Jukwaa la katiba la nena kuhusu tume ya nchimbi

Bunguabongo

Member
Jan 12, 2011
27
22
Jukwaa la katiba limetoa tamko kuhusu tume ya Nchimbi. Tamko likisomwa na mwenyekiti wa jukwaa hilo limesema; "kwanza ile siyo tume ni kamati iliyoundwa na nchimbi, kamati hii haitambuliki. Jukwaa linamtaka RAISI aunde tume ya kuchunguza mauaji ya mwandishi DM. Nchimbi hawezi kuunda tume maana yeye, pamoja na IGP wake na jeshi lote la polisi linastahili kuchunguzwa. Jukwaa limeenda mbali zaidi kwa kuitaka tume itakayoundwa,baada ya uchunguzi kukamilika, ipeleke majibu Bungeni kwa ajiri ya kupata ushauri wa kibunge. Mwenyekiti alimalizia kwa kusema...hatudanganyiki!" Aidha jukwaa la katiba linaitaka serikari kutoa tamko la kuisaidia familia ya DM kuisaidia kwa muda wa miaka ishirini ili watoto wa marehemu mpaka wafikie umri wa kujitegemea. Kwa maoni yangu jukwaa limenena vizuri kabisa, kwa mujibu wa sheria na kwa kuangalia familia ya marehemu, mjane na watoto. source; Star TV, Habari ya saa nne asubuhi ya leo.
 
Hivi si nimesikia kina Hellen Kijo Bisimba wanampango wa kwenda ICC, nadhani huko ndio mahali sahihi, mi sina imani na magamba, bunge wala serikali wala mahakama, wote ndo wale wale waliokunywa uji wa mgonjwa!
 
mambo yote yapelekwe kwa fatou bensouda, the hague. jaji mwenyewe nani hapa? ihema na mbarouku.
 
Jukwaa la katiba limetoa tamko kuhusu tume ya Nchimbi. Tamko likisomwa na mwenyekiti wa jukwaa hilo limesema; "kwanza ile siyo tume ni kamati iliyoundwa na nchimbi, kamati hii haitambuliki. Jukwaa linamtaka RAISI aunde tume ya kuchunguza mauaji ya mwandishi DM. Nchimbi hawezi kuunda tume maana yeye, pamoja na IGP wake na jeshi lote la polisi linastahili kuchunguzwa. Jukwaa limeenda mbali zaidi kwa kuitaka tume itakayoundwa,baada ya uchunguzi kukamilika, ipeleke majibu Bungeni kwa ajiri ya kupata ushauri wa kibunge. Mwenyekiti alimalizia kwa kusema...hatudanganyiki!" Aidha jukwaa la katiba linaitaka serikari kutoa tamko la kuisaidia familia ya DM kuisaidia kwa muda wa miaka ishirini ili watoto wa marehemu mpaka wafikie umri wa kujitegemea. Kwa maoni yangu jukwaa limenena vizuri kabisa, kwa mujibu wa sheria na kwa kuangalia familia ya marehemu, mjane na watoto. source; Star TV, Habari ya saa nne asubuhi ya leo.
Kwa mtazamo wangu naona hakuna haja ya kumsahihisha NCHIMBI kuwa hakuunda tume bali ni KAMATI ye kasema ni ''tume'',
Hivyo tumtuhumu kwa kuunda tume kinyume na sheria kama alivyo alivyosema T.LISSU,ili ajue watu wapo makini zaidi yake na yeye ni KILAZA tu hajui chochote ndo mana anakurupuka kuunda tume hali ya kuwa hana sifa za kufanya hivyo
1/ Cheo chake hakina hadhi ya kufanya hivyo,
2/ Yeye mwenyewe ni kiongozi wa wizara inayo tuhumiwa kwa namna nyingine na yeye ni mtuhumiwa.
USHAURI:
a/ Mh NCHIMBI kaonesha udhaifu mkubwa sana na kama anataka kuheshimu utala bora anatakiwa aji uzuru haraka iwezekanavyo asisubiri kama mwenzie yuleee w/afya,
b/ Mh Raisi nae anapaswa kuwachukulia hatua mara moja hao vilaza vinginevyo nae hataeleweka.
 
Yaani Nchimbi anataka kutufanya sisi ni Wajinga? Mauaji aamrishe yeye halafu anatuundia "Tume" ya Kimagumashi! Hili lijamaa halijastuka tu kwamba Watanzania wengi tumesoma na tunauwezo mkubwa wa kuelewa kuliko yeye? Hili jamaa hamna kitu. Angoje tu The Hague inamwita.
 
Back
Top Bottom