Jukwaa la Katiba lawatolea uvivu wanaomshauri JK

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,351
33,187
JKK(25).jpg

Rais Jakaya Kikwete.


Jukwaa la Katiba kwa mara nyingine jana liliibuka na kusema kuwa watendaji wa serikali katika masuala ya sheria hapa nchini uelewa wao ni mdogo ndiyo maana wanamshauri vibaya Rais Jakaya Kikwete.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deusi Kibamba, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kuongeza kuwa sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyosainiwa na Rais mwishoni mwa mwaka jana imeonekana kuwa na makosa kipindi kifupi baada ya kusainiwa.
"Kutokana na ushauri mbaya kwa Rais Kikwete ndiyo maana serikali kwa kipindi kifupi imeandaa muswada mpya wa sheria kwa ajili ya kuvifanyia marekebisho baadhi ya vifungu katika sheria hiyo hata kabla haijaanza kutumika," alisema.
Alitoa mfano kuwa serikali imekubali kukifanyia marekebisho kifungu kilichokuwa kikiwazuia wanasiasa kuingia katika tume itakayoundwa na Rais kwa ajili ya kukusanya maoni ya wananchi.
Alisema kifungu hicho kilikuwa kinawazuia wanasiasa kuwa wajumbe wa tume hiyo lakini kufuatia na marekebisho yatakayofanywa sasa itawapa fursa hiyo.
Aidha, kifungu kingine kinachoratajiwa kufanyiwa marekebisho ni kile ambacho kinasema tume hailazimishi kuchukua maoni kutoa asasi wala kwa mtu yoyote.
Hata hivyo, Kibamba alimpongeza Rais Kikwete kwa kukubali kufungua milango kwa makundi ya kiraia, vyama vya siasa na wananchi wengine kufika kwake na kutoa maoni yao.
Alimuomba Rais Kikwete kusitisha zoezi la kuteua tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya Katiba mpya kwa madai kuwa bado wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha.
"Serikali tuliitaka itoe nakala milioni 20 na kuzisambaza kwa wananchi vijijini na mjini lakini zoezi hilo halijafanyika na serikali inafanya hivyo huenda kwa makusudi kabisa," alisema.
Alisema wanaharakati wamekuwa wakipiga kelele kwa muda mrefu kuhusu umuhimu wa wananchi kushirikishwa kwa kutoa maoni yao katika mchakato wa kupata Katiba mpya lakini serikali imekuwa ikiwapuuza.
Aliongeza kuwa hajui ni kwa nini serikali na watendaji wake wanaogopa kuandikwa kwa Katiba mpya ambayo inakidhi matakwa ya wananchi wote.



CHANZO: NIPASHE
 
DEUS KIBAMBA na njaa iliyokithiri..... nchi haiendeshwi kwa kelele za wanaharakati bali kwa sheria na taratibu zinazokubalika kikatiba.
 
DEUS KIBAMBA na njaa iliyokithiri..... nchi haiendeshwi kwa kelele za wanaharakati bali kwa sheria na taratibu zinazokubalika kikatiba.

Sheria na taratibu za katiba ipi ikiwa hii ipo mezani tayari kuchinjwa kutokana na ubovu wake?naamini tu kuwa. Fikra mpya zitaunda katiba mpya,ila kwa mwendo unaoutaka ni wazi kuwa katiba mpya itatoka kwenye katiba ya zamani which is too wrong
 
Back
Top Bottom