Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,454
- 3,416
Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe walienda uwanjani hapo na baadaye kudai kuwa walizuiwa kuingia Uwanjani kwa ajili ya kuuaga mwili wa Mkapa
Katika Ufafanuzi wao CHADEMA huku wakiitaka Serikali itoe ufafanuzi kwa kuzuiwa kwao wamedai wao wamefuata ratiba waliyopelekewa ikionesha tarehe, muda, siku tukio na muhusika
Hata hivyo, Jana Msemaji wa Serikali aliweka bayana ratiba ya kufika uwanjani hapo ambapo Serikali iliwataka Viongozi wote wa Kitaifa na Viongozi wa Kisiasa kufika katika Uwanja wa Karimjee na kuacha magari yao hapo kukiwa na gari maalum la kuwapeleka uwanjani ambapo la mwisho liliondoka saa 1:30 asubuhi