikoa lakini badala yake Bwana Wegesa Suguta (John Heche) amekuwa akiwaita wenyeviti wamikoa na sababu kubwa ikiwa ni kwamba wengi wa wenyeviti hao hawastahili kuwepobavicha kutokana na kwamba umri wao kuwa zaidi ya miaka 35 hivyo kupoteza sifa za kuwa viongozi wa BAVICHA ambayo katiba inamtaka mwanabavicha yeyote kuwa namiaka 18-35, hivyo basi kwa kuhofia kupoteza nafasi zao hulazimika kukubaliana na lolote lile ambalo bwana Wegesa Suguta analitaka hata kama wakijua kwamba ni kinyume kabisa na matakwaya katiba na mwongozo wa baraza.

Hivyo kumpa Heche mwanya wakuamua lolote lileanalotaka ama kutumwa kulifanya. Kutokana na hilo natangaza wazikwamba kikao cha kamati tendaji kilichopita ni batili, chenye wajumbe batili, kimesimamiwa na viongozi batili kwa maana ya mwenyekiti na katibu wake maana wameshindwakuheshimu misingi ya kikatiba katika namna ya demokrasia ya chama chetu hivyo basi nachukua nafasi hii kuutangazia umma wa watanzania na wanachadema kwa ujumla wao kwamba maamuzi ya kamati tendaji yaliyotangazwa na kiongozi kilazana daraja la viongozi wa juu bwana Wegesa Suguta ni batili.

Ndugu wana habari,
Sifa ya Mwalimu ni kuweza kubadilisha hali ya umbumbumbu wa wanafunzi wake, Heche kama kiongozi, na Mwalimu kitaaluma (nina wasiwasi na ufaulu wake katika huo ualimu) alipaswa kuwa mfano bora kwa vijana wa Chadema kuwaelekeza na kuwafundisha namna ya kuheshimu misingi ya kikatiba ambayo kama chama na baraza tumejiwekea na tunapaswa kuifuata ni wazi kuwa Heche ameshindwa kuwa mfano bora kwa vijana, hajui kanuni za BAVICHA wala katiba ya CHADEMA, mkurupukaji, mropokaji, mwenye uwezo mdogo wa kufikiri, dikteta anayetumia mamlaka asiyokuwa nayo (akipewa mamlaka atatuchinja huyu) hivyo hafai kuwa hata Mwenyekiti wa serikali za mtaa, wala kuaminiwa popote kupewa nafasi ya kiuongozi. Ni wazi ubongo wake yeye nakatibu baraza bwana Munishi haujapewa tohara la kisiasa, ifike mahali wakubali kufundwa unyagoni na manyakanga wa kisiasa.

KUHUSUKUVULIWA UANACHAMA WA BAVICHA;

Ndugu wanahabari,
Kuhusu kuvuliwauanachama wa Bavicha ambao moja kwa moja napoteza sifa ya kuwa mwanachadema namshangaa kiongozi huyu ambaye sifa yake kuu siku zote ni ukurupukaji kwa kusema kwamba nimevuliwa uanachama wa Bavicha huku akijua wazi Bavicha haijawahi kuwa na kadi za baraza.

Katika mwongozo wa baraza lavijana kipengele cha 4.4 KUJIANDIKISHA UANACHAMA 4.4.1 inasema ili kijanaaruhusiwe kujiunga bavicha ni lazima awe na sifa zifuatazo
[a] Awe mwanachama wa CHADEMA
Awe na umri kati ya miaka 18 na 35
[c] Awe anakubaliana na misingiya mwongozo wa BAVICHA

4.4.2 Inasema kijana aliyekidhimatakwa hayo hapo juu, atanunua kadi ya uanachama wa BAVICHA

Kutokana na kipengele hicho namtaka bwana Wegesa Suguta auambie umma wa watanzania na wanaCHADEMA kadi yake yeye ya baraza la vijana ni namba ngapi na aliichukulia wapi? Aueleze umma wa watanzania kadi yangu ya baraza la vijana ni namba ngapi na niliichukulia wapi?

Ndugu waandishi wa habari,
Nidhahiri baraza la vijana chadema hatuna kadi ambayo kimsingi ndiyo utambulisho wa mwana BAVICHA endapo akishakidhi sifa zilizoainishwa hapo juu. Na ni wazikwamba vijana wote wa CHADEMA tuna sifa za kuwa wana Bavicha lakini si wanachama wa BAVICHA kutokana na kwamba nimekuwa nikimwambia mara kwa mara umuhimu wa kuirasimisha na kuianzisha ili iwe taasisi kamili kwa kuwa na kadi za vijana kama mwongozo wa vijana unavyojieleza.

UELEWA WANGU KUHUSUKUNDI ANALOLIITA NDUGU WEGESA SUGUTA (JOHN HECHE) NI “MASALIA”


Ndugu waandishi wa habari,
Hakuna kundi linaloitwa masalia ndani ya Chadema na BAVICHA. Gazeti la MWANAHALISI ndilo lililoandika kuwa vijana wote waliofutwa na kuondolewa kwenye uchaguzi wa BAVICHA mwaka 2011 ni MASALIA ya Zitto yanayopukutishwa Chadema. Kimsingi gazeti hili lilikuwa linafanya kazi yake ya kipropaganda ndani ya CHADEMA ili kukigawa Chama. Lilikuwa linatimiza wajibu wake wa kupika mpasuko ndani ya chama tena kwa kuhusisha na viongozi wakubwa ndani ya chadema.

Ni aibu kubwa sana na ni hatari kuona kiongozi kama Wegesa Suguta anakuwa mstari wa mbele kushabikia neno masalia, huku akijua wazi kufanya hivyo ni kuligawa baraza la vijana. Kwa nguvu moja nalaani kitendo hiki cha kipuuzi kinachofanywa na Mwenyekiti huyu wa BAVICHA cha kuchekelea upuuzi uliopikwa na gazeti la MwanaHalisi. Naomba atumie rasilimali za chama kujenga umoja wa vijana imara, tushirikiane kuimarisha Bavicha yenye tija kwa chama na sio kusherekea mpasuko ndani ya baraza la vijana.


UELEWA WANGU KUHUSU KITU KINACHOITWA PM7

Ndugu waandishi wa habari,
Naomba kunukuu maneno ya mtu maarufu sana mitandaoni na kwenye uga wa habari Mzee Mwanakijiji anasema
”Uongozi imara sio kutegeana, kunyemeleana na kufukuzana. Uongozi imara ni kushirikiana”.

PM7 ni jina lenye maana ya “PATRIOTIC MOVEMENT” yaani harakatiza kizalendo kwa mujibu wa Ndugu Ben saanane ambaye alitumwa na kiongozi wa juuwa chama kuja kulitekeleza kwa vijana walioenguliwa kwenye uchaguzi wa BAVICHAmwaka 2011 na wanaoonekana kusigana na kiongozi huyo kimawazo. PM7 ni wazoliliobuniwa na kiongozi mmoja wa juu wa chama akishirikiana na Ben saanane wakinuia kutega mtego wa kuwanasa vijana wanaoonekana wapo tofauti kimawazo nakiongozi huyo wa chama. Kwa kuwa wazo hilo lilikuwahalina manufaa kwa chama, halikutekelezwa.

Kiongozi huyo bila kumung’unya maneno ameamua kuwatumia vijana hao kuandaa kikao batili cha kamati tendaji ya John Heche ili awafukuze vijana hao. Hii ni hatari sana kuona kiongozi wa chama unageuka simba na kuanza kuwawinda watoto wake ili uwamalize kisiasa kwa sababu zako binafsi.

MAAJABU KATIKAMEDANI ZA SIASA ZA BAVICHA MWAKA 2013

Ndugu waandishi wa habari,

1. Hii ni ajabu sana katika kikaocha kamati tendaji batili, Ambao hatukuhojiwa ni watu wawili, mimi Juliana Shonzana kijana mmoja anaitwa Exaud Mamuya. Lakini Mimi Juliana Shonza nimehukumiwa bila hata kusikilizwa wala kupewa mashitaka na chombo chochote katika chama. Wakati huo huo Exaud Mamuya hajahukumiwa kwa madai hakufika kwenye kikao. Hii ni dhahiri huu ni mkakati wa kipuuzi ambao unaendeshwa na watu wapuuzi tena kwa misingi ya kikabila na kikanda.

2. Muasisi mwenza wa PM7 na kibaraka wa kiongozi wa juu wa chama aliyetumika kutoa shutuma chafu kwa Naibu Katibu Mkuu. Kijana anayefahamika kwa jina la Ben Saanane ameachwa kwa madai yeye amekiri mbele ya hiyo kamati tendaji kwamba ni kweli alinuia kumchafua Naibu Katibu Mkuu wa chama na kukivuruga chama. Wakati tuhuma zake zinafananana za Mchange na Mwampamba.

3. Mkakati wa John heche navibaraka wake umejikita kutukuza ukanda ndani ya chama tena wa wazi wazi.Ukanda huu umejidhihirisha kwenye kutoa hukumu batili za tuhuma kama ifuatavyo.

Vijana waliohukumiwa wote niwale wanaotokea Mbeya, Mbozi na Kibaha. Wakati Vijana wa Kilimanjaro wameachwa kwa madai wao wametoa ushirikiano.

Waliohukumiwa ni:
_Mtela Mwampamba-Mbozi, Mbeya
_Habib Mchange-Kibaha, Pwani
-Juliana Shonza-Mbozi, Mbeya
-Joseph Kasambala – Mbeya mjini (kasimamishwa)
- GWAKISA Mwakasendo –Rungwe, Mbeya (kasimamishwa)

Pamoja na wanachama watatu waliopo Mbeya mjini waliofukuzwa uanachama.

Waliosamehewa ni:
_Ben saanane-Kilimanjaro
_Exaud Mamuya-Kilimanjaro.

Hii ni dhamira ya wazi kabisa kwamba CHADEMA sasa ni chama cha kikanda, Viongozi wa CHADEMA wanatumika kutangaza ukanda kwa watanzania.

Kwa maana hiyo wale wote wasio wa kaskazini ndani ya Chadema tusitegemee kutendewa haki.

MAMBO NILIYOMSHAURI HECHE NA KUMUONYA:

Ndugu waandishi wa habari, Sisikama vijana tusigeuze siasa kuwa ajira wala chombo cha kuendeshea maisha, ni moja ya vikwazo katika kukuza demokrasia ya kweli, maana wengi wanaendekeza njaa na uhitaji wa maisha yao ili kupindisha ukweli.

Moja ya maswali yangu kwa Mwenyekiti ni kitendo cha kubinafsisha gari alilotoa Naibu Katibu Mkuu kwa ajili ya BAVICHA na badala yake akalifisadi, akafanya mali yake binafsi na kumuweka Mdogo wake Chacha Heche kuwa dereva wake, nimekuwa nikipinga matumizimabaya ya rasilimali hiyo kwa manufaa binafsi, na badala yake gari hiyo ifanyekazi iliyokusudiwa, huu ni msingi wa kuonyesha tofauti yetu na wanaotumiarasilimali za serikali (Taifa) kwa manufaa binafsi nay a familia zao.

Pia nilimshauri Mwenyekiti awe nakipato halali kama katiba ya chama inavyosema Sura 10 MAADILI YA VIONGOZI ibara ya 10 kifungu cha (6) kinasema Kiongozi anatarijiwa kujitosheleza yeye nafamilia yake kwa mapato halali ili kutokuwa ombaomba kwani tabia hiyo itadhoofisha uwezo wake wa kutoa uamuzi sahihi, ili kuwa mfano bora wauwajibikaji kwa vijana, kama ambavyo Mwalimu Nyerere alivyosema kipimo cha Utuni kufanya kazi, badala yake ametelekeza taaluma ya ualimu, aliyotumia pesa za walipa kodi kwa kusoma na muda wote ni kupiga soga bila uzalishaji na kujipatia kipato halali, na badala yake anategemea mshahara usio halali kuishi, ni wazi Mwenyekiti ni cheo cha kisiasa na hatakiwi kulipwa mshahara, wala kulipiwa nyumba kwa mujibu wa kanuni.

Badala yake majibu anafikiri ni kufanya njama na waliopindisha taratibu hizo ili alipwe mshahara kwa maslahi yao ya kisiasa. Na tumekuwa tukilipinga hilo kwani tunataka tuwe mfano wa utawala bora kwa vitendo na si maneno peke yake.

MWISHO:

Ndugu waandishi wa habari,
Nipokwenye mchakato na wanasheria wangu kushughulikia swala la kumpeleka mahakani Bwana John Heche na gazeti la Tanzania Daima toleo namba 2958 kwa kuniita msaliti wa CHADEMA, natumiwa na CCM na kuwa nina mahusiano (natumiwa) na Wassira tena bila kunihoji mimi Juliana Shonza. Kwa maana hiyo wamenichafua na kunidhalilisha mbele ya umma wa watanzania.

Pili naomba kuweka wazi kwambanatarajia kuomba ufafanuzi wa kikatiba juu ya shutuma zilizotolewa kwenye vyombo vya habari dhidi yangu na bwana Wegesa Suguta (John heche) ili aseme ni aminisho lipi la kuthaminisha na kusakidikisha mtazamo wa maono yake ili bongo za watanzania zijue ukweli. Mimi Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA natangaza rasmi Mtela Mwampamba na Habib Mchange ni wanachama hai na halali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Hivyo nawaomba waendelee na kazizao za ujenzi wa chama kwenye majimbo yao na taifa kwa ujumla. Nawaomba wananchi na wanachama wote wa CHADEMA waendelee kuwa na imani dhidi ya vijanahawa. Kama mlivyomwamini Mwampamba na kumpa kura 32000 na kama mlivyo mwamini Mchange na kumpa kura 10,400 kwenye uchaguzi wa Ubunge mwaka 2010. Vivyo hivyo naowaombamuendelee kushirikiana nao kuhakikisha wanatimiza adhima ya ukombozi mwaka2015.

Wenu katika ujenzi wa demokrasia makini

Juliana Daniel Shonza

M/Kiti BAVICHA-Tanzania Bara.


Ndani CCM kuna kitengo kinaitwa BAVICHA. Mang'ana.... Binti kaondoka ila anataman BAVICHA kwani anajua huko aliko nyota inafifia. Utabaki kuwa king'amuzi...cha G-spo...
 
Ndani CCM kuna kitengo kinaitwa BAVICHA. Mang'ana.... Binti kaondoka ila anataman BAVICHA kwani anajua huko aliko nyota inafifia. Utabaki kuwa king'amuzi...cha G-spo...

Unawasumbua watumiaji wa simu una-Quote uzi wote ili iweje mijitu mingine bana.
 
na kasura chako cha kinyeti ssisiemu watakuchapa kweli angalia usijeishia na mimba isiyojua baba yake wazo tu
 
Mkuu angalau umepunguza hasira yangu juu ya huyu binti, kwakweli leo nahisi angenitafutia BAN tu.
wewe mbona povu linakutoka acha ujinga wewe.unaonekana unauchu sana na madaraka wakubwa wameona hufai unaleta habari zaakina nape hapa toka zako tutafute viongozi walio tukuka.nenda zako kalime kahawa

f
 
Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA anayeshiriki kikamilifu kwenye shughuli za UV-CCM na CCM, ikiwa ni pamoja na mikutano ya ndani na hadhara, kampeni, akiwa amevaa sare za CCM? Juliana ulitumwa? Basi kama wewe kweli ni Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA, CCM ina haki ya kukufukuza mara moja, kwani wewe ni msaliti; ulienda kuipeleleza.
Nape Nnauye unangoja nini kumfukuzilia mbali huyu msaliti, ndumilakuwili?
 
Last edited by a moderator:
Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA anayeshiriki kikamilifu kwenye shughuli za UV-CCM na CCM, ikiwa ni pamoja na mikutano ya ndani na hadhara, kampeni, akiwa amevaa sare za CCM? Juliana ulitumwa? Basi kama wewe kweli ni Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA, CCM ina haki ya kukufukuza mara moja, kwani wewe ni msaliti; ulienda kuipeleleza.
Nape Nnauye unangoja nini kumfukuzilia mbali huyu msaliti, ndumilakuwili?

Nape na Mwigulu wafukuze godoro lao?
 
Vipi hao Wanasheria wake anaowasiliana nao ili alishataki Gazeti la T.Daima na J.Heche?yaani haka kadada pimbi kweli...
 
Leo.......................!!!

Juliana Shonza;6846728]Ndugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache wanachadema mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.

Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.

Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.

Pili napenda kutoa himizo kwa wanaccm na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.

Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na chadema tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua chadema 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.

Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.

Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.

Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.

Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.

Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.

Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.

Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.

CCM umoja ni ushindi.

Viva CCM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom